Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!


Tuwekee hapaaaaaaaaaa! hiyo barua
 
Mambo mengine tuwage tunafikiria. Wao wenyewe PCCB wanatoa-ga posho marambilimbili. Leo eti wanapokuja na madai ya kitu ambacho hata wao wanakifanya, tuwaeleweje?

Tumeambiwa wakiwaita-ga waheshimiwa hao ambao leo wanajidai kuwahoji, wanwalipa mpaka malazi hata kama wengine wako Dar!

Upuuzi gani huu leo wanakuja nao?

Hawa jamaa si lolote wametumwa waje watulize upepo. Serikali imekamatwa pabaya. Na kwa taarifa yao hakuna kurudi nyuma, mpaka Hosea aondoke.

Ningekuwa Mbunge ningemtaka Rais amwondoe hosea halafu ndio PCCB iwahoji wabunge.
 
Nchi hii ina mambo kweli.....viserikali corrupt vinakuwa na mikoroganao mingi sana.
 
asante kiongozi kwa reminder .i said it early kuwa Sitta ni mbabaishaji..he has nothing serious to speak kuhusu ufisadi
Hata Hawa wanaojiita wapinzani wa CCM, ni pamoja na zitto na DR slaa. si watetezi wa umma bali ni watu wa kuangalia kitu gani kitanipatia umaarufu na kukisema. watanzania walio wengi ni watu wasiopenda wenzao wapate kuzidi wao. hivyo daima ni watu wanaounga mkono watu wanaopingana na mapato ya wale wanaopata. SAsa hapa utaona hata Pinda ni mtu wa kujifanya yuko na watanzania wengi eti apendi ufahari ( mashangingi na suti), Wakati yeye mwenyewe anapanda mashangingi na kuvaa suti sana tu. sasa mi nafikiri kama kuna matatizo ni mfumo mzima. Ebu tusubili pale hawa wanaopinga humu jf kama wakienda bungeni watapunguza posho kwa wabunge (never). wanalalama kwa sababu wao wamekosa position ya kula. Sasa ya posho ni magumu sana tu. Ebu tuangalie mambo ya msingi, kwani tunapolalama na posho wajanja wanachota hela za kilimo kwanza kujiandaa na uchaguzi mwakani. baada ya matokeo tunaanza tena kulalama walichota hela za kilimo kwanza. Kwa mfumo huu tutaendelea kuwa walalamikaji milele.
 
hii ni propaganda tuu hili suala la posho mara mbili lipo hata serikalini na huko PCCB.
hamna jipya
 
CCM walipisha hiyo kwa kuibatiza jina takrima. Hiyo ni rushwa kwa sababu binadamu ameumbwa na aibu, ukishamkirimia basi mnakuwa marafiki na hata pale alipotakiwa kukufokea atakutaka radhi.

Sasa hii mazoea ya watz imekua tabia sasa, hata wabunge wanaona kila kazi ni ulaji tu na blabla.
 
hii ni propaganda tuu hili suala la posho mara mbili lipo hata serikalini na huko PCCB.
hamna jipya

Suala la posho mbili mbili kuwapo serikalini halimaanishi kuwa sahihi! Why can't you simply be reasonable?
 
Kitu ambacho wengi wanashindwa kutofautisha hapa ni kwamba hizo posho zimelalamikiwa na hao wanaozitoa. Sasa toka lini ukarimu wa kiafrika ukalalamikiwa?

Kinachoonekana hapo sio ukarimu bali hao waheshimiwa wana demand hizo posho kitu ambacho ni makosa.

Wewe unamchunguza Mkurugenzi wa Tanesco, tena mtu huyo huyo anakufungia pesa kwenye bahasha, mbona conflict of interest iko wazi mno hapo?

Imagine wewe ni mchunguzi wa matumizi mabaya ya halmashauri ya wilaya, ukifika huko unapewa posho na hiyo hiyo wilaya unayoichunguza, sisi Watanzania hatuoni tatizo hapo?

Kama wabunge na viongozi wengine wataruhusiwa kufanya wanachofanya sasa, tutakuwa tumefungulia mkondo wa rushwa ya kutisha kwenye jamii. Kwanini wanaochunguza case wasipewe posho na wahalifu?

Matokeo yake pesa tunazotenga kwa maendeleo ya nchi zitaishia kwenye takrima.

Baadhi ya maoni ya watu hapa yanasikitisha sana, kama tunahalalisha uwizi wa waziwazi kama huo, tusahau nchi yetu kwenda mbele. Suala hapa sio wabunge tu bali ni kwa kila mtu, kuanzia rais mpaka chini.

Tuache kuunguza pesa za wananchi kwa mambo ya kutajirisha watu wachache.

