TANZIA President Bingu wa Mutharika of Malawi is dead!

TANZIA President Bingu wa Mutharika of Malawi is dead!

Vyanzo vyangu vya habari malawi vimethibitisha Dr Bingu wa Mutharika amefariki wanapeleka mwili wake south africa ili kuandaa mazingira ya utawala nchi hiyo.....utabiri wa TB Joshua umetimia
imeandikwa: kila nafsi itaonja mauti ! Sasa utabiri ni nini hapo ?
 
Huyu Mzee naona ameisha vuta tayari ila kama kawaida ya politics za Afrika huwa hawataki kusema ukweli mapema. Maana wanaogopa swala zima la usalama na transition kama itaenda peacefully. Hisia zangu awali zilikuwa kwamba kama alikuwa na cardiac arrest tangu saa tatu asubuhi na wanakuja kumrusha kwenda Sauzi saa moja jioni sina hakika kama alikuwa bado mzima. Nadhani walimpeleka ili kutoa nafasi ya kufanya maandalizi ya kutangaza msiba, na pia kama angekuwa bado yuko Lilongwe then ingekuwa rahisi kuvujisha taarifa za siri na wangelazimika kuweka mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambako mlolongo ungekuwa mrefu sana na siri ingevuja haraka sana.

Pamoja na hayo, media houses za Malawi zinafuatilia kwa karibu sana issue nzima. Ukishakuwa na Rais ambaye umejenga mtandao wa maadui kila kona, unaweza kushangaa watu wakisikia taarifa za kifo chako wanashangilia badala ya kuzimia kwa kukulilia.

Habari kamili iko kwenye hii link, kwamba Mzee Bingu wa Mutharika ameishavuta na wamemsogeza Sauzi ili waweze kuweka mambo sawa. So, official information itatoka kesho na by then watakuwa wameishajua nini cha kufanya. Muda huu vikao vinaendelea japo naona dalili zote za fujo zinainyemelea Malawi, na tunaweza kushuhudia Katiba ikiwekwa kando ili mbwa mwitu wenye uroho wa madaraka waweze kuingia IKULU na kumuweka kando Mama Joyce Banda ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais.

Malawi President Bingu wa Mutharika dies – exclusive | Malawi news, Malawi - NyasaTimes breaking online news source from Malawi

http://greatlakesvoice.com/malawi-president-bingu-wa-mutharika-is-dead/

Hizo ni taarifa za usiku ambazo ziliandikwa baada ya mwili wa Bingu wa Mutharika kupelekwa Sauzi.
 
  • Thanks
Reactions: 911
mnamchuria kifo hajafa bado
cardiac arrest watu wanadhani kafa
labd tupate taarifa kamili kutoka ikulu ya malawi
angekufa kweli BBC CNN na local medias wangeshatangaza hadi mdaa huu naandika hakuna taarifa kamili

Taarifa kamili kwako ni lazima itoke Ikulu?
Unajua siri zilizo Ikulu ya Malawi? Kama hawajaweka mambo yao ya ulinzi kwa namna wanayoona inafaa hawawezitangaza ila ukweli ndiyo huo. hata wengine bado wanabisha kama wewe: Wachache waangalie hapa
Is Malawi President Dead Or Alive? Alive. But really Dead. | Face of Malawi
 
Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, "Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana."


Nakuheshimu mno king of MMU ...ila judgement zako zisizo na hoja ndizo zitafanya nisikuheshimu.U r more than that the Boss.
Nimekopy hiyo statement hapo juu kutoka hiyo link umetoa.
Kwanza hebu jiulize...kwa nini kichwa cha habari kimeanza na kiulizo(hii inaonyesha sio habari ya uhakika).
Pili unauhakika gani kama huyo mama hajapika hayo maneno?Umewahi kumsikia Tb Joshua akitamka?
Na tatu kwa nini unapenda kuhukumu?wewe ni Mungu? au malaika? Wewe ndio msafi sana au mtakatifu wa kuanza kusema Lowasa ana dhambi isiyopasa kusameheka?
U never know in this life.Kama wewe huna imani na utabiri/prophesy basi usipike mambo yasiyo na uhakika kujaribu kuweka ubaya wa kitu bila sababu.Wala huna sababu ya kumchukia mwenzio anayeabudu ngo'ombe kama wewe unaabudu jiwe.
Muhimu.....mie sio muumini wa huyo TB joshua wala huyo Lowasa lakn najaribu kuangalia ukweli.

