Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Wanabodi,
Jana niliangalia tukio la uapisho wa wateule wapya, Ikulu Dar es Salaam, na nilifarijika sana kuona miongoni mwa waalikwa wa tukio lile, ni Mzee wa Ngomeni, Richard Mwasha kwa jina maarufu la Kuhani Musa.

Nimefarijika sana kumuona Rais Samia akitoa sababu za kumteua kila aliyemteua na kumpa majukumu kwa uwazi kabisa.

Enzi za Kikwete, Tanzania tulisaini ule mkakati wa Open Government Initiative uliokuwa unasisitiza ukweli na uwazi, truth and transparency, JPM alipoingia, aliufuta mkakati huo, hata Bunge live likafutwa, mikutano ya vyama vya siasa ikapigwa marufuku na hata mikutano ya ndani kuzuiwa.

Rais Samia alipoingia, na falsafa yake ya 4R, akafanya mabadiliko mengi makubwa ikiwemo kufungulia mikutano ya siasa.

Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na wasaidizi wake, lakini kwenye kufikia maamuzi, rais anafikia uamuzi yeye kama yeye, na halazimiki kufuata ushauri wa yeyote, na hawajibiki kutoa sababu yoyote ya maamuzi yake.

Powers za rais kuteua na kutengua zinaitwa discretion powers, kwa rais kuteua, kutengua au kutumbua bila kutaa sababu yoyote kwa yeyote.

Hivyo kitendo cha Rais Samia kuwa open and transparent kwa kueleza sababu za kumtea fulani mahali fulani na kumpa majukumu kwa uwazi, hii ni hisani kubwa na nzuri kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Anachokifanya rais Samia kuwa muwazi, open and transparent sababu za kuwateua wateule wake, ni hisani tuu, tena hata uapisho live Mubashara kisha kutolewa hotuba, kumeanza na JPM, zamani hatukuwahi kuwa na hotuba kwenye uapisho, ni kuapa tuu and that was it.

Kitu kizuri zaidi, sio tuu rais Samia anakuambia kwanini amekuteua, bali anaelekeza uende ukafanye nini!. Mfano RC Makonda amepewa special task Arusha, jiji la kitalii, hivyo anapaswa kwenye kukuza Utalii, ila pia kuna maelekezo mengine ya kuyashughulikia na Kuwashughulikia ikiwemo issues za wale machalii wa RChuga na 'cha Arusha".

Yule RC wa Mara ambaye ni mjeshi, kaelekezwa kwenda kushughulikia kijeshi jeshi kile kilimo cha lile zao, (hakulitaja) ambalo Mara ni maarufu na kulivusha mpakani na nchi jirani.

Hiki anachofanya Ras Samia ni sawa na ile Open Government Initiative, kwa mteuliwa kupewa changamoto openly and transparently, akishindwa ku deliver
The public yote itajua hivyo hiki ni kitu kizuri kwa uwajibikaji.

Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, au kupata taarifa, the right to information act, hivyo wananchi kuelezwa kila kinachowahusu ni haki yao na sio hisani.

Kwa vile Rais Samia ameisha onyesha njia kwa Kutuhisania, tuwe watu wa shukrani kwanza kwa kumshukuru kwa hiyo hisani tuu kwanza, kisa sasa tumuombe atupe na haki ya kupata taarifa, asiishie kwenye kutupatia taarifa za uteuzi tuu, tupatiwe na taarifa za sababu za utenguzi kwasababu maofisa hao ni watumishi wa umma, wanaolipwa na fedha za umma, hivyo umma una haki zote za kujua kuhusu utendaji wa wateule hao, na sababu za kutenguliwa kwao na kutumbuliwa.

Mfano Paul Makonda, baada ya kuteuliwa Mwenezi wa CCM, amefanya wonders katika kipindi kifupi na kurejesha imani ya wananchi kwa CCM, kwa kuwakimbiza viongozi mchaka mchaka, wengi wakitaraji mchaka mchaka huo ungeendelea hadi 2025, katika uchaguzi Makonda aingie Bungeni, na kupewa Wizara nyeti, lakini mara ghafla Makonda kama Mwenezi, akatumbuliwa!.

Mtu yoyote mwenye cheo kikubwa, akaondolewa na kuteuliwa cheo kidogo ni kutumbuliwa tuu!, hivyo Makonda ametumbuliwa uenezi na kupoozwa na u RC, Dr. Bashiru Ali Kakurwa alitumbuliwa uenezi na kupoozwa na ubunge wa kuteuliwa. DGIS wametumbuliwa mara kadhaa na kupoozwa na ubalozi, wengine wakitumbuliwa wanasugua bench, kama Balozi Liberata Mulamula, Prof. Kabudi, William Lukuvi na wengine wengi, the public has the right to know sababu, na sio kusubiria kuhisaniwa.

Kama ilivyo sifa njema kuteuliwa, mtumishi wa umma akiboronga, the public ielezwe!.

