PPRA: Inapotokea kuna changamoto ya Mtandao katika Mfumo wa NeST huwa tunasogeza mbele muda wa Tenda

PPRA: Inapotokea kuna changamoto ya Mtandao katika Mfumo wa NeST huwa tunasogeza mbele muda wa Tenda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwachama wa JamiiForums.coma kulalamikia changamoto ya Huduma ya Mtandao katika Mfumo wa NeST, ufafanuzi umetolewa na mamlaka inayohusika

Kusoma hoja ya Mdau kwa zaidi bofya hapa ~ PPRA Mtandao wa Manunuzi (NEST) una changamoto sana

Afisa Uhusiano wa Umma wa PPRA, Joseph Muhozi anasema anafafanua:
Mifumo ya Mtandao inaweza kutokea kuyumba, inapotokea hali hiyo kama kuna changamoto ya Mtandao nak ama kuna Tenda huwa zinasogezwa mbele ili kuwe na ‘fair’.

Inapotokea hali hiyo tumekuwa tukitoa taafia kwa Wateja wetu kwa kuwatumia barua pepe, hivyo ni suala la Mtandao ambalo linaweza kutokea na likawa nje ya uwezo wetu.

Tunafanya jitihada za kutosha ili kuwa na mtandao imara, lakini pia kuna muda unaweza kuwa ni mtandao wa mtu mmoja anayehusika kawa mtandao wake.

Inapotokea hivyo tunaweza kuwapa nafasi ya kuongeza muda kama nilivyosema.
 
Back
Top Bottom