Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Preta nijibu pm yangu sim yako haipo hewani kwenye airtel money yako nimekutumia Million 7 kwaajili ya dinner ya kesho!! ooh sorry nimekumbuka ulinitumia email uliniambia kile ki Benz kipya kina slow pancha kipaki kuna ki Rolls Royce new model nimekiagiza Marekani moja kwa moja! Halafu weekend hii nadhani tutakuwa Dubai kwa ya matembezi!!


Jambazi on significant make..

Amazing!
 
preta naitwa rugebalila ni mhaya kutoka kwetu kule kwa matajir kagera nina gar langu la v8 nzur sana natembelea full tank ikipungua lita tano naongez

kila nikionana na trafik njian na hajanisimamisha nageuza gar kumuhonga lak maana namuona labda alikuwa na mawazo nilipokuwa napita namiliki vitu ving sana na ninajuana na wabunge weng sana naomba unipe nafas kwenye moyo wako kwenda marekani itakuwa ni kama kichaa kwenda milembe


Kwamba woote sasa mnatangaza nia ama vipi???

Vampire hunter ni kilietivu alafu hana gilaji...
 
Nafuatilia kwa ukaribu sana.........
Preta toa tamko, mie unikubalie
Zima zote chokochoko, penzi letu walilie
Ardhini kama Choroko, wapotee watitie
Mwingine usimkubalie, hawana nia ya kweli

Upendo wangu wa dhati, moyoni nimekuweka
Umekaa kwenye chati, lala nami kwenye mkeka
Wengine siguse titi, nitachukia hakika
La Azizi maliza ubishi, watoto wakalale

Kwangu wewe kama mboni, ntakupatia ulinzi
Nitakusafisha mtoni, mi nawe nguo na uzi
Kama ni maji pomoni, kipimo cha langu penzi
Achana na hawa wa msimu, mi wako wa kudumu

Nitafugia hata mbwa, kumalizia ghadhabu
Ka hujapika ubwabwa, dogi apewa adhabu
Wewe kamwe hutaguswa, wewe ka safi dhahabu
Wengine mabondia wa wapenzi wao, usiwape nafasi

Nena unikate kiu, kubali tumalizie
Vijana sasa msahau, jaribu tena badae
Mnaula wa kaukau, mchuzi nani kujazie
Sweet maliza kesi, waumbuke na zao pensi
 
Preta toa tamko, mie unikubalie
Zima zote chokochoko, penzi letu walilie
Ardhini kama Choroko, wapotee watitie
Mwingine usimkubalie, hawana nia ya kweli

Upendo wangu wa dhati, moyoni nimekuweka
Umekaa kwenye chati, lala nami kwenye mkeka
Wengine siguse titi, nitachukia hakika
La Azizi maliza ubishi, watoto wakalale

Kwangu wewe kama mboni, ntakupatia ulinzi
Nitakusafisha mtoni, mi nawe nguo na uzi
Kama ni maji pomoni, kipimo cha langu penzi
Achana na hawa wa msimu, mi wako wa kudumu

Nitafugia hata mbwa, kumalizia ghadhabu
Ka hujapika ubwabwa, dogi apewa adhabu
Wewe kamwe hutaguswa, wewe ka safi dhahabu
Wengine mabondia wa wapenzi wao, usiwape nafasi

Nena unikate kiu, kubali tumalizie
Vijana sasa msahau, jaribu tena badae
Mnaula wa kaukau, mchuzi nani kujazie
Sweet maliza kesi, waumbuke na zao pensi

Kijana huna kipaji, then wajitangazia ushindi
Hukumbuki kule zenji, yalomkuta yule dingi
Preta ni wangu mi mnyamwezi, nimpe love mingimingi
Wauza mitumba hawawezi, wanachojua fujo nyingi

Preta nkubali mimi, upate raha ya maisha
True love iko kwa mimi, wengine wanakupotosha
Waliku wapi toka zamani, Mpaka thread nimeanzisha
Hao hawana thamani, wanataka kunikwamisha

Hebu njoo utoe msimamo, vijana waache maneno
Tuwazike ndani ya shimo, tuwakate na msumeno
Tuwalambishe ndimu, tuwaache waking'ata meno
Mapenzi yetu yadumu, kikubwa tuwe na msimamo

Sera nshamwaga nyingi, njoo utupe yetu hukumu
Naamini kuna vigingi, wapo radhi wanipe sumu
Ila usijali preta, hawawezi kutudhuru
Wakileta za kuleta, watakimbia ka kunguru
 
Uwanjani mmekimbia, Preta mumeniachia
Mmebaki mnanyatia, moyoni mwenu mwalia
Binti anayevutia, mkonowe mmeachilia
Vimpire_Hunter na Moto, nyie moto wa mabua.

