binafsi nimemsikia tuu..simjui hata anafananaje?
kwa uchache ni msukuma mmoja wa miraba minne aliyekuwa ana nguvu sanaa.akivaa guo lilishonwa kwa ngozi.ana unywele mmoja mreefu mpaka matakoni ambao wakati mwingine kwayo aliutumia kuvuta gari au pikipiki.natamani siku nisikie stor za pawa mabula
vile vitu vilikuwa na mahusiano na uchawi mababu walikuwa na dawa zao za ajabu sana kwa wasambaa kuna kitu inaitwa[ muku]ukichanjiwa ukapigana ni hatari sana,au kubeba mzigo mzitomuraa
alikua anapangua risasi kwa mkono ina maana alikua mchawi?
wimbo ulikuwa unaimbwa hivi,Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.
Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.
wimbo ulikuwa unaimbwa hivi,
Power.....ngeta.......super......kibonge( rudia×4)
mkuu power ten by ten hujamuweka hapo ila kati ya wote maarufu ni MABULA hivi bado yupo hai?tulikuwa tuna wa ranks hivi.
1.power MABULA
2.power gronda
3.power ngeta.
4.power silasi
hiyo ndiyo top 4 ,walikuwa ni hatari tupu watu hawa.
Najua wengi hamkushuhudia pambano Kali kabisa LA kihistoria kati ya power MABULA vs power groda,,,ilikuwa hatari tupu.
mkuu power ten by ten hujamuweka hapo ila kati ya wote maarufu ni MABULA hivi bado yupo hai?
unajua awa mapower walikuwa wengi miaka hiyo,uyu ten ten simkumbuki.mkuu power ten by ten hujamuweka hapo ila kati ya wote maarufu ni MABULA hivi bado yupo hai?
Amen Mkuu, Mungu ni Mkuu Sana.Huu Uzi umenikumbusha mbali sana. Power mabula kipindi Fulani alikuja shuleni kwetu. Kiingilio kwenda kumuona ilikuwa shillingi tano. Unfortunately sikuwa na hela. Kwa hiyo kengere ilivyopigwa saa Tisa tuko parade wale wenye hela wakaenda ukumbini kumuona Power Mabula. Wale tusiokuwa Na kitu tukaambiwa tuelekee nyumbani. That's how I missed to see this guy alive vuma kuliko maelezo.
In all tumetoka mbali. When I look back kwamba I could not afford five shillings to see something I really wanted, nasema Mungu ni mwema. May this generation be inspired by our hardships we went through to make this world a better place and improve the wellbeing of humanity in general.
MABULA hakuwa wa Mara alikuwa wa shinyanga,ila amefanya maonyesho mengi sana Mkoa wa Mara.Ni kweli huyo jamaa, alikuwa na nguvu kweli kweli, nasikia alikuwa ni mtu wa Musoma, Mara uko...! Hayo ni mambo ambayo kweli alikuwa anafanya, na alikuwa ana uwezo wa kunywa chupa za orange squash mpaka mbili bila ya kuzimua.
Si hivyo tu, alikuwa anauwezo wa kuzuia piki piki kwa kutumia nywele na wakati mwingine meno. Na hata kuzuiya gari kwa kutumia nywele zake. Na alikuwa akivunjiwa jiwe kubwa kifuani kwake.
Pia kulikuwa na mwingine anaitwa power Bernard, na wakaja mwishoni mwishoni kina power Bukuku, ila wengine nimewasahau.
Gonga hapa mkuu, kuna uzi kama huyo.
Power-mabula-moris-nyunyusa-na-mwinamila-tz-imewaenzi-vipi.html
Huyu power alikuwa anapenda kuja shuleni kwetu UKOMBOZI shule ya msingi miaka ya 86,87unajua awa mapower walikuwa wengi miaka hiyo,uyu ten ten simkumbuki.
Alikuwa hatari ila kiboko alikuwa power MABULA.Power Ngeeeeta Supeeeer kibongeee......nimekumbuka mbali sana aiseeee