Tena kwa maoni yangu, nafasi za juu zote wakiwemo wakuu wa mihimili, Jaji Mkuu, Spika na wakuu wa zile independent organs zote, nafasi zinapokuwa wazi, Watanzania wenye sifa waombe, washindanishwe tupate the best ndipo rais apelekewe kuteua, na sio huu utaratibu wa sasa wa watu kuokotana, kuteuana na baada ya siku mbili kutenguliwa, haileti picha nzuri sana kwa awamu hii ya Rais Samia.

Nchi nyingi wakiwemo jirani zetu Kenya, Jaji Mkuu, anaomba kazi, anasailiwa, the best amechaguliwa.

Nimalizie kwa kumpongeza tena Rais Samia kwa kutuhisania openness and transparency kwenye teuzi zake, openness hii na transparency hii tuifanye na haki na sio hisani.

Wasalaam

Paskali
Nakubaliana nawe kabisa- ukiongea uzuri unataja na kujuza ubaya pia. Kwa kuzingatia hayo utaona mapungufu ya Mongella kule Arusha ambayo yanalengwa yakatekelezwe na Makonda.
Paskal hata hivyo RJMT amesema mabadiliko mengi msingi wake ni kuboresha utendaji akimaanisha hakuna makosa makubwa- ni tactical based reshuffles
 
Openness and Transparency after the Fact ? Yaani unafanya vyovyote unavyofanya alafu unatoa maelezo kwanini umefanya ?

Kwangu mimi angeonyesha Transparency kwenye ile Mikataba / Makubaliano ambayo impact yake ni mpaka vizazi na vizazi ndio ingekuwa jambo lenye National Interest (Hayo mengine ya panga pangua naona kama matumizi mabaya ya Kodi zetu)
 
Mbona ipo?
 
Mbona ipo?
Transparency kwenye mikataba ipo ?

Kwamba kabla ya haya makubaliano ya Bandari kuvuja kuna aliyejua ? Kwamba Mkataba wa Bagamoyo amabyo JPM alisema tunapigwa wengine wakabisha hatupigwi mpaka leo kuna anayejua ukweli ni upi ?

Kwamba mkataba wa Bandari ambao ulikuwa ni kuangalai uwezo kwa miaka mitano alafu ikiwa poa waongeze miaka kumi itaongezwa mpaka miaka kumi na tano hata kabla ya mitano kuisha kuna aliyefahamishwa ?
 
Hayo yote ni ctr + c na ctrl + v kutoka kwa Magufuli hakuna jipya hapo.Tena Magu alikuwa anakueleza na makosa yako kabisa
 
Transparency kwenye mikataba ipo ?

Kwamba kabla ya haya makubaliano ya Bandari kuvuja kuna aliyejua ? Kwamba Mkataba wa Bagamoyo amabyo JPM alisema tunapigwa wengine wakabisha hatupigwi mpaka leo kuna anayejua ukweli ni upi ?

Kwamba mkataba wa Bandari ambao ulikuwa ni kuangalai uwezo kwa miaka mitano alafu ikiwa poa waongeze miaka kumi itaongezwa mpaka miaka kumi na tano hata kabla ya mitano kuisha kuna aliyefahamishwa ?
Hi habari ya kuvuja ni dhana ya ajabu sana kwa sababu
1. MoU zilitajwa rais aliporudi kutoka ziara ya UAE.
2. Kwenu msiojitegemea ki akili mlianza kujua MoU na IGA baada ya serikali kuipeleka bungeni na kwa kawaida serikali ikipeleka jambo bungeni hilo tayari ni la jumia yote. Hii ilifanyika kati ya 4/5 ya mwezi husika na Mbowe akawambianyie waumini wake 7 ya mwezi huu (NOTE SINA HAKIKA SANA).
 
Unajua maana ya total transparency mkuu ? Ninachosema hii mali ni ya UMMA kwahio mikataba yote inayohusu hii mali iwe open na kwa lugha rahisi kwa kila mwenye macho aweze kusoma akitaka na kuelewa hata bibi yangu kule kijijini akihitaji aweze kusoma na kuelewa

Haya mambo ya Usiri wa mikataba ndio yanayoendelea kutuingiza Chaka....
 
Labda unisaidie na tena unisaidie kwa mifano hiyo total transparency ni kitu gani na inatekelezwa nchi gani? Nina hakika mkeo/mmeo hajui mapato yako na nyinyi ujmla wenu ndiyo Tanzania.
 
Kwahio ikifanyika / isipofanyika nchi fulani na sisi tusifanye... unaongelea mapato yangu Je mapato ya nchi na rasilimali za nchi ni mali za watawala wa kipindi hicho ?

