Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

"Nani hajui kama wewe pesa za mafisadi zimekufikia?.Suala la kupokea posho mara 2 limeanza leo?.Basi wachunguze tangia bunge limeanza. Na je yale maazimio 23 akiwemo Osea kujihuzulu imekuaje kugongona na ilo la posho za wabunge, kwani osea amekuwa mkuu wa takukuru leo, alikuwa wapi siku zote?.Wewe ni mmojawapo wa mafisadi.

Hivi kwa kuwa wizi ulianza nyakati za akina Yuda Iskariote aliyekuwa anaiba fedha za hazina au mtoto wa Adamu na Hawa (wazazi wetu wa kwanza), Kaini alipomuua ndugu yake Habili, tuseme hayo sio makosa kwa sababu yameanza muda mrefu? Hakuna expiry date ya makosa na kumbuka kuwa hoja ya posho mbili kwa kazi moja haijaibuliwa na TAKUKURU bali na Bunge lenyewe! Labda ujiulize Bunge lilikuwa wapi muda wote mpaka liibue hoja sasa hivi?
 
Mafisadi wajanja sana tayari wamesha vuluga akiri za Wadanganyika.
 
Hosea yupo kwa faida ya mafisadi wenzake......subirini muda ukifika tutajua yote,,,,,,,,lazima watafikishwa mahakamanii....siku yao inakuja
 
Ni kwa taratibu gani ya kisheria TAkukuru wanatakiwa kutoa posho kwa wabunge?


hawa wanaotoa hizi posho kwa wabunge ni kina nani? wanazitoa wapi na katika fungu gani? Na kwanini wakidaiwa na wabunge wasigome?



Hiyo sheria imepitwa na wakati, mtu akikupa zawadi atakuwa amekupa rushwa? Basi wengi wetu humu tuna hatia ya kupokea zawadi!




Wabunge wakiwa bungeni hakuna mahakama inayoruhusiwa kuwachunguza au kufanya uchunguzi wowote bila idhini ya Spika. Siyo kuombwa na Katibu wa Bunge. Bunge likikaa hakuna chombo cha dola kinachoweza kuleta hata summons ya kumuita mbunge yoyote. Sasa TAKUKURU wamepata wapi nguvu ya kuwaita wabunge kutoka kwenye kikao cha bunge kwenda kufanya uchunguzi wao? Soma sheria ya Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge Ibara 5 na ya 11!




Hata kama hilo ni kweli, wanapoanza uchunguzi wao wanatakiwa watoe taarifa kwa Spika. Sheria inasema hilo haliwezekani "without Speaker's leave"!



Wabunge hawahitaji kumpigia kura yeye kwani hawamthibitishi uteuzi wake. WAbunge wataipigia kura serikali! Yaani, kutokuwa na imani na waziri mkuu. Sasa JK itabidi achague kumtosa Hosea au serikali yake iporomoke tena sababu ya kiburi cha watu wanaofikiri wako juu ya sheria.



Hilo ni kweli, lakini ifanye kazi yake kisheria. Na hilo ni kusitisha uchunguzi wao sasa hivi, kuomba kibali kwa Spika wanapomtaka mbunge yoyote kutoa ushirikiano wakati kikao cha bunge kinaendelea. Nje ya hapo, wao ndio wamejinyanyua juu ya sheria.




Imewadhalilisha wabunge kwa kufanya uchunguzi wakati kikao cha bunge kinaendelea bila ruhusa ya Spika.




Na hilo linamjumuisha Hosea na Pinda. Kama ingekuwa kweli wanatawala kwa sheria Pinda alitakiwa kujiuzulu siku ile alipotoa ruhusa ya watu kujichukulia sheria mkononi utadhani hiyo sheria ni mapendekezo ya aina fulani.



Misimamo mingine siyo ya kupongeza ni ya kubeza. Msimamo wa kudai ana madaraka ambayo hana siyo msimamo wa kupongezwa.



