Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Nakubaliana nawe kabisa- ukiongea uzuri unataja na kujuza ubaya pia. Kwa kuzingatia hayo utaona mapungufu ya Mongella kule Arusha ambayo yanalengwa yakatekelezwe na Makonda.
Paskal hata hivyo RJMT amesema mabadiliko mengi msingi wake ni kuboresha utendaji akimaanisha hakuna makosa makubwa- ni tactical based reshuffles
 
Openness and Transparency after the Fact ? Yaani unafanya vyovyote unavyofanya alafu unatoa maelezo kwanini umefanya ?

Kwangu mimi angeonyesha Transparency kwenye ile Mikataba / Makubaliano ambayo impact yake ni mpaka vizazi na vizazi ndio ingekuwa jambo lenye National Interest (Hayo mengine ya panga pangua naona kama matumizi mabaya ya Kodi zetu)
 
Mbona ipo?
 
Mbona ipo?
Transparency kwenye mikataba ipo ?

Kwamba kabla ya haya makubaliano ya Bandari kuvuja kuna aliyejua ? Kwamba Mkataba wa Bagamoyo amabyo JPM alisema tunapigwa wengine wakabisha hatupigwi mpaka leo kuna anayejua ukweli ni upi ?

Kwamba mkataba wa Bandari ambao ulikuwa ni kuangalai uwezo kwa miaka mitano alafu ikiwa poa waongeze miaka kumi itaongezwa mpaka miaka kumi na tano hata kabla ya mitano kuisha kuna aliyefahamishwa ?
 
Hayo yote ni ctr + c na ctrl + v kutoka kwa Magufuli hakuna jipya hapo.Tena Magu alikuwa anakueleza na makosa yako kabisa
 
Hi habari ya kuvuja ni dhana ya ajabu sana kwa sababu
1. MoU zilitajwa rais aliporudi kutoka ziara ya UAE.
2. Kwenu msiojitegemea ki akili mlianza kujua MoU na IGA baada ya serikali kuipeleka bungeni na kwa kawaida serikali ikipeleka jambo bungeni hilo tayari ni la jumia yote. Hii ilifanyika kati ya 4/5 ya mwezi husika na Mbowe akawambianyie waumini wake 7 ya mwezi huu (NOTE SINA HAKIKA SANA).
 
Unajua maana ya total transparency mkuu ? Ninachosema hii mali ni ya UMMA kwahio mikataba yote inayohusu hii mali iwe open na kwa lugha rahisi kwa kila mwenye macho aweze kusoma akitaka na kuelewa hata bibi yangu kule kijijini akihitaji aweze kusoma na kuelewa

Haya mambo ya Usiri wa mikataba ndio yanayoendelea kutuingiza Chaka....
 
Labda unisaidie na tena unisaidie kwa mifano hiyo total transparency ni kitu gani na inatekelezwa nchi gani? Nina hakika mkeo/mmeo hajui mapato yako na nyinyi ujmla wenu ndiyo Tanzania.
 
Labda unisaidie na tena unisaidie kwa mifano hiyo total transparency ni kitu gani na inatekelezwa nchi gani? Nina hakika mkeo/mmeo hajui mapato yako na nyinyi ujmla wenu ndiyo Tanzania.
Kwahio ikifanyika / isipofanyika nchi fulani na sisi tusifanye... unaongelea mapato yangu Je mapato ya nchi na rasilimali za nchi ni mali za watawala wa kipindi hicho ?

Nikiingia mkataba mimi mwenye mali kama nina nyumba au shamba langu ndio nitaelezewa kila kitu kinachohusu huo mkataba haya mambo ya siri ya mikataba yameletwa / yaliwekwa kwenye trade secrets (kutokuweka wazi siri za kibiashara) jambo ambalo kwenye mambo haya ya rasilimali za nchi hayapo (kwahio usifananishe mapato yangu na mwenye mali / mwananchi kutokujua anaingia mikataba ya aina gani na anagawa nini kwa gharama ambayo hata wajukuu zake watalipia...
 
nadhani tunapotezeana mda- kaa na ndoto zako nami nibaki na uhalisia wa dunia
 
nadhani tunapotezeana mda- kaa na ndoto zako nami nibaki na uhalisia wa dunia
Uhalisia wa dunia ni mzuri kubakia na status quo kama wewe umeshika mpini na sio kwenye makali (uhalisia wa dunia kwa sasa ndio unafanya Afrika kuwa shamba la bibi) Hao so called wawekezaji wanapenda sana watu kama wewe wa kuendelea na uhalisia..., Na Watu wangeendelea kuwa na Uhalisia wa wakati husika mpaka leo tungekuwa tunasujudia wachache kwamba ndio wana damu ya ufalme hence haki yao ni kututawala....
 