Nikiingia mkataba mimi mwenye mali kama nina nyumba au shamba langu ndio nitaelezewa kila kitu kinachohusu huo mkataba haya mambo ya siri ya mikataba yameletwa / yaliwekwa kwenye trade secrets (kutokuweka wazi siri za kibiashara) jambo ambalo kwenye mambo haya ya rasilimali za nchi hayapo (kwahio usifananishe mapato yangu na mwenye mali / mwananchi kutokujua anaingia mikataba ya aina gani na anagawa nini kwa gharama ambayo hata wajukuu zake watalipia...
 
nadhani tunapotezeana mda- kaa na ndoto zako nami nibaki na uhalisia wa dunia
 
Uhalisia wa dunia ni mzuri kubakia na status quo kama wewe umeshika mpini na sio kwenye makali (uhalisia wa dunia kwa sasa ndio unafanya Afrika kuwa shamba la bibi) Hao so called wawekezaji wanapenda sana watu kama wewe wa kuendelea na uhalisia..., Na Watu wangeendelea kuwa na Uhalisia wa wakati husika mpaka leo tungekuwa tunasujudia wachache kwamba ndio wana damu ya ufalme hence haki yao ni kututawala....
 
Wafalme ndiyo walikuwa watawala halisi na sahihi at least based on religion, sociology, and anthropology knowledge available. Kura haziwezi kutoa mtawala halisi na sahihi. Kweney vitabu vya dini upo ushahidi - mungu alishagawa talanta akamaliza; wewe alikupa ya kibishana humu na kuonea wenzako wivu, chuku na akili mbovu.
Mkuu, angalia mpira wa miguu, yupo Messi wenzake wote wanaheshimu talanta yake wala hawawazii ukubwa wa malipo anayopewa. Hapa Yanga na Simba ukimleta Messi ukamalipa kuliko wenzake , wenzake watasusa kumpa pasi na kumwambia acheze mwenyewe kwa vile yeye ndiye analipwa malipo makubwa kuliko wote. NDIYO AKILI YAKO.
Walioko serikalini wnadhamana ambayo wewe huna- usijifananishe nao.
 
Huo ni mtizamo wako wala siwezi nikakubishia ila hii ni argument tofauti na ya siku nyingine lakini just imagine apatikane mfalme ambaye hana Hekima na anachukia tuseme watu weusi and you happen to be mtu mweusi katika jamii hio nadhani hapo utaimba a different tune ya unayoimba sasa hivi

Wewe unaongelea individuals na watu mimi naongelea mifumo - Messi na umahili wake hawezi kucheza peke yake wala hatusemi sababu ni Messi basi asiambiwe kitu... by the way Hii inaingiliana vipi na mimi kusema mikataba yote iwe wazi (Total Transparency Nukta kwa Nukta) ? Kwamba ikiwa wazi waliko Serikalini hawatafanya kazi yao ?

Ni kina nani wameingia Mikataba ya Kimangungo na mingine ambayo inabidi ivunjwe kutokana na kwamba haifai na inavunjwa kwa gharama kubwa (kama sio hao hao unaosema walipewa talanta na wapo Serikalini) ? Okay basi waendelee kufanya wanachofanya lakini kifanyike kwa UWAZI sababu hii ni Mali ya Wananchi wote wa Sasa na vizazi vijavyo...
 
Mkuu mifumo ni zao la individuals in their totality
 
Mifumo mizuri haijalishi ni nani at a given time yupo incharge hata asipokuwepo mtu bado itakwenda bila shida yoyote, na ni either mifumo ni mizuri au mibaya na ubaya au uzuri unajulikana tu kwa kuangalia Pro and Cons...; Sasa wewe niambie kuna ubaya gani wa jambo lolote linalohusu Mali ya Taifa (wenye mali ambao ni wananchi) wasijue yote yanayohusu mali zao ? Yaani hio Mikataba iwe translated kwa lugha nyepesi hata layman kitaa akitaka ajue what is what....
 
Haiondoi generic notion that- mfumo ni zao la individuals in their totality and once the mifumo are in place they exist outside the individual and control them.
Mali ya taifa iko chini ya wenye dhamana waliopata hiyo dhamana kutokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii nzima.
 
What does this even mean... tunapoongelea mfumo wa Upumuaji hatuongelea mapafu peke yake au pua au haimaanishi pua inaweza kujiamulia kufanya inachofanya....,Na haimaanishi kwamba mapafu yakifeli hatuwezi kutumia mashine kusaidia upumuaji - In the end whats important ni exchange of oxygen and carbon dioxide....... (na kwenye lecture at hand whats matters ni jinsi gani tunaweza kuhakikisha rasimali za vizazi vyote (future and present) hatuvifuji kwa upuuzi wa wachache

Kwamba Jamii nzima ilikubaliana mali yao wenye dhamana wafanye wanachofanya bila consultation au ka usiri ?; Wakati wa Utumwa Je watumwa walikuwa consulted ? Je chochote kinachoendelea kwa wakati husika kimekubaliwa na Jamii nzima ?
 
Nikisema wenye dhamana waliotokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii unaona kama kweli ulikuwepo wakati wa utumwa?
 
Back
Top Bottom