Wabunge wakikubali kushindwa mbele ya TAKUKURU na wakapigishwa magoti then the parliament has officially become irrelevant!. Hosea hawezi kutunishia misuli bunge akabakia alivyo!

Mwanakijiji,
Siamini kama unaamini unachokitetea hapa.
 
Kamati ya bunge imekiri ndani ya ripoti yake kuwa hakukuwa na rushwa katika mchakato mzima. Sasa adhabu dhidi ya hosea ni ipi wakuu?
 
Hosea kwanza bwaga manyanga kwa kuwajibika kwako na kuisafisha Ricmomd. Baada ya hapo tuachia TAKUKURU yetu ikiwa na heshima na taazima yake. Kama ungewajibika kwa hilo leo hii Mbunge asinge weza kukataa kuhojiwa na taasisi yenye heshima, na hii ni mwanzo wa kuwafanya Watanzania kuto ieshimu taasis nyeti namna hiyo kwa nchi.
Tafadhari tumia busara katika kufanya maamuzi, Elimu unayo ya kukutosha utapata kazi nyingine ya kufanya tu mwana wane.
Usiogope Mwenzio Edward Lowasa ilijiuzulu, kwanini isiwe wewe,chukua hatua kabla huja iaibika kwasababu mapendekezo 23 ya kamati ya Richmond(Kamati ya aikina Mwakembe yanahitaji hujiuzulu).
Fanya hivyo kwa heshima ya Nchi na Rais pia.
 
Mwanakijiji:

Listen to how masterful you are at defending your position when your mind is made up and you are not prepared to entertain any views to the contrary - whether those views are valid or not:

Kama posho zimetolewa kwa wabunge bila kufuwata sheria kama TK alivyoandika:
1. Posho walizotoa Takukuru kwa wabunge hazi kutolewa mara mbili. Ofisi ya Bunge haikuwalipa posho wabunge ku attend seminar hiyo. Kwa hiyo ni Takukuru tu ndio iliyowalipa.
wewe ukajaribu ku argue kuwa hapa sheria haikuvunjwa:


Ni kwa taratibu gani ya kisheria TAkukuru wanatakiwa kutoa posho kwa wabunge?

Lakini TK alipojaribu kuonyesha jinsi sheria ilivyovunjwa pale aliposema:
3. Kwa sheria za Takukuru, kupokea pesa bila kuzitolea jasho ni rushwa.
Wewe ukageuga mara moja na ku-dismiss the importance of existing laws (so you can win this argument I suppose) when you responded by suggesting:


Hiyo sheria imepitwa na wakati, mtu akikupa zawadi atakuwa amekupa rushwa? Basi wengi wetu humu tuna hatia ya kupokea zawadi!

Poor TK, he will never win this debate at this rate! He is doomed if he ignores the law and he is doomed if he follows the law! Stupid me, I was under the impression that your main line of argument throughout this entire debate was essentially that the PCCB did not follow existing laws when they requested an interview with Dr Mwakyembe. What I didn't know was the fact that your use of the law argument is arbitrary and selective!

Now based on these minor observations, would I be stretching the truth if I concluded that you a devout adherent of the philosophical doctrine that says: “My mind is made up, don't confuse me with the facts!”
 
Hosea alitisha Bunge

Na Muhibu Said
3rd November 2009

headline_bullet.jpg
Awaambia wabunge hawako juu ya sheria, watahojiwa

headline_bullet.jpg
Awataka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye

headline_bullet.jpg
Asisitiza hana mpango wowote wa kujiuzulu Takukuru

headline_bullet.jpg
Spika Sita asema Hosea anatapatapa na kupotosha umma



Hosea%20E(1).jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, amelivimbishia msuli Bunge.

Katika kauli ambazo ni nadra kutolewa hadharani na kiongozi huyo wa taasisi nyeti dhidi ya muhimili mmojawapo wa dola, pia alisema tuhuma za kuisafisha kampuni ya kitapeli ya kufua umeme ya Richmond, anazohusishwa nazo na Bunge, kamwe hazimnyimi usingizi na kwamba, kama wabunge wanamuona hafai, basi watumie utaratibu wao wa kupiga kura bungeni ya kutokuwa na imani naye ili ang’olewe kwani Takukuru siyo mwisho wa maisha yake.

