Nimesoma uzi wa Bibie
Sky Eclat kule Jukwaa la Historia na nimeshangaa kuona mfanano mkubwa kati ya Rais wa zamani wa Zaire na mmoja wa Marais wa sasa wa taifa moja la Afrika Mashariki:
Mfano:
Mobutu alipendelea kupeleka miradi mikubwa ya maendeleo kijijini kwao Gbadolite.
Alipenda kununua midege mikubwa mikubwa aina ya Concord kutoka Ufaransa kwa malipo cash. Mara nyingi midege hii ilipark tu Uwanja wa Ndege wa Kijijini Kwao Gbadolite.
Alijenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kijijini kwao Gbadolite.
Alijenga hospitali kubwa ya Rufaa kijijini kwao
Alihakikisha mahoteli Makubwa, mabenki na taasisi nyingine za kitaifa zinakuwa na matawi Kijijini kwako
Alipenda wanawake wazuri
Alipenda kuua, kutesa, kupoteza Wapinzani wake
Aliwanunua Wapinzani wake pale alipokuwa hawezi kuua ama kupoteza
Mawaziri wote walioonekana "wabishi" walifukuzwa kazi na/ama kuuawa
Mara nyingi aliwafukuza kazi ghafla viongozi wake na baadaye kuwateua kwa kuwapandisha cheo
Alifungia vyama vya siasa, NGOs na Vyombo vya habari
I See too many similarities, hebu someni na nyinyi halafu mseme:
Kwa hisani ya
Sky Eclat wa JF
Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alikuwa kiongozi wa kijeshi dikteta huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo mwaka 22 October 1977 Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36. 1 May 1980 alimuoa Bobi Ladawa pamoja na pacha mwenzake...