KERO Responded Posta ya Dar kuna chemba zinatiririsha maji taka barabarani, Mamlaka hazijaona, mbona zipo kimya?

KERO Responded Posta ya Dar kuna chemba zinatiririsha maji taka barabarani, Mamlaka hazijaona, mbona zipo kimya?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Eneo la Posta barabara inayotokea kwenye Kanisa la KKKT kuelekea Karemjee kuna chemba zimepasuka zinatiririsha maji taka, hali ni mbaya hasa kwa watembea kwa miguu.

Tunaomba mamlaka zitafute suluhu ya hii changamoto, njia nzima imejaa maji taka hali ambayo inaleta kero na hofu ya Watu kupata magonjwa.

Changamoto hiyo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikijitokeza kwenye maeneo tofauti ya Posta Jijini Dar es Salaam bado sijaona jitihada za mamlaka kuleta suluhu.

Tunaomba mamlaka zilifanyie kazi hasa suala hilo ikizingatiwa Posta ni sehemu ambazo kuna ofisi za umma na binafsi nyingi, hivyo changamoto hiyo inaathiri Watu wengi.




WhatsApp Image 2025-04-08 at 10.42.53_bf51ba25.jpg

WhatsApp Image 2025-04-08 at 10.42.52_a4671806.jpg
Pia soma ~ Chemba zilizokuwa zikitiririsha majitaka barabarani maeneo ya Posta (Dar) zimerekebishwa
 
Eneo la Posta barabara inayotokea kwenye Kanisa la KKKT kuelekea Karemjee kuna chemba zimepasuka zinatiririsha maji taka, hali ni mbaya hasa kwa watembea kwa miguu.

Tunaomba mamlaka zitafute suluhu ya hii changamoto, njia nzima imejaa maji taka hali ambayo inaleta kero na hofu ya Watu kupata magonjwa.

Changamoto hiyo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikijitokeza kwenye maeneo tofauti ya Posta Jijini Dar es Salaam bado sijaona jitihada za mamlaka kuleta suluhu.

Tunaomba mamlaka zilifanyie kazi hasa suala hilo ikizingatiwa Posta ni sehemu ambazo kuna ofisi za umma na binafsi nyingi, hivyo changamoto hiyo inaathiri Watu wengi.

kariakoo ndo kiboko yao mitaa yote imejaa vinyesi chemba zinatema kati kati ya barabara
 
Duuh. Nayakumbuka sana hayo maeneo. Bila shaka migahawa ya hapo inapata athari mno.

Hiyo migahawa miwili inawateja wengi mno na vyakula safi. Poleni.
 
Sio maji machafu Mavi Mavi Mavi kote inanuka Mavi kila unapopita ni harufu ya Mavi tu kila kona kila sehemu jua likiwaka kidogo panatulia ikinyesha tu Mavi yanaanza kunuka
Kuna video imetrend jana inawaonesha wamama wawili wanamwaga uchafu kwenye maji yamvua huku mvua ikinyesha hapo Dar, tena uchafu toka kwenye viloba, nasikia na kuna wengine uwa wakiona mvua ndio wanaona wakati muafaka wa kutemesha vyoo. Inasikitisha sana sasa hapo kipindu pindu kikizuka itakuaje.
 
Back
Top Bottom