Dk. Hoseah alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zilizochukuliwa na Takukuru za kuwahoji baadhi ya wabunge kwa kupokea posho mara mbili kwa kazi moja kutoka taasisi tofauti za umma.

Ufafanuzi huo aliutoa katika mkutano wake na waandishi wa habari, aliouitisha makao makuu ya Takukuru, jijini Dar es Salaam.

Alisema mchakato wa Takukuru wa kuwahoji wabunge kuhusu tuhuma hizo, unaendelea kwa vile unalindwa na sheria na kwamba, kama wamemuona hafai, basi watumie utaratibu wao wa kupiga kura bungeni ya kutokuwa na imani naye, badala ya kuendelea kulalamika kuwa wamedhalilishwa.

Dk. Hoseah, ambaye jana alizungumza kwa kujiamini, alitoa kauli hiyo alipoulizwa na mmoja wa wanahabari kwamba, wabunge wameonyesha hawana tatizo na Takukuru, bali wana tatizo na Dk. Hoseah kuhusiana na kashfa ya Richmond, kwanini basi asijiuzulu kama kweli yeye ni muadilifu?

“Zoezi linaendelea, kwa sababu sheria inatulinda, hatuhitaji kuomba kibali cha mtu yeyote. Kazi yetu ni kutafuta ukweli, hakuna kudhalilishana hapa. Kama wameona hawana imani na mimi, wapige tu kura, mimi nachapa kazi yangu, sikosi usingizi, niko hapa kuwatumikia Watanzania.

Labda sura yangu mbaya, hiyo ni bahati mbaya. Lakini kuna maisha baada ya Takukuru,” alisema Dk. Hoseah bila kufafanua na kuongeza:
“(Wabunge) waache danganya toto hapa, kwani huo ni uchunguzi tu wa kawaida, mbona wananchi wengine tunawahoji, mbona hawalalamiki kwamba, wamedhalilishwa?”

Alisema kamwe hawezi kujiuzulu kuongoza taasisi hiyo na hana mpango huo na kudai kwamba, hata taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, kifungu cha 20, haijapendekeza afanye hivyo.
“Tusome taarifa ya Kamati ya Bunge Ibara ya 20. Mpango huo (wa kujiuzulu) sina, nihukumu kwa makosa niliyotenda, si hisia. Siwezi kujitia kamba nionekane mzalendo,” alisema Dk. Hoseah.

Alitoa kauli hiyo alipotakiwa na mwanahabari mwingine katika mkutano huo wa jana, aonyeshe uzalendo kwa kujiuzulu kama walivyofanya baadhi ya viongozi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika kashfa ya Richmond.

Awali, alisema amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zilizochukuliwa na Takukuru za kuwahoji baadhi ya wabunge kwa tuhuma hizo, baada ya kuwapo na kauli na mitazamo mbalimbali miongoni mwa jamii kuhusu jambo hilo, na pia, madai kuwa taasisi hiyo imekosea kuwahoji wabunge na kwamba, imeingilia haki na kinga ya wabunge.

Alisema miezi kadhaa huko nyuma, Takukuru imekuwa ikipokea taarifa zinazohusu baadhi ya wabunge kupokea posho mara mbili wanapokwenda kufanya kazi zao za Kamati za Bunge; kwa kulipwa na Ofisi ya Bunge kama ilivyo wajibu na wanapofika kwenye wizara au shirika la umma au idara inayojitegemea ya serikali, wamekuwa wakilipwa posho na yule wanayemkagua.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa Takukuru alisema kitendo cha kulipwa posho mara mbili kwa kazi hiyo hiyo na taasisi mbili tofauti za umma, ni kinyume cha sheria za matumizi ya fedha za serikali.

