Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu

kama watanzania wangekua na akili timamu wangejua kabisa ambaya yanaendelea baada ya uchaguzi

haya yanayofanywa na polisi ni maagizo pia,sababu serikali inajua wazi kabisa kwamba wananchi hawajawahi kuwa chanzo cha vurugu,bali wao na jeshi la polisi na vyombo vya usalama

mbona sahivi jeshi limekua na weledi ghafla?!...kumbe huwa ni makusudi,na inafahamika kwamba baada tu ya uchaguzi hali itarudi vile kama mwanzo,isiwadanganye hii hali...Siro hana weledi wowote,ni anatumiwa tu kwa remote na anafata,angekua mweledi angesimama hata kipindi cha baada ya uchaguzi.
 
Police wetu wakiamua wanafanya kazi yao vizuri.
 

Bandiko hili halipaswi kupita pasipo kuungwa mkono! Asante sana kwa angalizo ulilotoa. Naamini watu wa system wanaopitia mandiko haya watafikisha ujumbe kwa wahusika.
 
Kaka hongera Sana kwa kukitambua hilo. Binafsi nimeona IGP Siro anastahili hii pongezi mpaka hapa tulipofikia.

Matarajio ya watu kwa yatakayotokea baada ya ujio wa Tundu Lisu ni tofaut na jinsi ilivyo Sasa. Kampeni zinaebdelea za kistaarabu kabisa Amani imetahamalaki . Hii ndio Tanzania yenye misingi ya Amani tangia tupate Uhuru

Niendelee kuvisii vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuhakikisha Amani inakuwepo, waangalie Uhuru wa watu kufanya yao ambayo hayavunji sheria za nchi.
Nawapongezeni Sana vyombo vya ulinzi na usalama
 
Ni kweli kabisa, jamaa anafanya kazi maana hata kiwango cha mapomu kimepungua. Ila mleta mada weka vizuri Tittle yako. Inaonesha kama unapongeza wote uliowataja. Ina ukakasi kimantiki
 

Pamoja na mashaka lakini Sirro hadi hapa kaonyesha njia na kuwa inawezekana.

Bado Juma na Kaijage. Tunaendelea kusubiri tukitambua kuwa wapo wanaotamani kuwa kama wangekuwa wao ni ma IGP!
 

..wapinzani wamedhihirisha kwamba wao ndio walinzi wa amani ya nchi yetu.

..maeneo yote aliyopita TL hakujatokea tukio lolote na uvunjifu wa amani.

..mara uvunjifu wa amani husababishwa na polisi wetu kukosa weledi, na mfano matukio ya kuuwawa kwa daudi mwangosi, na aquilina akwilini.
 
Mahakama kusimamisha kesi za Lissu tumeona haki inawezekana. Polisi pia tumeona.

NEC na ZEC mmegusa gusa mzizi wa fitina bado.

Tupeni raha kwa kutupa haki tu wana wa nchi hii.

Hii nchi ni yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…