PPPTZ: Kampuni ya Kifaransa ya ALSTOM kujenga reli za juu kutoka Posta mpaka magomeni kwenda mlimani City kisha Tegeta

Maamuzi ya namna hiyo alikuwa anaweza Magufuli peke yake
 
Ili kujenga inabidi wabomoe road tena alafu wanarekebisha after 8months kama posta sijui inaenda mwezi wa kumi na ngapi kisehemu kifupi hakiishi
 
Porojo tu, mjenzi alikuwa mmoja tu kwenye hii Nchi.
 
Wafanye fast na iwe kweli
 
Naona Tz inauzwa kila kona ila niwakumbusheni watanganyika hiki wanacho kifanya hawa walio zeeka kwa sasa wao wanatizama masilahi Yao ya sasa hivi ili wapate mapesa wale wao na vizazi vyao je Nini hasara yake kwa mtz wa baadae Haka kaanchi katabinafsishwa na mabebelu alafu hakutakuwepo wa kumtupia lawama make watakua wamesha kufa wote hao mtaa waachia matatizo watz wa naokuja viongozi msifanye mambo ya hovyo kwenye nchi ya tanganyika kwakua mnakufa kesho ebu jengeni taifa ambalo hata kama mmekufa muendelee kuishi kwenye mioyo ya vizazi na vizazi vya tanganyika kama ilivyo kwa baba wa taifa Nyerere
 
Mmeshindwa kuendesha mwendokasi, Barbara zipo, abiria wapo ila kuendesha TU mmeshindwa mnataka ma treni ya juu?????
Barbara ya Kibaha chalinze Ina foleni muda wote, mnataka kujenga reli Manzese?
Kwenye vikao vyenu hua mna discuss kitu Gani? Taarab ?
 
Kuna mmoja aliletwa na mwakyembe tukapigwa mashairi kama haya na akaishia hewani kama kawaida, hope walishindwana amount ya rushwa miaka mingi ilopita, baadaye ikafanikiwa treni ya mwakyembe
yule alikuwa tapeli wa kimataifa, huku usa alikuwa anamiliki ka-stationary kamtaani.
 
Nzuri sana
 
Kafulila hajawai kuleta mradi wowote wa PPP. Kabakia kuwa chawa tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…