Dk. Hoseah alisema kufuatia hali hiyo, Februari 26, mwaka huu, Takukuru iliandikiwa rasmi na Ofisi ya Bunge kuitaka ichunguze tuhuma hizo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Alisema Takukuru ilipata taarifa hizo na ilifanya uchunguzi wa msingi kwa kutumia taratibu zake na matokeo ya uchunguzi umeonyesha kuwa tuhuma hizo zinaelekea kuwa ni za kweli.

Dk. Hoseah alisema baada ya Takukuru kuridhika kuwa kuna hoja ya msingi ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, waliona kuwa kuna haja ya kuwahoji wahusika ili kuwapa nafasi ya kujua tatizo na wao watoe maelezo yao kwa mujibu wa haki za asili ili waweze kukamilisha uchunguzi wao.

Hata hivyo, Dk. Hoseah alikataa kuwaonyesha wanahabari barua inayodaiwa kuandikwa na Ofisi ya Bunge kuiomba Takukuru iwahoji wabunge alipotakiwa na baadhi ya wanahabari kuionyesha na kusisitiza kuwa hata viongozi wa taasisi na mashirika ya umma waliowapa wabunge posho hizo, baadhi yao wameshahojiwa na Takukuru.

“Nia yetu ni kutaka kujiridhisha iwapo tuhuma zilizotolewa kwetu ni za kweli na matokeo ya uchunguzi wetu yaweze kuthibitisha kama kuna ukweli kiasi gani kuhusu tuhuma hizo,” alisema Dk. Hoseah na kuongeza kuwa uchunguzi wao hauwalengi wabunge waliomo kwenye Kamati ya Nishati na Madini na Kamati Teule ya Bunge na kusema kwamba, hata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) pia, alihojiwa licha ya kwamba, si mjumbe wa kamati hizo.

Alisema wameshutumiwa kwamba, mahali na mazingira ya kuwahoji wabunge havilingani na hadhi ya wabunge na kusema kwamba, jambo hilo linaweza kuwa na ukweli kwa namna fulani kwa mtazamo wa mtu na kulitaka Bunge liwapatie bajeti ya kutosha ili waboreshe mazingira yao ya kazi.

Dk. Hoseah alisema pia, wametuhumiwa kwamba wabunge wamekuwa wanahojiwa na maafisa wadogo sana na kusema kwamba, anayesimamia jambo hilo ni Ofisa Mchunguzi Mkuu, ambaye amekuwa katika fani hiyo tangu mwaka 1973 na kwamba, kwa umri alionao hadi sasa, anatarajia kustaafu mwakani.

“Siamini mtu anayekaribia umri wa kustaafu mwakani ni kijana mdogo. Na kama hivyo ndivyo, ndiye mwenye umri mkubwa tuliyenaye ndani ya Taasisi kwa wakati huu,” alisema.

Alisema Takukuru pia imetuhumiwa kwamba kwa kuwahoji wabunge imekiuka sheria inayohusu Kinga, Madaraka na Haki za Wabunge na kusema kwamba, wanachoamini kwamba taasisi haikukiuka sheria hiyo akisema kwamba, kinga ya wabunge haihusu vitendo kama hivyo wanavyovichunguza.

Dk. Hoseah alisema kinga ya wabunge inahusu kauli aliyoitoa bungeni au kwenye kamati yoyote ya Bunge, maandishi ya mbunge kwenye taarifa ya Bunge au Kamati ya Bunge na kwa chochote kitakachotolewa na mbunge bungeni kwa njia ya muswada uwe wa binafsi au vinginevyo.

“Mtanzania yeyote awe wa cheo chochote hana kinga dhidi yake kwa tuhuma zinazoangukia katika makosa ya rushwa yanayotawaliwa na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007 ambayo waheshimiwa wabunge wenyewe waliitetea na kuitunga kuwa sheria,” alisema Dk. Hoseah.

