Yaani mishahara waliyokuwa wanalipwa, only God knows walikuwa wana-survive vipi!
Kama tutakuwa tunajadili kwa kunyoosheana vidole, tunaweza tusifikie muafaka. Ila tukijikita kwenye utaifa na uhalisia, basi tunafika sehemu tukauona ukweli.
Ukisema mwenye mtazamo huu ni mfuasi/shabiki wa JPM, na yeye akasema kwakuwa waliminywa kipindi cha JPM ni genge la wa Msoga, basi hakutakuwa na hoja zenye afya hapa.
Kwakuwa uko kwenye taasisi za kifedha, ni ninj kinakupa uhitaji wa kuajiri? Wasomi waliojaa mitaani, uwiano wa kazi kwa watu waliopo kazini? Matakwa ya kisiasa? Uchumi wa nchi?
Ikifanya tathmini, kuanzia wizarani, kila mtu anatimiza majukumu yake vizuri na kwa kiwango cha majukumu aliyosaini, kuna gap litakalohitaji kuajiri? Kwa kiasi gani? Kwanini hawaajiri?
Taasisi binafsi, mtu mmoja anapiga kazi za watu hata wanne walioko serikalini, kazi zinaenda, efficiency inaonekana, mambo ni tofauti sana na huko serikalini, wizi upo kwa efficacy timilifu kabisa.
Mashirika ya umma, kuyabinafsisha haikuwa kosa, labda utaratibu uliotumika ndo ulikuwa kosa (Tanesco kuweka chini ya NetGroup haikuwa imeuzwa unless kama utasema iliuzwa kwa kiasi gani na kwa nani). Kwa mfumo wa kiserikali, hakuna shirika lolote litakalojiendesha kwa tija na hasa kama linahusika na uzalishaji au utoaji huduma kwa jamii, sababu zilizomfanya Samia aseme pesa alizokopa kwaajili ya corona, zisipitie utaratibu wa kawaida na uliozoeleka kwenye matumizi yake ndo sababu hizo hizo zinazokwamisha taasisi zote za serikali.
Kuondoa pesa mtaani, sidhani kama kunahusiana na umasikini, hali ya nchi iko hivyo, anzia kwenye bajeti ya nchi, useme inawezekana vipi pesa zijae mtaani? Kwa utaalamu wako kwenye fedha, inapaswa kuwa vipi hapa? Tukope, tusambaze pesa mtaani, zikae kiholela tayari kwa upigaji, ndio maendeleo? Watu wanafanya kazi zaidi ya moja, mpaka masaa 18 kwa siku iki kuipata hiyo fedha, sisi tunataka iwepo tu mtaani kwa kwenda ofisini kunyanyasa wananchi na kuhudhuria semina na warsha zisizo na tija? Uhalisia ni huo, Mwinyi na Kikwete wamemwaga pesa, wametengeneza majizi na wao wakiwa sehemu ya upigaji, nchi ilipiga hatua gani?