Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
View attachment 2316635View attachment 2316636
Wana JF Wenzangu, hebu tuacheni ushamba!, Media kumpongeza Rais kwa kazi nzuri na kufanya vema, sio kujipendekeza au kujikombakomba kunyemelea uteuzi!, rais wetu pia ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, akifanya vema, anastahili pongezi as encouragement, aendelee kufanya mazuri zaidi na zaidi, lakini baadhi ya watu humu kiukweli mnakera, sisi watu wa media, kila tukimpongeza rais kwa kufanya vema au mazuri yoyote, mnatuzodoa na kutunyooshea vidole kuwa pongezi hizo ni pongezi za kinafki kujipendekeza tuu ili kusaka uteuzi!.
Tangu rais Samia ameingia madarakani amefanya mengi makubwa mazuri ya kustahili sifa na pongezi za dhati, lakini pia Rais Samia sio malaika, hivyo anaweza kukosea na tutamkosoa!. Hivyo katika mazuri, nami nimempongeza kwa mengi, lakini nakereka kila nikipongeza nabezwa kuwa nafukuzia uteuzi!, hivi watu mnaona pongezi tuu?, critics hamzioni?.
Jana Rais Samia kateua majaji wapya 22 wa mahakama Kuu, katika uteuzi huo majaji 11 ni Wanawake na 11 ni wanaume, nikapandisha bandiko la pongezi
Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?
wale wazodoaji wakaniibukia eti ni bandiko la kujipendekeza, eti kwa vile sifa za kuwa jaji ni kuwa na LL.B, na mimi ninayo, sasa naupumulia u Jaji!. Acheni hizo!.
Haya sasa Mungu bariki, mimi niko Mbeya, kwenye maonyesho ya Nane Nane nikifanya Vipindi vyangu vya Nane Nane na PPR, na rais yuko Mbeya, ndiye mgeni Rasmi kwenye kilele cha Nane Nane, hivyo kesho ndio itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Rais Samia face to face, tangu Mungu alipomteua kuwa rais wetu, hivyo ikitokea katika pita pita za mabandani. ikitokea akapita karibu yangu, nitamsalimia kwa sauti kubwa tuu na atasikia, sijui kama atajibu, shikamoo yangu...
Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa DC, DED, RAS, RC, JAJI, or anybody!.
ila nikipata fursa ya kumsalimu kwa karibu, nitampa ukweli huu wa jinsi JF mnavyokera kwa kumweleza wazi kuwa pongezi zetu kwake kwa sisi baadhi yetu, ni pongezi bonafide genuine, kumpongeza kwa dhati kabisa kwa mazuri anayolifanyia taifa letu na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote licha
- Pascal Mayalla ni Mtanzania, anayekidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa na rais kushika wadhifa wowote kama U DC!. Siku zote nimekuwa nikisema sihitaji uteuzi, ila kuna mwana jf mmoja akauliza kama ikitokea ghafla mara pap... Pascal Mayalla umeteuliwa DC, Jee Utakataa?. Nilishindwa kujibu!, Ukiteuliwa ukikataa utaonekana ni mtovu wa nidhamu!. Ili kuzuia utovu wa nidhamu, ni vizuri uki declare interest wazi, openly na publically, Pascal Mayalla hahitaji uteuzi wa kuwa DC!.
- Kwenye uteuzi wa Majaji wapya, mmoja wa majaji wapya ni mwandishi wa habari binti, tulimpokea pale RTD, tukamfundisha kazi, akaenda kusoma sheria, akawa wakili wa kujitegemea juzi kateuliwa Jaji. Mimi pia nimesoma sheria, tena LL.B yangu ni LL.B (HONS) ya UDSM, hivyo ninakidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa kuwa Jaji, lakini naomba kukiri, siwezi kumhukumu mtu kifo, hivyo siwezi kuwa Jaji na naomba nisiteuliwe kuwa Jaji!.
Japo Kuna Wengi Wanapenda Uteuzi, Lakini Kuna Watu wa Ajabu!, Hawataki Kabisa Uteuzi wala Kazi za Malipo Manene!.
Kuteuliwa wadhifa wowote na rais wa JMT ni heshima kubwa, hivyo wateuliwa hufurahi kuheshimishwa, hivyo kuna wengi wanautamani sana u DC, U DAS, DED RC etc, amini usiamini, kuna watu fulani ambao hawazimikii kabisa uteuzi wowote wa ubwete!, au kazi za malipo manene!. Watu hao sio tuu ni wazuri at what they do, but they love what they do, and they are the best at what they do, ukiwateua watu hawa na kuwa u DC, japo u DC ni cheo kikubwa, lakini uki compare watakacho fanya kwenye U DC compared to what they do, it's a waste!. Just imagine unamchukua mtu kama Profesa wa Chuo Kikuu kama Prof. Shivji, ateuliwe DC!.
Mimi ni mtu wa mastory mastory, wale wa mastory, tuendelee, wale wa short and clear, nenda mwisho.
Rais wetu Mama Samia, ameonyesha kwa kauli, maneno na matendo kuwa yeye ni mtu msikivu, na kuna mazuri mengi ameyafanya na anaendelea kuyafanya, yanayostahili pongezi. Sisi watu wa media, tukiandika jambo lolote zuri kumpongeza rais Samia kwa mazuri yake, tunanyooshewa vidole kuwa tunanyemelea uteuzi wa UDC, U RC au Ukurugenzi yaani U RAS au U DAS!. Kwa vile mimi ni Mtanzania na nina sifa za kustahili kuteuliwa nafasi yoyote ya uteuzi, kwa sababu ni haki yangu, kama Mtanzania, naomba ku declare publically kuwa mimi Pascal Mayalla, sipongezi kwa kutafuta uteuzi wowote wa u DC au u RC au Ukurugenzi, au uteuzi wowote wa Mama!.
Na kwa vile mimi niko Mbeya kwenye Nane Nane, na Mama Samia pia yuko Mbeya kuja kufunga Nane Nane, hapo kesho, ikitokea nikakutana na Mama Samia kesho kwenye Nane Nane,
Simulation ya encounter ya Pasco na Mama Samia
PM:“Sjikamoo Mama!...
RS : Marhaba Mwanangu.
PM: Nina Salaam zako kutoka JF!, akisimama, then nitampa salaam zake,
Asiposimama, then salaam zangu zitakuwa zimeishia hapo!.
Ikitokea amesimama, then nitampongeza kwa kazi nzuri!, na Tatu nitampa salamu zenu wana jf, na mimi Pascal Mayalla kumtamkia mama kuwa sitaki uteuzi wowote!.
Namna ya kukutana na kuzungumza na rais Samia hapo kesho ni kwa kutumia kitu kinachoiitwa na power of mind suggestibility, kama niliotumia hapa
Kesho ni zamu ya Rais Samia
Wasalaam.
Paskali.