“Kwa heshima na unyeyekevu mkubwa kwa waheshimiwa wabunge nawaomba waiache Takukuru ifanye kazi zake kwa mujibu wa sheria. Waheshimiwa wabunge, nawaomba muongoze kwa mfano.

“Bunge letu lina sifa kubwa ya kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi ambao ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka, tungependa suala hili lisiwe chanzo cha kulipunguzia heshima yake kubwa ndani na nje ya nchi ambayo Bunge letu tukufu limejijengea. Tupeni ushirikiano wenu ili tuwatumikie wananchi wa Tanzania vizuri,” alisema Dk. Hoseah.

Hata hivyo, alipoulizwa na Nipashe jana kuhusu barua inayodaiwa na Dk. Hoseah kwamba, iliandikwa na Ofisi ya Bunge kuiomba Takukuru iwahoji wabunge kuhusu posho mbili, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alisema hakuna barua ya namna hiyo iliyoandikiwa na Ofisi ya Bunge.

“Aionyeshe hiyo barua na imesainiwa na nani. Sababu ninachojua tuhuma ambazo ziliandikiwa barua tena na makatibu wa kamati mbili za Bunge, zilihusu tuhuma dhidi ya baadhi ya wabunge kudai rushwa ya fedha taslimu.

Tuhuma hizo zilitoka Ikulu ndio makatibu wa kamati hizo wakaiandikia Takukuru kuiomba ichunguze na hayakuwa maombi ya jumla ya kuvamia Ofisi za Bunge na kuanza kuwahoji waheshimiwa wabunge bila utaratibu,” alisema Spika Sitta.

Kuhusu kauli ya Dk. Hoseah ya kuwataka wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani naye kama wanamuona hafai, Spika Sitta alisema: “Anatapatapa, na ni upotoshaji kwa umma kwani kwa mujibu wa Katiba ya nchi, anayepigiwa kura na wabunge ya kutokuwa na imani naye ni Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Rais na wala si waziri wala mkuu wa taasisi.

Dk. Hoseah anaibuka na kauli hizi huku Bunge likitarajiwa wakati wowote kuanzia sasa kupokea taarifa ya Serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Richmond, kati yake ikiwa ni kuchukuliwa hatua kwa kiongozi huyo kwa kutokuwa makini katika uchunguzi wa mkataba huo.

Takukuru kabla ya kamati teule ya Bunge kuchunguza mchakato wa Richmond na ripoti yake ikamfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu kwa sakata hilo, Takukuru walikuwa wamechunguza mkataba huo na kuona ni safi.


CHANZO: NIPASHE
 
Lakini huyu jamaa nimesikia nyepesi kwamba familia yake iko Marekani, yeye anakaa hapa kuvuna tu, ndio maana jana alisikika akisema makelele hayamnyimi usingizi. Ati anasema kujiuzuru ni makelele tu, yeye hajali wala kutishika. Mtu ambaye anakaa mkao wa kuvuna namna hiyo anajua ukimtimua anaenda zake kwa Obama, nyie imeshakula kwenu tu.

Sijui wanatumia vigezo gani kuteua watu wa namna hiyo. Sasa kiburi kimeongezeka kwa kuteuliwa kwake na UNDP. Mlie tu, maana kucheka watanzania hamjui, mbavu hamna!

Leka
 
Alisema Takukuru ilipata taarifa hizo na ilifanya uchunguzi wa msingi kwa kutumia taratibu zake na matokeo ya uchunguzi umeonyesha kuwa tuhuma hizo zinaelekea kuwa ni za kweli.

  1. Kama walishafanya uchunguzi na kuridhika kuwa tuhuma ni za kweli kwa nini sasa wasiwashitaki hao wabunge mahakamani?
  2. Kwa vile hakuna sheria inayomlazimisha mtu kukubali kuhojiwa, kwa nini Hosea anaendelea kupiga kelele za kung'ang'ania kuhoji wabunge wasiotaka kuhojiwa badala ya kuwaburuza mahakamani wakati ushahidi anadai kuwa tayari anao?
 
