Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Pamoja na yote kwa hali ya amani inayoendelea kuwapo, itakuwa ni kukosa uelewa kutompa pongezi binafsi afande IGP Simon Sirro. Hii zaidi ikiwa kwa jinsi alivyo lidhibiti jeshi la polisi vilivyo tangia kuwasili kwa bwana Tundu Lissu hadi hii leo. Kwa hakika Sirro ni IGP wa watu.
Ni wazi kuwa wapo kina mamboleo, kina mutoro na wale kama yule bwana wa Mbeya ambao wangependa mno kufanya yao kwa minajili ya kujipendekeza tu.
Kamanda Sirro amekuwa muda wote macho kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani wala wa sheria pasipo na kujali makunyanzi. Siyo siri tena kuwa tunayoyaona ni jitihada binafsi za kamanda Sirro.
Kwa hakika so far so good - na amang'ana mbuya, mura!
Heko Tundu Lissu na wafuasi wako kwa kuzingatia sheria na taratibu zote zilizopo kwani ndani ya changamoto zilizopo, kwa hakika mmeufanya utendaji wa kamanda Sirro na polisi wake kuwa ni wenye tija kubwa.
Ni dhahiri kuwa "sote kwa pamoja tunaweza!"
Ifahamike kuwa hata Prof. Juma na mh. Jaji Kaijage kwa niaba ya mahakama na tume, kama alivyo Sirro mnayo sehemu yenu na uhuru wa kutosha kuhakikisha kuwa amani inadumishwa hapa nchini. Kwa kutojipendekeza tu, kama wale wajenga maofisi Chatto, nanyi pia mnaweza kutia mchango wenu mkubwa na wa kutosha tu. Mbona Sirro ameweza?
Mahakama na Tume ya uchaguzi tupeni raha kwa kutumia busara zenu kama wanadamu tu.
Wakuu wa mahakama na tume mliteuliwa kusaidia kuiweka nchi salama na kwa hakika inawezekana. Yawezekana kuwa haupo muda ulio bora kuisadia hii nchi katika hilo labda juliko ulivyo muda huu. Kwani wasiotutakia wale mabingwa wa kukaanga mbuyu sasa hivi hawalali.
Macho yetu yote kwenu. Tunaamini inawezekana na kuwa hamtatuangusha.
Sirro ametutoa kimasomaso dhidi ya wabaya wetu hao ambao wangependa mno kutuona tukitoana macho na kuuwana. Chonde chonde mahakama na tume tusaidiane sote kudumisha amani.
Kinachoombwa kwenu ni kutenda haki na kwa uwazi tu kwa wagombea wote. Kwa hakika tunayowaomba si makubwa kwani kimsingi tunawaomba kutekeleza wajibu wenu tu na wala si zaidi hapo.
Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa
Wito: Chonde chonde, Tanzania ni zaidi mno ya yeyote