Hujamwelewa boss!! kama jamaa anaamini utabiri wa TB Joshua kwa Bingu wa Mutharika, basi aamini na utabiri wa TB joshua kwa Lowassa!!

They guys was just teasing his mind

umekuja na mijimaneno hayo!
 
first sio lazima kuniheshim
haina umuhimu saana kwangu
but tumia 'logic' na uelewe maandishi na sio kumvamia mtu na kumponda....tena huku
ume panic na kuongea vingine visivyokuwepo.....
jifunze kuelewa kinachoandikwa kwanza....

ni wapi mimi kama mimi nimesema Joshua kasema Lowassa atakuwa Rais?

hivi unaelewa maana ya neno 'wanadai'???????

na hiyo link si umeiona 'ina madai'?
weather 'madai' na ya kubuni ya Shelukindo au ni ya mhariri....mimi inanihusu vipi?
mimi i simply 'refer' to hayo madai...na link nikaiweka.....na hayo madai yameongelewa mno humu

sasa wewe unatoa wapi ujasiri wa kuniambia 'no research no right to speak'??????

mimi nimesema wapi hiyo ni 'confirmed news'??????

nilichosema ni ku refer 'madai'....ya watu akiwemo Shelukindo........na magazetini imeandikwa

sasa ni vipi mimi nakuwa 'hater??????

tuheshimiane aiseee

Kijana/mzee ,heshima huwa hainunuliwi.Ukijiheshimu na utaheshimiwa.
Mie sijakuponda ila nimekuelimisha.inaelekea wewe ni mgumu wa kuelewa logic.
Hata hivo message sent and delivered.
Jifunze kuheshimu imani za watu wengine na sio kupotosha watu kwa kuficha ukweli.
I wish you happy Easter.
 
Hujamwelewa boss!! kama jamaa anaamini utabiri wa TB Joshua kwa Bingu wa Mutharika, basi aamini na utabiri wa TB joshua kwa Lowassa!!

They guys was just teasing his mind

umekuja na mijimaneno hayo!

Halafu na wewe ndio unadandia treni kwa mbele.Kama hujaelewa tulia.Huo utabiri wa TB Joshua kwa Lowasa haupo in first place.Tulia dogo acha mapepe.
 
Vyanzo vyangu vya habari malawi vimethibitisha Dr Bingu wa Mutharika amefariki wanapeleka mwili wake south africa ili kuandaa mazingira ya utawala nchi hiyo.....utabiri wa TB Joshua umetimia

