Mshika mapembe
Kwa jinsi jamaa wanavyoporomosha mashairi nina imani utatongozeka tu. Huna mahali pa kujificha. Uzuri umekuponza.Nafuatilia kwa ukaribu sana.........
we 2pia tu au ni2mie privateIli iweje......?.....tupo mnadani........?......
Acha longolongo we sema tu unashing ngapi? (R.I.P Mangwear)
Preta nijibu pm yangu sim yako haipo hewani kwenye airtel money yako nimekutumia Million 7 kwaajili ya dinner ya kesho!! ooh sorry nimekumbuka ulinitumia email uliniambia kile ki Benz kipya kina slow pancha kipaki kuna ki Rolls Royce new model nimekiagiza Marekani moja kwa moja! Halafu weekend hii nadhani tutakuwa Dubai kwa ya matembezi!!
preta naitwa rugebalila ni mhaya kutoka kwetu kule kwa matajir kagera nina gar langu la v8 nzur sana natembelea full tank ikipungua lita tano naongez
kila nikionana na trafik njian na hajanisimamisha nageuza gar kumuhonga lak maana namuona labda alikuwa na mawazo nilipokuwa napita namiliki vitu ving sana na ninajuana na wabunge weng sana naomba unipe nafas kwenye moyo wako kwenda marekani itakuwa ni kama kichaa kwenda milembe
Preta toa tamko, mie unikubalieNafuatilia kwa ukaribu sana.........
Preta toa tamko, mie unikubalie
Zima zote chokochoko, penzi letu walilie
Ardhini kama Choroko, wapotee watitie
Mwingine usimkubalie, hawana nia ya kweli
Upendo wangu wa dhati, moyoni nimekuweka
Umekaa kwenye chati, lala nami kwenye mkeka
Wengine siguse titi, nitachukia hakika
La Azizi maliza ubishi, watoto wakalale
Kwangu wewe kama mboni, ntakupatia ulinzi
Nitakusafisha mtoni, mi nawe nguo na uzi
Kama ni maji pomoni, kipimo cha langu penzi
Achana na hawa wa msimu, mi wako wa kudumu
Nitafugia hata mbwa, kumalizia ghadhabu
Ka hujapika ubwabwa, dogi apewa adhabu
Wewe kamwe hutaguswa, wewe ka safi dhahabu
Wengine mabondia wa wapenzi wao, usiwape nafasi
Nena unikate kiu, kubali tumalizie
Vijana sasa msahau, jaribu tena badae
Mnaula wa kaukau, mchuzi nani kujazie
Sweet maliza kesi, waumbuke na zao pensi
Kama ni ushindi utakuwa ni wakoUwanjani mmekimbia, Preta mumeniachia
Mmebaki mnanyatia, moyoni mwenu mwalia
Binti anayevutia, mkonowe mmeachilia
Vimpire_Hunter na Moto, nyie moto wa mabua.
Hamuwezi kuhimili, magumu ya kupitia
Dhaifu yenu miili, hamna ya ukweli nia
Nimewazidi akili, kileleni nafikia
Mwende kimya kimya, msijeanza maneno ya mkosaji.
Uwanja huu ni mpana, mi na Preta meshibana
Bahatisheni kwa Anna, hawezi sema hapana
Ye nami tumeshikana, hatuwezi kuachana
Miss Chagga, Afrodenzi na Lara 1 nao ni wanawake, jaribuni huko.
Preta sio kama Tupa, visu butu kunolea
Mekosa mistari supa, moyoni nachekelea
Mmepata yote mifupa, nje nje amewatolea
Hiyo mistari yenu kajiribuni kwingine
Preta nipe langu Kombe, peke yangu nimesalia
Mzobemzobe nikusombe, achana na masalia
Tuchinje mkubwa ng'ombe, tusiache hata mkia
Kama Sikamona, Zawadi ya Ushindi nipatie.
Thank you!Yo most welcome sir
lazima hapa aingie line walahiPreta nikubali usione aibu,
Kuitwa vampire isiwe sababu,
Humu JF kuna mijitu ya ajabu,
Lakini wewe mpenzi ni kama dhahabu
Mimi ni yatima nionee huruma,
Pia ni bikra skuwa na demu uko nyuma,
Kila nkitongoza ilikuwa inabuma,
Lakini kwako mpenzi ntakuwa imara kama chuma..