Nikilinganisha jinsi expenses scandal ilivyowakaanga wabunge hapa UK kwa kulaaniwa na kila mtu kuanzia muuza mitumba mpaka mamilionea. Kwa TZ kupokea posho mbili ni mbaya zaidi lakini spika bila hata kuona aibu anakuja kuhalalisha; hata hapa JF tunahalalisha, yaani sisi Waafrika tuna matatizo makubwa sana na tuna safari ndefu mno kuelekea uongozi wa haki na sheria.
 
Tetetetete. Bwana tusidanganyane hapa hakuna Mbunge hata mmoja naetetea wananchi. Linapokuja swala la pesa lazima utasikia kila mbubge anapigana kufa aipate. kwa kifupi wabunge wetu ni wajasiliami kama sisi. whenever their is an opportunity for sure they are going for it. that's why siwezi kumshangaa spika 6 and others.
 
Mtanzania: Huu ukarimu wa Kiafrika (takrima) ulitupa shida sana kwenye mambo ya uchaguzi, kwa hiyo sasa hivi nako tuutoe kwenye "double payment." I think it is a matter of time takrima itazikwa tena kwa mara ya pili!
 
Mimi nakushangaeni ndugu zetu huko TzB, eti mnaambiwa CCM kuna kikundi cha wabunge wanapambana na ufisadi...humo yumo Mwekyembe na Spika Sitta na wenzao...tangu lini? mimi hujiuliza swali hili...keni Yuu imajini zat...hawa wote wanashabikia wizi kwa kutetea malipo ya kazi moja marambili wakati kuna Mtanzania anaishi chini ya dola moja...hajuwi kula yake, kuvaa yake wala tiba yake?
Tangu lini mfuasi wa shetani akaingia Msikitini au kanisani...wakati huo huo akabaki kushabikia vitendoa vya kishetani...Watz amkeni, CCM haina mpiganaji wa ufisadi...wote ni mafisadi...kuwapo wao na kutokuwapo madarakani hakuna tofauti yoyote zaidi ni faida kwa wananchi wa kawaida.
 
Ndio sio ajabu kupata posho zaidi ya moja siku hizi. Ilikuwa dhambi wakati wa Ng'walimu JKN na Azimio lake la Arusha alilozikwa nalo. Hawa jamaa wa kizazi kipya walienda kuliua Azimio la Arusha Zanzibar ambalo lilikuwa na miiko na maadili ya wafanyakazi wa Umma, na wakaruhusu kuweka tafsiri operationally. Kuiba ni kusogeza, rushwa ni takrima, hongo ni shukrani..... ubepari ni uwekezaji, ufisadi ni uthubutu kiuchumi, kutanua ni ku-overtake. Sasa hao wanaopiga kelele za posho zaidi ya moja wako dunia ya wapi? Si ndio maana wapinzani wanalilia katiba mpya ambamo kila kitu kitasawazishwa?

Kama hilo halikubaliki asiyetaka watu watese kwa zamu na ajinyonge. Kila ng'ombe hula nyasi kwa kipenyo cha kamba aliyofungiwa. Aliyefungiwa kamba ndefu of course atakula nyasi nyingi zaidi, asionewe wivu. Tanzani Hooooovyoooooooo!

