Ndugu, hawa watu siyo wabaya kuoa na hata Mungu anaruhusu jambo hilo, ila tatizo aina ya hawa singo maza tulio nao Leo wenye namba na mawasiliano ya hao wanaowaita washawaumiza kimapenzi na kuwatelekeza ndo shida ya kwanza ilipo.
Pili hiyo familia unailea vipi na hao ndg wa watoto wa uzao wako bila wao kubaguana, hapo sitaki kufafanua ila ugumu utakuja kuuona mwenyewe mbeleni.
NB; ukiwa kama kijana aidha wa kiume/kike epukeni kuwa na mtoto kabla ya ndoa kamili hata kama una uwezo wa kumlea, ni tatizo litakalotafuna maisha yako yote, hakuna mzazi/ndg/rafiki mwenye mapenzi mema atakayekushauri kuoa/kuolewa na single mother/father.