We ni mzuri, jina lako ni preta,
Nikikupata hapa JF ntapeta
Najua huwezi kunipwerepweta,
Japo snitch wanaponda, na uzushi kuleta
Preta ooooh pretaaaaaa nikubalieeeee
Preta oooh pretaaa usinizingueeee
Dah! Shaaban Robert kafufuka nn maana mnapanga vina balaaaMapenzi ni kujituma, si uonewe huruma
Wewe hata si yatima, mali nyingi umechuma
Tochi yako naizima, gizani mpaka kiama
Huruma ni kwa walemavu na wasiojiweza, sio kwenye mahaba
Tengeru ni karibu, upweke katu hutaona
Njoo kwangu unitibu, maumivu nitapona
Tafanya taratibu, gusa kila kona
Preta achana na Vimpire_hunter, jina lake na avatar vinatisha.
Sooth maanaye mkweli, mi jina langu thabiti
Ninayo tamu asali, na kuna pipi kijiti
Achana nae wa mbali, ni kigumu kizingiti
Nitafute Tengeru Sokoni, siku ya mnada
Sina hata benzi, naamini sio kigezo
Pata na la dhati penzi, natilia sana mkazo
Hao sugu kwa uzinzi, kwao huo ndio mchezo
Preta, we will meet somewhere, someday in Arusha-I hope!
Ntamani niyaone haya mashairi jukwaani jamanWauzaji wa mitumba, hata si watu dhalili
Ashakum! we mshamba, umeonyesha dalili
Mitumba ni adimu pamba, kuzivaa ni kama zali
Kwenye mitumba hakuna saresare, kila mtu hutoka tofauti
Preta hahitaji matunzo, anahitahi nzito huba
Kwao wanao uwezo, anapata mahitaji si haba
Hongo huleta mzozo, pesa pelekea kahaba
Hapa ni raha na utamu tu, pesa ni majaliwa-leo zipo kesho hazipo
Hamuchelewi kudai, mlivyotoa kwa hiari
Wewe mfano hai, umemdai Asha tayari
Umeruka juu kama Tai, anzisha kwangu hatari
Mbona wewe hujarudisha ulivyopewa, mpaka ukawa unahonga?
Wakujua kwa mromboo, nyama choma ya mbuzi
Nyama mpaka kokolikoo, hapana fanya ajizi
Waisikia tu moshonoo, hujafanya uchunguzi
Huko ndo kuna raha zetu sie wa 'Sokoni'
Preta kwako hoi hoi, moyo wangu watweta
Achana na huyo goigoi, maombi rasmi naleta
Kwa mwingine sitoi, kwako sana nitapepeta
Shughuli naiweza, kila siku hata ukitaka
Uwanjani mmekimbia, Preta mumeniachia
Mmebaki mnanyatia, moyoni mwenu mwalia
Binti anayevutia, mkonowe mmeachilia
Vimpire_Hunter na Moto, nyie moto wa mabua.
Hamuwezi kuhimili, magumu ya kupitia
Dhaifu yenu miili, hamna ya ukweli nia
Nimewazidi akili, kileleni nafikia
Mwende kimya kimya, msijeanza maneno ya mkosaji.
Uwanja huu ni mpana, mi na Preta meshibana
Bahatisheni kwa Anna, hawezi sema hapana
Ye nami tumeshikana, hatuwezi kuachana
Miss Chagga, Afrodenzi na Lara 1 nao ni wanawake, jaribuni huko.
Preta sio kama Tupa, visu butu kunolea
Mekosa mistari supa, moyoni nachekelea
Mmepata yote mifupa, nje nje amewatolea
Hiyo mistari yenu kajiribuni kwingine
Preta nipe langu Kombe, peke yangu nimesalia
Mzobemzobe nikusombe, achana na masalia
Tuchinje mkubwa ng'ombe, tusiache hata mkia
Kama Sikamona, Zawadi ya Ushindi nipatie.