View attachment 3358496
==
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM, yenye Makao yake Makuu nchini Ufaransa, iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli ili kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Kampuni ya ALSTOM.
Kama anavyosisitiza siku zote Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila na ndio faida ya PPP kwamba ALSTOM watajenga hiyo reli Kwa pesa zao ikiisha tunamwacha anaiendesha Kwa muda wa Mkataba na baada ya Mkataba reli na kila Kitu vinakuwa Mali ya Watanzania.
Hongera Mkurugenzi David Kafulila
==