Leka
 
Bunge la walafi na waroho na wabinafsi wakubwa Afrika
PENGINE tufanyeni utafiti kuhusu ni wabunge wa nchi ipi Afrika ambao ndio wanaoongoza kwa uroho, ulafi na ubinafsi.
Na wakati huohuo tuangalie Spika Kigeugeu na mbelenyuma mkubwa kuliko wote Afrika huku tukizingatia kuwa haijawahi kutokea fisi kuwa wakili katika kesi ya simba, mbweha, chui, paka na nyauduma kuiba nyama ya jamii husika.
Mimi ninaamini kabisa kwamba kuna nchi hapa Afrika ambao wanakula posho kumi kwa hivyo mbili za wetu sio kitu cha kutisha.
Ninaamini pia kwamba wabunge wetu kwa viwango vya Afrika wanalipwa mshahara kidunchu kuliko wote na wao ni safi mno kiasi ambacho yule ambaye ni tajiri ana pikipiki tu kama sio baiskeli.
Na ndio maana mnashangaa kuona kwamba nyie mkizungumzia wao kuacha mashangingi na kukubali magari madogo kama wenzao wa Kenya wao wanakaa kimya kwa sababu HAWANA, HAWANA KABISA!
Na wabunge hawa na mawaziri hawataki kuishi Dodoma kwa sababu hakuna bahari na ndito za IFM, CBE na UDSM ambazo kwao ni hasusa.
Wabunge wetu wanaoongoza kwa kutetea maslahi ya wale waliowatuma kuwawakilisha gizani kama sio bungeni na nitaorodhesha mafanikio yao kadhaa.
1. Kila Mtanzania katika kila jimbo hivi sasa angalau ana kiwanja kilichopimwa na kanyumba angalau ka vyumba kimoja na nusu.
2. Kila mji na kijiji Tanzania sasa kina barabara ya lami.
3. Kila jimbo Tanzania lina shule 100 za msingi, 200 za sekondari na Vyuo Vikuu vya Kikakoliki 3 vya Kiislamu Kimoja, vya Kiaghakan viwili na vya makafiri 4.
4. Kila mji na kijiji Tanzania hivi sasa vina umeme wa uhakika.
5. KIla jimbo Tanzania lina mfuko wake wa maendeleo ambao wa chini kabisa una shilingi bilioni 1,000.
6. Shule zote hapo juu zina walimu wenye nyumba nzuri na samani za Modern Furniture na hakuna anayepata mshahara chini ya shilingi milioni 2.
7. ATCL, yaani, lile shirika la ndege mnalodhani limekufa ndio shirika bora kuliko yote Afrika.
8. TRL na TAZARA ni baadhi ya mashirika bora ya reli duniani.
9. Barricks inalipia umeme wa vijiji vyote mkoani Mara kwa miaka 50 ijayo.
10. Wanafunzi wa vyuo vikuu toka kila jimbo sasa sio chini ya laki moja.
11. Wagonjwa katika kila jimbo hivi sasa wanatibiwa bure asante kwa hisani ya wachimba dhahabu nchini.
12. Kila mwananchi ana simu za mkononi. Moja ambayo ataitumia kupigia kura mwaka 2010. Nyingine kupokelea fedha kiasi cha shilingi milioni moja atakazotumiwa na mifuko ya rais wastaafu kila mwezi.
13. Ndege 1,000 zimenunuliwa ili kupiga mabomu mawingu ili yanye mvua kila jimbo.
14. Hivi leo kila Ubalozi wetu nchi za nje una hosteli yake ambayo kila Mtanzania anaweza kukaa kwa gharama ndogo na kupata huduma zote ili kurahisisha shughuli yake iwe ni kusoma, kuwekeza, biashara au diplomasia.
15. Mtanzania yoyote sasa anaweza kusoma hadi levo ya digrii kwa kutumia lugha mama yake ya Kiswahili.
16. Kila jimbo Tanzania litakuwa na intaneti ya bure kwa wasio na hela na pia redio na televisheni stesheni na gazeti lao la kutoka mara mbili kwa wiki maana mawasiliano ndio ufunguo wa maendeleo.

17. Maji kutoka Ziwa Mama Nyerere (VIctoria), Lake Nyasa, Lake Rukwa na Tanganyika yatatumika sio tu kunyweeshea mashamba makubwa ya ujima bali pia kuzalisha umeme kwa matumzi ya nyumbani na kuuza nchi za nje.
18. TBC sasa ni kama BBC na inasikika kote Afrika, Uarabuni na Ulaya kitlevisheni na kiredio.
Nchi kadhaa Afrika sasa zimekubali Kiswahili kuwa lugha ya taifa au angalau lugha ya pili au ya tatu nchini mwao.
19. Ubia katika ya wahandisi binafsi na wale wa vyombo vya dola sasa unasaidia kuzalisha magari ya aina mbalimbali, matrekta, friji, televisheni, mitambo ya kurusha matangazo, vifaa vya hospitali, satelaiti, kompyuta na kadhalika.
20. KUbwa zaidi ni kwamba uko bado TANZANIA na yote hayo bado ni ndoto maana wabunge badala ya kuyazungumzia wao wanazungumzia POSHO ZAO MBILI, TATU, NNE na Mungu awalaani kwazo milele na milele na hasa mwaka 2010! Upinzani acheni use..... unganeni msidanganywe kwa serikali kuahidi kuwapa wagombea urais wenu takrima au mtakwenda na maji kama kawaida yenu....
 

Hayo uyasemayo ni kweli, japokuwa wapinzania wengi wana harufu na maziwa waliyokuwa wananyonya kule CCM kabla ya kuonja joto ya jiwe na kung'atuka! Ndio maana Wapinzania wote, isipokuwa Zitto na Dkt Slaa, hawajasema chochote kulipwa mara mbili kwa kazi moja! Isitoshe wakati Dkt Slaa alipotoa hoja Bungeni kwamba posho zao ni kubwa na zipunguzwe, Wapinzania walivaa mashati ya kijani mioyoni mwao na kugeuka bubu! Ndio maana watz bado wamewapa CCM "benefit of doubt!"
 
Hao wabunge wahojiwe pamoja na waliowapa hizo posho wahojiwe pia! na kama ikigundulika ilikuwa rushwa ili wafunike mambo TAKUKURU wapeleke kesi mahakamani kuliko kila siku kutuchosha na kelele zao. Wizi mtupu!!!!
 
