PPPTZ: Kampuni ya Kifaransa ya ALSTOM kujenga reli za juu kutoka Posta mpaka magomeni kwenda mlimani City kisha Tegeta

Shenz type, Kwa nini hizo pesa zisijenge Barabara mpya mbovu za dsm
 
Nimeelewa kumbe wamefanya mazungumzo, ni vizuri kuwa na mazungumzo.
Hizo reli zajuu ndio zinakuwaje maana pale posta hata mradi wa mabasi yaendayo kasi haujakamilika,
Mambo ni dabo dabo
Yaani hazigusi ardhi, zinafanana na ndegeulaya.
 
Wazungu waache ujinga. Reri zinajengwa chini ya ardhi (kama huko kwao) na sio juu ya ardhi! Juu ya ardhi kazi yake ni kujenga maghorofa tu! Kujenga reli juu ya ardhi ni uchafuzi wa mazingira na ni kuziba nafasi ya kufanya miradi mingine mikubwa mingi ya maendeleo yakiwemo hayo maghorofa makubwa. Kwao wazungu hata nguzo za umeme hazipo bali nyaya za umeme zinapitishwa chini ya ardhi. Wakome kutumia umbumbumbu wa viongozi wetu kutuharibia Jiji.

Aisee... Wasamehe mkuu muda umewaacha sana.
 
Waache Pwagu na pwaguzi
Wa upgrade tu squatters areas
Makazi ya watu

Huu mradi ujenzi wa mwendokasi
Unavyofanyika ni uhuniuhuni tu

Ova
 
Juzi hapa kati nilipita JNIA terminal 2 kwa safari ya kaskazini. Katika kusuburi flight nikakaribishwa na kuteta na kijana mmoja mchangamfu kwenye mgahawa mmoja kule ndani upande wa Airside.

Mazungumzo yetu yakijikita kwenye maboresho ya kufa mtu ya terminal 2 yaliyo ahidiwa miaka miwili iliyopita yaliyopaswa kufanywa na wawekezaji au makampuni ya ufaransa.

Pamoja na mbwembwe zote za kutia saini na kufyatua mapicha yenye watu waliovaa tabasamu hadi kwenye magego... Terminal 2 iko kama ilivyofunguliwa miaka ya 80 na mbaya zaidi mvua zikichanganya linavuja. Jamaa yangu tuliyezungumza naye aliishia kunipa matumaini kuwa baada ya uchaguzi huu wa CCM kazi ya ukarabati itaanza.

Nikikumbuka enzi za treni ya juu ya Mwakyembe, na Air Tanzania kushirikiana na Oman Air kufanya mambo ya kisasa, napata wasiwasi na dhamira kuu ya yote haya yanayotendeka ndani ya shamba la bibi.
 
Hivi terminal 3 ilifunguliwa miaka ya 80?
Kama sikusoi ilianzwa wakati wa Kikwete na kukamilika zama za Magufuli.
 
Juzi hapa kati nilipita JNIA terminal 2 kwa safari ya kaskazini. Katika kusuburi flight nikakaribishwa na kuteta na kijana mmoja mchangamfu kwenye mgahawa mmoja kule ndani upande wa Airside.

Mazungumzo yetu yakijikita kwenye maboresho ya kufa mtu ya terminal 2 yaliyo ahidiwa miaka miwili iliyopita yaliyopaswa kufanywa na wawekezaji au makampuni ya ufaransa.

Pamoja na mbwembwe zote za kutia saini na kufyatua mapicha yenye watu waliovaa tabasamu hadi kwenye magego... Terminal 2 iko kama ilivyofunguliwa miaka ya 80 na mbaya zaidi mvua zikichanganya linavuja. Jamaa yangu tuliyezungumza naye aliishia kunipa matumaini kuwa baada ya uchaguzi huu wa CCM kazi ya ukarabati itaanza.

Nikikumbuka enzi za treni ya juu ya Mwakyembe, na Air Tanzania kushirikiana na Oman Air kufanya mambo ya kisasa, napata wasiwasi na dhamira kuu ya yote haya yanayotendeka ndani ya shamba la bibi.
😂😂
 
View attachment 3358496
==
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM, yenye Makao yake Makuu nchini Ufaransa, iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli ili kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Kampuni ya ALSTOM.

Kama anavyosisitiza siku zote Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila na ndio faida ya PPP kwamba ALSTOM watajenga hiyo reli Kwa pesa zao ikiisha tunamwacha anaiendesha Kwa muda wa Mkataba na baada ya Mkataba reli na kila Kitu vinakuwa Mali ya Watanzania.

Hongera Mkurugenzi David Kafulila

==
David Kafulila tangu ameingia PPP iliyoanza tangu wakati wa JK mwaka 2009, lakn mabadiliko na mjadala wa PPP nikama vile imeanza na Kafulila. Mwamko wa Umma, Serikali na Sekta Binafsi sasa ni PPP ndio habari nzima.
 
View attachment 3358496
==
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM, yenye Makao yake Makuu nchini Ufaransa, iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli ili kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Kampuni ya ALSTOM.

Kama anavyosisitiza siku zote Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila na ndio faida ya PPP kwamba ALSTOM watajenga hiyo reli Kwa pesa zao ikiisha tunamwacha anaiendesha Kwa muda wa Mkataba na baada ya Mkataba reli na kila Kitu vinakuwa Mali ya Watanzania.

Hongera Mkurugenzi David Kafulila

==
Siamini mpaka nione wanajenga, CCM ni waongo sana na upenda kucheza na akili za Watanzania kwa sababu wanajuwa hawataulizwa maswali.
 
Ngoja tuone, isije ikawa ni makubaliano kati ya matapeli, nakumbuka huu mradi uliyeyuka kwa kasi ya ajabu👇

Ngoja tuone 😂
 
Back
Top Bottom