Wafalme ndiyo walikuwa watawala halisi na sahihi at least based on religion, sociology, and anthropology knowledge available. Kura haziwezi kutoa mtawala halisi na sahihi. Kweney vitabu vya dini upo ushahidi - mungu alishagawa talanta akamaliza; wewe alikupa ya kibishana humu na kuonea wenzako wivu, chuku na akili mbovu.
Mkuu, angalia mpira wa miguu, yupo Messi wenzake wote wanaheshimu talanta yake wala hawawazii ukubwa wa malipo anayopewa. Hapa Yanga na Simba ukimleta Messi ukamalipa kuliko wenzake , wenzake watasusa kumpa pasi na kumwambia acheze mwenyewe kwa vile yeye ndiye analipwa malipo makubwa kuliko wote. NDIYO AKILI YAKO.
Walioko serikalini wnadhamana ambayo wewe huna- usijifananishe nao.
 
Huo ni mtizamo wako wala siwezi nikakubishia ila hii ni argument tofauti na ya siku nyingine lakini just imagine apatikane mfalme ambaye hana Hekima na anachukia tuseme watu weusi and you happen to be mtu mweusi katika jamii hio nadhani hapo utaimba a different tune ya unayoimba sasa hivi
Wewe unaongelea individuals na watu mimi naongelea mifumo - Messi na umahili wake hawezi kucheza peke yake wala hatusemi sababu ni Messi basi asiambiwe kitu... by the way Hii inaingiliana vipi na mimi kusema mikataba yote iwe wazi (Total Transparency Nukta kwa Nukta) ? Kwamba ikiwa wazi waliko Serikalini hawatafanya kazi yao ?

Ni kina nani wameingia Mikataba ya Kimangungo na mingine ambayo inabidi ivunjwe kutokana na kwamba haifai na inavunjwa kwa gharama kubwa (kama sio hao hao unaosema walipewa talanta na wapo Serikalini) ? Okay basi waendelee kufanya wanachofanya lakini kifanyike kwa UWAZI sababu hii ni Mali ya Wananchi wote wa Sasa na vizazi vijavyo...
 
Mkuu mifumo ni zao la individuals in their totality
 
Mkuu mifumo ni zao la individuals in their totality
Mifumo mizuri haijalishi ni nani at a given time yupo incharge hata asipokuwepo mtu bado itakwenda bila shida yoyote, na ni either mifumo ni mizuri au mibaya na ubaya au uzuri unajulikana tu kwa kuangalia Pro and Cons...; Sasa wewe niambie kuna ubaya gani wa jambo lolote linalohusu Mali ya Taifa (wenye mali ambao ni wananchi) wasijue yote yanayohusu mali zao ? Yaani hio Mikataba iwe translated kwa lugha nyepesi hata layman kitaa akitaka ajue what is what....
 
Haiondoi generic notion that- mfumo ni zao la individuals in their totality and once the mifumo are in place they exist outside the individual and control them.
Mali ya taifa iko chini ya wenye dhamana waliopata hiyo dhamana kutokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii nzima.
 
Haiondoi generic notion that- mfumo ni zao la individuals in their totality and once the mifumo are in place they exist outside the individual and control them.
What does this even mean... tunapoongelea mfumo wa Upumuaji hatuongelea mapafu peke yake au pua au haimaanishi pua inaweza kujiamulia kufanya inachofanya....,Na haimaanishi kwamba mapafu yakifeli hatuwezi kutumia mashine kusaidia upumuaji - In the end whats important ni exchange of oxygen and carbon dioxide....... (na kwenye lecture at hand whats matters ni jinsi gani tunaweza kuhakikisha rasimali za vizazi vyote (future and present) hatuvifuji kwa upuuzi wa wachache
Mali ya taifa iko chini ya wenye dhamana waliopata hiyo dhamana kutokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii nzima.
Kwamba Jamii nzima ilikubaliana mali yao wenye dhamana wafanye wanachofanya bila consultation au ka usiri ?; Wakati wa Utumwa Je watumwa walikuwa consulted ? Je chochote kinachoendelea kwa wakati husika kimekubaliwa na Jamii nzima ?
 
Nikisema wenye dhamana waliotokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii unaona kama kweli ulikuwepo wakati wa utumwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…