Lakini huyu jamaa nimesikia nyepesi kwamba familia yake iko Marekani, yeye anakaa hapa kuvuna tu, ndio maana jana alisikika akisema makelele hayamnyimi usingizi. Ati anasema kujiuzuru ni makelele tu, yeye hajali wala kutishika. Mtu ambaye anakaa mkao wa kuvuna namna hiyo anajua ukimtimua anaenda zake kwa Obama, nyie imeshakula kwenu tu.

Sijui wanatumia vigezo gani kuteua watu wa namna hiyo. Sasa kiburi kimeongezeka kwa kuteuliwa kwake na UNDP. Mlie tu, maana kucheka watanzania hamjui, mbavu hamna!

Leka

Ikulu inaelekea wameyasikia hayo majivuno na kuridhika nayo. Si unakumbuka waliyavumilia hata yale ya 'Vijisenti'?
 
Mkurugenzi wa Takukuru Dr. Hosea, baada ya kutema cheche ile jana, leo ametinga rasmi katika viwanja vya Bunge na kukutana uso kwa uso na Spika Sitta, hivyo kumaliza rasmi malumbano yao kwa kukumbatiana kwa vicheko, tashwishwi na bashasha tele.

Swali jee Hosea amekuja kufanya nini Dodoma ilhali kesho Jumatano ndio serikali inawekwa kikaangoni kwa kutomuwajibisha Hosea!?
 
Hosea anasema hakuna mtanzania mwenye kinga juu ya sheria ya TAKUKURU, kwani mkapa sio mtanzania? ametuliza waziwazi.
 
Hosea anasema hakuna mtanzania mwenye kinga juu ya sheria ya TAKUKURU, kwani mkapa sio mtanzania? ametuliza waziwazi.

Mkapa hayuko juu ya sheria. Sheria iliyopo ndo inayomlinda.
 
Kubinika we acha tu kaka, haya ndo mambo ya Balali kumbe ni raia wa Marekani, si mambo ya kiini macho haya, mtu anateuliwa kuwa mtu mkubwa hivo hata usalama wa TAIFA HAWAFANYI KAZI YA KUMCHUNGUZA jamaa yukoje yukoje na anaishi wapi na kama ana uraia wa nchi mbili, sijui tunaenda wapi jamani. Mwl angekuwepo angewachapa viboko sana kama walivochapwa akina Warioba enzi hizo
 
Wanafanya kile kitu kinaitwa, KUPINGANA BILA KUPIGANA.
 
Ujio huu wa ghafla wa Dr. Hosea hapa Viwanja vya bunge mjini Dodoma, kumepata tafsiri mbili za haraka haraka, ya kwanza ni amekuja kukata mzizi wa fitna kumaliza malumbano ya nani zaidi kati ya Takukuru na Bunge kuhoji sakata la posho mbili mbili.

Ujio huu umetafsiriwa ni mwitikio wa kilio cha wabunge kuhusu kuhojiwa na maofisa wadogo, na mahali pasipo na hadhi, kwenye jengo la Takukuru na kukutafsiri hivyo ni kudhalilishwa. Hivyo sasa Hosea mwenyewe ameingia kazini na ataanzia kwa kumhoji Sitta, akifuatiwa na Mwakiembe, tena mahojiano hayo atayafanyia ofisi za bunge zenye hadhi stahiki yao.

Ujio huu wa Hosea ni uthibitisho kuwa anajiamini, na anajua atendalo, na amini nawaambie sio Sitta wa Mwakiembe atakayethubutu kukohoa, ni kuufyata tuu na kuhojiwa.
 
I dont understand ulichotaka kuwasilisha hapa, nadhani hawajagombana sitta na Hosea, bali kinchogomba hapa ni mitizamo kati ya PCCB na Bunge. Wao kukumbatiana hakuwezi kuondoa misuguano.
 
Pasco kweli umechoka na feelings, mi sidhani hivo, hayo ufukiriayo nafikiri ni ndoto za abunuasi
 
Back
Top Bottom