Hamuwezi kuhimili, magumu ya kupitia
Dhaifu yenu miili, hamna ya ukweli nia
Nimewazidi akili, kileleni nafikia
Mwende kimya kimya, msijeanza maneno ya mkosaji.

Uwanja huu ni mpana, mi na Preta meshibana
Bahatisheni kwa Anna, hawezi sema hapana
Ye nami tumeshikana, hatuwezi kuachana
Miss Chagga, Afrodenzi na Lara 1 nao ni wanawake, jaribuni huko.

Preta sio kama Tupa, visu butu kunolea
Mekosa mistari supa, moyoni nachekelea
Mmepata yote mifupa, nje nje amewatolea
Hiyo mistari yenu kajiribuni kwingine

Preta nipe langu Kombe, peke yangu nimesalia
Mzobemzobe nikusombe, achana na masalia
Tuchinje mkubwa ng'ombe, tusiache hata mkia
Kama Sikamona, Zawadi ya Ushindi nipatie.
 
Uwanjani mmekimbia, Preta mumeniachia
Mmebaki mnanyatia, moyoni mwenu mwalia
Binti anayevutia, mkonowe mmeachilia
Vimpire_Hunter na Moto, nyie moto wa mabua.

Hamuwezi kuhimili, magumu ya kupitia
Dhaifu yenu miili, hamna ya ukweli nia
Nimewazidi akili, kileleni nafikia
Mwende kimya kimya, msijeanza maneno ya mkosaji.

Uwanja huu ni mpana, mi na Preta meshibana
Bahatisheni kwa Anna, hawezi sema hapana
Ye nami tumeshikana, hatuwezi kuachana
Miss Chagga, Afrodenzi na Lara 1 nao ni wanawake, jaribuni huko.

Preta sio kama Tupa, visu butu kunolea
Mekosa mistari supa, moyoni nachekelea
Mmepata yote mifupa, nje nje amewatolea
Hiyo mistari yenu kajiribuni kwingine

Preta nipe langu Kombe, peke yangu nimesalia
Mzobemzobe nikusombe, achana na masalia
Tuchinje mkubwa ng'ombe, tusiache hata mkia
Kama Sikamona, Zawadi ya Ushindi nipatie.
Kama ni ushindi utakuwa ni wako
 
Preta nikubali usione aibu,
Kuitwa vampire isiwe sababu,
Humu JF kuna mijitu ya ajabu,
Lakini wewe mpenzi ni kama dhahabu

Mimi ni yatima nionee huruma,
Pia ni bikra skuwa na demu uko nyuma,
Kila nkitongoza ilikuwa inabuma,
Lakini kwako mpenzi ntakuwa imara kama chuma..

We ni mzuri, jina lako ni preta,
Nikikupata hapa JF ntapeta
Najua huwezi kunipwerepweta,
Japo snitch wanaponda, na uzushi kuleta

Preta ooooh pretaaaaaa nikubalieeeee

Preta oooh pretaaa usinizingueeee
lazima hapa aingie line walahi
 
Mapenzi ni kujituma, si uonewe huruma
Wewe hata si yatima, mali nyingi umechuma
Tochi yako naizima, gizani mpaka kiama
Huruma ni kwa walemavu na wasiojiweza, sio kwenye mahaba

Tengeru ni karibu, upweke katu hutaona
Njoo kwangu unitibu, maumivu nitapona
Tafanya taratibu, gusa kila kona
Preta achana na Vimpire_hunter, jina lake na avatar vinatisha.

