Hapo kwenye paragraph ya mwisho wahanga ni wengi sana.
Kuna demu mmoja tumekuwa nae kitaa kimoja, tangu akiwa mdogo alikuwaga anatamani sana kuzaa na mzungu, yaani yeye ndoto zake alikuwa anasema ni lazima aje kuolewa na mzungu au ikishindikana kuolewa basi hata kuzaa nae tu.
Alikuwa anatamani sana kuwa na biracial child, ukicheki simu yake unakuta amejaza picha za vitoto vizuri vizuri tu kama vile vya Mabeste.
Sasa baada ya kuona hakuna uwezekano wa kumpata mzungu ikabidi ajipachike kwa chalii mmoja wa kiarabu anauza spare parts za piki piki, akajibebesha na mimba kabisa ya yule mwarabu.
Baada ya mwarabu kupewa taarifa za ujauzito alichomwambia yule demu ambaye mimi ni kama dada yangu aende akaitoe ile mimba, akampa na hela kabisa ya kutolea mimba. Yule sister alivyo ambiwa hivyo alimtukana sana yule mwarabu akasema mimba hatoi kama ni kulea atalea mwenyewe na ukawa ndio mwisho wa mahusiano yao.
Baada ya sister kujifungua alimuita yule mwarabu amuone mtoto wake, mwarabu akamwambia hamtambui yule mtoto kama ni wake akampa na vitisho vingi sana.. Sister akakubali yaishe na hakumsumbua tena.
Imepita miaka minne sasa tangu hilo tukio litokee mwarabu alishaoa mwarabu mwenzie wala hana habari na mtoto aliyezaa na sister, na sister nae hana habari na mwarabu kabisa.
Anachojivunia tu sasa hivi huyo dada yangu ni kupata katoto kazuri. Ila ana shida kibao yeye na mwanae, last time nimeenda home nilivyoonana nae aliniomba nimsaidie 50k, nilipojaribu kumuuliza kuhusu baba wa mwanae kama anawajibika akanijibu "hebu naomba usinilize".
Na hawa ndio aina ya single mothers wa miaka ya leo hii, they're the victims of their own stupid mistakes.