Umeandika kirahisi mnoo kuliko uhalisia. Ngoja nikupe uhalisia.
1. Baadhi ya nchi (hususani Ujerumani) kanisa katoliki limepitisha azimio la kuwatambua na kuwabariki waumini na viongozi mashoga. Mpaka sasa Vatican haijachukua hatua yoyote ya kuwafukuza au kuwatenga maaskofu wa kanisa katoliki nchini Ujerumani. Kwa lugha nyepesi sana, Kanisa Katoliki la Ujerumani lina nguvu kubwa ya kuitikisa Vatican!
2. Kanisa katoliki hubadilisha misimamo na mitizamo yake mbalimbali kulingana na nyakati, mazingira na misukumo ya kijamii. Mfano halisi ni suala la uzazi wa mpango. Kwa hiyo hata hili la mambo ya Ushoga lolote linaweza kutokea kupitia kanisa katoliki hivyo usije ukashangaa.
3. Kanisa katoliki halifungwi sana na kile kilichoandikwa ndani ya Biblia, linafungwa zaidi na tamko la vatican (kile kitakachoamriwa na papa na baraza lake tu), na tamko hilo huenda likabadilika, kuboreshwa au kufutwa baada ya muda fulani. Hivyo omba sana Mungu ili papa na wale wanaomzunguka wasikutwe na huo upepo wa kishoga.
4. Msimamo wa waumini wa katoliki Ulaya na kwa sehemu fulani America ndio wenye nguvu kubwa katika kuliendesha kanisa Katoliki duniani (kama huamini hilo, tazama nani huchukua cheo cha upapa, na makadinali wengi hutokea wapi), sasa kile kinachoendelea ulaya kijamii, taratibu taratibu ndicho hicho hicho utakuja kukikuta ndani ya kanisa katoliki.
5. Kwa sehemu kubwa sana, kanisa Katoliki limepoteza nguvu ya ushawishi kijamii katika nchi nyingi za ulaya (waumini wamepungua, waumini wengi hawafuati misimamo ya kanisa, idadi ya makasisi imepungua, kashfa za ubakaji zimelikumbuka kanisa, makanisa mengi yamefungwa), hivyo njia yoyote (hata ya kuhalalisha visivyofaa kama ushoga) huenda ikatumika na kanisa Katoliki ili kufufua ushawishi na kukubalika.