Hao wabunge wahojiwe pamoja na waliowapa hizo posho wahojiwe pia! na kama ikigundulika ilikuwa rushwa ili wafunike mambo TAKUKURU wapeleke kesi mahakamani kuliko kila siku kutuchosha na kelele zao. Wizi mtupu!!!!

Usijali, takrima itazikwa kwa mara ya pili! It is a matter of time!
 
Spika Six ameniangusha kwenye hili,posho hizo ni kubwa sana na si halali kuchukua mara mbili mbili,hakuna tofauti na ufisadi. Kwasababu ubunge na uongozi kwa ujumla ni kama biashara,then ili kupata mipesa yote hiyo ni lazima uinvest pesa za kutosha,hivyo mtu anainvest kwenye kuhonga nk ili apate donge nono mara baada ya kushinda,Tanzania masikini ndio wengi zaidi,na bado hawapati wawakilishi wa kweli,system ni mbovu na status quo waelewe hilo,sasa kama wewe unayejiita mpiganaji bado unatishwa na mafisadi kwasababu ya kukumbatia system ya kifisadi,then uhalali wa upiganaji wako ni upi? No wonder mzee MKJJ anauliza...Je wapiganaji wa CCM mnachopigania ni kipi?
 

Kwa hiyo kwa Spika Sitta bungeni ni sehemu ya kufaidi?

To be fair to Sitta though, rafiki yangu Kuhani au kaka yake Dilunga wangeuliza "Mona article haina direct quote yeye matamshi ya spika kuhusu wivu?"
 
Naona Zito na Dr. Slaa mmesahau ule usemi unaosema, “ukiona ndugu wanagombana, chukua jembe kalime. Wakipatana wewe kavune”. Najua mnajua wazi kuwa wanaopokea posho mara mbili serikalini ni wengi mno ila hili la wabunge limekuja tu kwa sababu watu wengine hawatakiwi humo ndani ya CCM. Mnajua wazi kuwa hili limeibuka tu kwa sababu kundi moja la wanaCCM limeona wenzao wanifaidi serikali ya CCM hivyo wakaamua kuitana mafisadi (japo wote ni mafisadi). Kumbuka Uchunguzi uligundua kuwa Mbunge Chitalilo aligushi vyeti ila serikali ikasema haina interest ya kumpeleka mahakamani. Hamuoni kuwa huu uchunguzi wa TAKUKURUni kiini macho ili kuwanyamazisha vidomodomo ndani ya CCM. Siku Chitalilo akinyanyua tu mdomo utasikia anapelekwa mahakamani. Hivyo ninaamini kuwa sakata la Richmond likipoa, hutakaa usikie lolote kuhusu posho mara mbili na TAKUKURU hiyo hiyo itasema hakukuwa na kosa la kijinai ila ni ukiukwaji mdogo tu wa taratibu za fedha. Na hapo CCM wakipatana usijeshangaa Zito na Dr Slaa wakageuziwa kibao wakaitwa wachonganishi, wapinzani uchwara na/au wachochezi.
Mh. Dr. Slaa na Zito Kabwe, Huku mikoani CHADEMA tunaipenda sana, acheni kuingilia mambo mnayojua kuwa ni kiinimacho. Njooni huku tuandae vijana wa kusimamia kura (mawakala wa uchaguzi mapema). Msikubali kuingilia mambo ambayo unajua kuwa serikali tulo nayo haina utashi wa kisisa wa kushughulikia hili suala la posho mara mbili japo ni wazi kuwa kisheria ni kosa. Kwa wale wasiojua makosa ya Rushwa kuna kosa moja linaitwa “Obtaining advantage without lawful consideration”. Hivyo TAKUKURU wanao uwezo wa kuchunguza na kuwafungulia mashtaka hao walochukua posho mara mbili ila ikitokea issue ya Richmond ikipita bila matatizo ..................
 
Kupokea posho mara mbili mbili kunadumaza Taifa. Kwanini wasipige kelele? Ni kuogopa kuitwa wapinzani uchwara? Mbona hilo wameshaitwa saaana. Kwanza wao ni wabunge, na issue inahusu wabunge. Kama wabunge wa upinzani lazima wataulizwa na waandishi wa habari ni nini msimamo wao. Wakikaa kimya watapakaziwa wanalindana. Halafu hivi kutafuta mawakala si jukumu la mgombea? Sidhani kama ni busara kumhusisha Katibu Mkuu au Naibu wake. Watafanya mangapi? Hilo ni suala la kurugenzi ya Uchaguzi.

Mimi binafsi wabaya wangu wakigombana nitashabikia ili wauwane wasije hata kuafikiana baadaye. Kama ikishindikana nitachochea mpaka watoane macho hata wakija patana wana makovu ya kudumu. Hapo nitajihesabu nimeshinda.

.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…