BBC Swahili Dk 58 zilizopita
Kutokana na hali hiyo,Mutharika amesafirishwa hadi Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na
aliondoka katika uwanja wa ndege wa Lilongwe milango ya saa sita na nusu usiku kuelekea Johannesbuerg.
Alisafirishwa Afrika kusini katika hali ya usiri mkubwa na akiwa hana fahamu.
Walioandamana nae ni mkewe na jamaa wa karibu zaidi wa rais huyo
Hii imezuia hali ya hofu na utata mkubwa nchini Malawi kwani kwa muda mrefu kumekuwa na shinikizo za kumtaka Mutharika ang'atuke .
Radio ya kitaifa ilikuwa imetangaza kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 na ambaye alikuwa hali mahututi atapelekwa hadi afrika kusini kwa matibabu maalum.
Wakati huo huo viongozi wa Malawi walitaka nchi iwe na utulivu huku watu wakimuombea apate afueni.
Afisa mmoja mkuu wa serikali ya Malawi alinukuliwa akisema kuwa Rais Mutharika aliangua akiwa katika makaazi yake rasmi na kupelekwa hospitalini ambako aliwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Akiwa hospitalini chini Malawi, Mutharika alitembelewa na maafisa wakuu katika serikali yake wakiwemo mawaziri, mkewe na wanawe.
Makamu wa Rais Bi Jocye Banda alikuwa wakwanza kuthibitisha habari za kuugua kwa Mutharika.
Kabla ya tamko hilo Bi Banda vyombo vyote vya habari vilikuwa vimebana kutoa habari zozote kuhus hali ya raia Bingu wa Mutharika.
Lakini baada ya Makamu wa rais kufichua kuwa Kiongozi wao ni mgonjwa, ndipo Radio ya kitaifa ikatangaza kuwa Mutharika atapelekwa Afrika kusini kwa matibabu maalum.
Kulingana na katiba ya Malawi ikiwa Mutharika atashindwa kuendelea na kazi yake ya Urais basi Makamu wake Bi Joyce Banda atalazimika kushikilia hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia .
Hata hivyo Bi banda na rais Mutharika walikuwa hawasikilizani kwani walikosana mwaka wa 2009 na Makamu huyo wa Rais akalazimika kuhamia upinzani
 
Halafu na wewe ndio unadandia treni kwa mbele.Kama hujaelewa tulia.Huo utabiri wa TB Joshua kwa Lowasa haupo in first place.Tulia dogo acha mapepe.

kumbe tulidanganywa?? aisee..

basi nimetulia mtoto wa kike wa sayuni! shemeji yangu hajaenda kushtaki kwenye kile chama cha akina baba?
 
kumbe tulidanganywa?? aisee..

basi nimetulia mtoto wa kike wa sayuni! shemeji yangu hajaenda kushtaki kwenye kile chama cha akina baba?

Red.....Wadanganyika huwa tunaamini kila kitu bila kutafuta ukweli.tubadilike
Kwenye bluu sijaelewa na siwezi jibu swali halijaeleweka.Kama kuna swali la nyongeza uliza
 
kuna thread ili lletwa kipindi cha nyuma kwamba kuna Mchungaji wa Nigeria Tb Joshua ametabiri mwaka huu kuna Raisi wa Africa atafariki.

Nimeskia kwenye Redio Kwamba Raisi wa Malawi yuko Maututi hospitalini.
 
Binafsi sina uhakika.Lakn pia nadhani unabii ulisema raisi atakufa.Kuwa mahututi sio hoja.Mzima anaweza kufa na mahututi akapona..
 
Binafsi sina uhakika.Lakn pia nadhani unabii ulisema raisi atakufa.Kuwa mahututi sio hoja.Mzima anaweza kufa na mahututi akapona..
hahaha i made this thread as an alert kuwakumbusha watu..about the prophesy nimejaribu ku fatilia juma pili iliyo pita aliwambia waumini wake Wamuombe Raisi mzee atakufa Mungu asha muonesha kila kitu ila waombe labda Mungu anaweza badilisha asife.ila alicho sema it is very near to happen na akasema that president is not from west africa .haya yalikuwa ya jumapili ya juzi. lets wait n see wat will happen maana siku 60 alizo sema yule mchungaji zisha fika alitoa utabiri huu mwezi wa february
 
Raisi wa malawi amefariki kama Ilivyo tabiriwa na Nabii TB joshua kuwa nadani ya siku 60 kiongozi mzee Afrika atafariki dunia Raisi huyo asubui alikuwa maututi lakaini habari za saivi zinasema ameshafariki source reuters

r


(Reuters) - Malawi President Bingu wa Mutharika has died after a heart attack, medical and government sources said .


The 78-year-old was rushed to a Lilongwe hospital on Friday after collapsing but was dead on arrival, the sources said.
 
Huyu nae alikuwa mzigo mzito kwa Malawi.Mungu ampumzishe panapohusika.Wapate faraja ya kujenga nchi yao.Aise Malawi hawajaonja mema ya nchi hata siku moja tangu waambiwe wako huru!!!
 
Back
Top Bottom