Nasemaje ikome...
Kuzaa azae mwingine kukereka akereke mwingine inahusu? Wameachana, wamekataliwa, wamepata mimba kwenye starehe, wamepata kwa mume wa mtu.its non of your business!
Unakuta mwanaume mzima na kende zako kubwa ka machungwa ya supermarket kutwa umekaa kumsimanga mwanamke kisa kazaa ulitaka awe mgumba?
Kuzaa kazaa yeye, analea mwenyewe.anasomesha mwenyewe ila we kutwa kuongea kinachokukera nini hasa?
Sikiliza nkwambie..mama ni msingi! Msingi wa watoto na familia kwa ujumla. Jiulize kwanini familia nyingi mama akifa familia inayumba sana na kusambarathata?mabalaa hayaishi. Inakosa furaha na uchangamfu kama mwanzo? Mama ni msingi wa malezi mema, ulinzi, furaha, mafanikio, baraka nk. Mama akikosekana watoto wanayumba
Kama msingi wako ulisimama mpaka Leo umekomaa jibaba zima.basi usitikise wa mwenzio tafadhali.yule kichanga ni binadamu mwenzio pia.malezi mema ulopitia nae anayahitaji.
Kama we unavyompenda mamako.nae ana upendo kwa mamake. Kama unavyoombea mamako aishi umri mrefu Nae anatamani kuendelea kumuona. Inashangaza mwanamke tangu ana mimba mpaka anajifungua ni maneno tu masimango tu mpaka wanakua frustrated, wana huzuni, wanaweza pata hata magonjwa ya moyo kama si kujikaza.
Kama unavyouheshimu msingi wako.uheshimu wa mwenzio. Kama unavyoupenda wako, nae anaupenda wake. Kama hupendi kuona wako ukitikiswa tena ukiwa tayari umekomaa usitikise wa mwenzako ambae bado hata hajakomaa na anauhitaji kwa asilimia kubwa kuliko wewe.
Nadhani nimeeleweka