Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
View attachment 2316635View attachment 2316636
Wana JF Wenzangu, hebu tuacheni ushamba!, Media kumpongeza Rais kwa kazi nzuri na kufanya vema, sio kujipendekeza au kujikombakomba kunyemelea uteuzi!, rais wetu pia ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, akifanya vema, anastahili pongezi as encouragement, aendelee kufanya mazuri zaidi na zaidi, lakini baadhi ya watu humu kiukweli mnakera, sisi watu wa media, kila tukimpongeza rais kwa kufanya vema au mazuri yoyote, mnatuzodoa na kutunyooshea vidole kuwa pongezi hizo ni pongezi za kinafki kujipendekeza tuu ili kusaka uteuzi!.
Tangu rais Samia ameingia madarakani amefanya mengi makubwa mazuri ya kustahili sifa na pongezi za dhati, lakini pia Rais Samia sio malaika, hivyo anaweza kukosea na tutamkosoa!. Hivyo katika mazuri, nami nimempongeza kwa mengi, lakini nakereka kila nikipongeza nabezwa kuwa nafukuzia uteuzi!, hivi watu mnaona pongezi tuu?, critics hamzioni?.
Jana Rais Samia kateua majaji wapya 22 wa mahakama Kuu, katika uteuzi huo majaji 11 ni Wanawake na 11 ni wanaume, nikapandisha bandiko la pongezi
Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?
wale wazodoaji wakaniibukia eti ni bandiko la kujipendekeza, eti kwa vile sifa za kuwa jaji ni kuwa na LL.B, na mimi ninayo, sasa naupumulia u Jaji!. Acheni hizo!.
Haya sasa Mungu bariki, mimi niko Mbeya, kwenye maonyesho ya Nane Nane nikifanya Vipindi vyangu vya Nane Nane na PPR, na rais yuko Mbeya, ndiye mgeni Rasmi kwenye kilele cha Nane Nane, hivyo kesho ndio itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Rais Samia face to face, tangu Mungu alipomteua kuwa rais wetu, hivyo ikitokea katika pita pita za mabandani. ikitokea akapita karibu yangu, nitamsalimia kwa sauti kubwa tuu na atasikia, sijui kama atajibu, shikamoo yangu...
Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa DC, DED, RAS, RC, JAJI, or anybody!.
na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote
Paskali.