Sooth maanaye mkweli, mi jina langu thabiti
Ninayo tamu asali, na kuna pipi kijiti
Achana nae wa mbali, ni kigumu kizingiti
Nitafute Tengeru Sokoni, siku ya mnada

Sina hata benzi, naamini sio kigezo
Pata na la dhati penzi, natilia sana mkazo
Hao sugu kwa uzinzi, kwao huo ndio mchezo
Preta, we will meet somewhere, someday in Arusha-I hope!
Dah! Shaaban Robert kafufuka nn maana mnapanga vina balaaa
 
Wauzaji wa mitumba, hata si watu dhalili
Ashakum! we mshamba, umeonyesha dalili
Mitumba ni adimu pamba, kuzivaa ni kama zali
Kwenye mitumba hakuna saresare, kila mtu hutoka tofauti

Preta hahitaji matunzo, anahitahi nzito huba
Kwao wanao uwezo, anapata mahitaji si haba
Hongo huleta mzozo, pesa pelekea kahaba
Hapa ni raha na utamu tu, pesa ni majaliwa-leo zipo kesho hazipo

Hamuchelewi kudai, mlivyotoa kwa hiari
Wewe mfano hai, umemdai Asha tayari
Umeruka juu kama Tai, anzisha kwangu hatari
Mbona wewe hujarudisha ulivyopewa, mpaka ukawa unahonga?

Wakujua kwa mromboo, nyama choma ya mbuzi
Nyama mpaka kokolikoo, hapana fanya ajizi
Waisikia tu moshonoo, hujafanya uchunguzi
Huko ndo kuna raha zetu sie wa 'Sokoni'

Preta kwako hoi hoi, moyo wangu watweta
Achana na huyo goigoi, maombi rasmi naleta
Kwa mwingine sitoi, kwako sana nitapepeta
Shughuli naiweza, kila siku hata ukitaka
Ntamani niyaone haya mashairi jukwaani jaman
 
Uwanjani mmekimbia, Preta mumeniachia
Mmebaki mnanyatia, moyoni mwenu mwalia
Binti anayevutia, mkonowe mmeachilia
Vimpire_Hunter na Moto, nyie moto wa mabua.

Hamuwezi kuhimili, magumu ya kupitia
Dhaifu yenu miili, hamna ya ukweli nia
Nimewazidi akili, kileleni nafikia
Mwende kimya kimya, msijeanza maneno ya mkosaji.

Uwanja huu ni mpana, mi na Preta meshibana
Bahatisheni kwa Anna, hawezi sema hapana
Ye nami tumeshikana, hatuwezi kuachana
Miss Chagga, Afrodenzi na Lara 1 nao ni wanawake, jaribuni huko.

Preta sio kama Tupa, visu butu kunolea
Mekosa mistari supa, moyoni nachekelea
Mmepata yote mifupa, nje nje amewatolea
Hiyo mistari yenu kajiribuni kwingine

Preta nipe langu Kombe, peke yangu nimesalia
Mzobemzobe nikusombe, achana na masalia
Tuchinje mkubwa ng'ombe, tusiache hata mkia
Kama Sikamona, Zawadi ya Ushindi nipatie.


Sooth debe tupu mfanowe, bila kutika hilo sio debe,
Mpaka kiboga uliwe, na zikuiishie zako ngebe,
Usilazimishe uchaguliwe, kama denti achuaguavyo mkebe,
Moto nakoleza pambano, Preta ni wangu wa enzi.

Preta ni wangu wa enzi, Vampire anajibaraguza,
Sooth hata unyoe bwenzi, Preta atakuuchuuza,
Hamuwezi nipoka wangu Mpenzi, haitotokea hiyo miujiza.
Miaka Nenda miaka rudi , Preta ndiye wangu laazizi

Preta ndiye wangu laazizi, ndiye wa moyo wangu mahamumu,
Hata kwa ndumba na mizizi, penzi letu katu hamtohujumu,
Hata muwe ving'ang'anizi, atawaona nyoka wa midimu,
Preta ndiye wangu nyonda, nina mtunza tangu enzi,

Tangu enzi nina mtunza, mapenzi na huba Nampatia,
Kutengeza magari nimemfunza, noti na kipato ajipatia,
Nimemnunulia starlet glanza, Sokoni kwa raha ajiondea,
Afrodenzi naye Lara 1, wakufaa wewe Sooth mdandiaji,

Sooth mjaribu miss chagga, huyo ni maji mara moja,
Preta wangu takubwaga, hata u jaribu mara elfu moja,
Misimamoye hakunaga, hata ulie mara elfu Mia moja.
Preta ni mmoja tu, nami moto2012 ndiye wake

Preta ni wangu waridi, mtima wangu ameujaza,
Mwendowe maridadi, tabasamule laniliwaza ,
Hakika sio mkaidi, Sooth kukuachia stoweza,
Preta wangu waepuke, Vampire naye Sooth.
 
Back
Top Bottom