Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?


Ni kweli mkuu regulations nyingi sana huwa haziwi published ila kukiw ana issue utaziona
Ila its time now sheria na kanuni nyingi kuwa published na kwa hili nilidhani TLS wana jukumu kubwa sana kuhakikisha kuwa sheria na kanuni zote zinakuwa kwenye mtandao na uwepo wa access ya sheria na kanuni kwa kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo
Ila sijui TLS wanafanya kazi gani maana kazi zao ni hizo na pia kutetea sheria na kanuni nyingi kuwa kwenye lugha ambayo inaeleweka kwa watu wote kuliko kubakia kuwa chama ambacho kinakutana kutoa matamko tuu yasiyo na nguvu au utekelezaji
 
Reactions: EMT
Ulitegemea atapata div one?! Like father like daughter ....subiri necta watampa div one ya heshima!
 


Unaongea watu wasiojua kutofautisha mazoea na sheria. Kutangaza matokeo ni BIG NO.
 
Reactions: EMT
tena mimi nimuombe mama salma kuwa kwa sasa amwangalie sana Ali.....la asivyo waaibika sana na hao watoto wao!!!

Mkuu Edson..unakaa Urisino au Maeneo Ya Regent nini?...maana unaongea vitu vya ukweli sana...na s ALi tu hata Yule Khalifani na Khalifa pamoja na Rashidi Chodo aanze kuwaangalia sasa...ila mama Salma si mwalimu kwann anashindwa kuwa na watoto karibu ili awasimamie katika ELIMU?
 
Tambua kaka baba ake ana uwezo wa kubadili yote hayo. Tusilalamike tu kwa ajili ni mtoto wa raisi. Kuna wengine pia wana athiriwa na hili. Labda mzee wake ataona sasa umuhimu wa swala la privacy.

Nimeeleza hapo juu kwamba mie siongelei mtu, naongelea system.

System nzima ya kuanika matokeo ya mitihani kwa majina, especially mtandaoni ni mbovu. Mtoto wa rais au mvuvi wa mto Rufiji.

It just so happens kwamba issue imekuwa magnified sasa.

Kaka na babayake wana uwezo wa kubadilisha hayo kivipi? Wapige simu baraza la mitihani na kuamuru matokeo yatolewe kwa namba halafu mseme Kikwete dikteta? Au wabadili vipi?
 

Mkuu hii ni changamoto na kutoa matokeo ya mtihani na kuonyesha namna wanafunzi walivyopata matokeo mabovu sio kumkatisha tamaa mtu yoyote ila ni kuionyesha jamii iangalie ukubwa wa tatizo na chanzo cha tatizo
Wanafunzi wengi wamefail sio kwamba ni huyo aliyetajwa tuu ila wako wengi sana wana zero kabisa ambazo haziwapi hata vyeti kuonyesha kuwa wamefikia form four
Je tatizo ni nini na kwa nini wanafunzi wengi hivyo wamafail mitihani yao
Je kwenye shule husika hakukuwa na continue assessment za wanafunzi husika
Je walimu wa hizo shule hawakuwa na record za wanafunzi wao kujua maendeleo yao
Walifanya nini ili kuepusha aibu ya shule zao kuwa na matokeo mabaya
Je ni walimu wabovu au ni wanafunzi ambao walikuwa wanaenda tuu shule kukamilisha ratiba
Je serikali ina mkono wake katika kufanya matokeo kuwa mabaya kihivyo kwa kuwalipa mishahara walimu ambayo haiwatoshelezi au kutohakikisha kuwa mazingira ya kusomea ni mazuri kwa wanafunzi kwa maana ya vifaa na vitendea kazi kwa walimu na wafunzi
Je huu mfumo wa zimamoto wa kuanzisha shule nyingi ambazo hazina walimu wala vitendea kazi una manufaa
Tungejiuliza hayo wala tusingekuwa tunajadili privacy za watu maana matokeo yasingekuwa mabaya wala kusingekuwa na aibu ya wanafunzi wengi kupata zero
 
Unaongea watu wasiojua kutofautisha mazoea na sheria. Kutangaza matokeo ni BIG NO.

Kwa mawazo yako mkuu yafanyweje
maana hata wangeandika no bado buku la matokeo linapatikana kwenye kila shule na mtu yoyote anaweza kwenda pale na kujionea
May be ungewashauri NECTA wawe na utaratibu wa kumtumia kila mwanafunzi matokeo yake kwenye private email yake au barua
na ujue sio wote wenye access na email au hata hizo barua
 
Huyu mtoto angepata div one mngelialia hivi?

Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
 

Kweli Mkuu TLS wanaweza kusaidia lakini pia mamlaka husika zilizopewa na bunge delegated power ya ku-legislate inabidi nao wa-publish hizo delegated legislation kwenye tovuti zao. Kwa mfano, kama NECTA wana Regulations zilizotengenzwa chini ya hiyo Act, it does not make any sense kuweka sheria mama kwenye tovuti bila ya hizo Regulations. The Act provides a general framework lakini details zinapatikana kwenye regulations, guidance, notices, etc.
 

Tatizo sio NECTA, tatizo ni sisi tunaokuwa kama hatujawahi watoto au ndugu zetu waliofeli. Kiukweli inasikitisha sana pale mwanao au ndugu yako anapofanya vibaya kwenye mtihani, hasa hasa anapokuwa the only failure.

I symphathize with Mwanaasha na her family.
 

Ungefikiria vyema tangia NECTA wameanza kutoa majina ya watu siyo leo kwa vile mtoto wa Jeykey au Pombe kafeli ndiyo privacy isisitizwe.
Mleta mada kauliza kama huyo binti anaweza kuishtaki NECTA ila siyo wanafunzi wote. Siku zote tulikuwa wapi kufikiria kuna breach of privacy?
Angefaulu huyo binti, tungesisitiza hiyo privacy? Hayo mengine uliyoongelea kuhusu utamaduni ndiyo hivyo mkuu!
 
Hata bila NECTA kutoa matokeo haya hadharani, JF wangeyakosa?
 
Watu tunatofautiana akili. Ndiyo maana kuna ule msemo: "Akili ni nywele, kila mtu ana zake". Hivi karibuni kuna mzazi huko Mkoani Pwani maeneo ya Ikwiriri kama sikosei alimfuata Mtendaji wa Kijiji na kumuuliza afanye nini na mwanae ambaye amechaguliwa kwenda Kidato cha Kwanza wakati hajui "KUSOMA na KUANDIKA". Huenda Mwanaasha aliingia Sekondari akiwa kama huyo mtoto wa Ikwiriri. Achunguzwe alivyosoma Elimu ya Msingi na maendeleo yake huko Sekondari kabla ya kujibu hoja zake huko Mahakamani. All in all hana kesi.

imwan
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
Mkuu uko sahihi kabisa. Issue ni faragha ya mtu. Nadhani hii itawafumbua macho NECTA na come next year watakuwa wamejirekebisha. Waanze kutumia namba na siyo majina. Zile namba wanazopewa wanafunzi zinakuwa zina maana gani? Pia matumizi ya ICT nadhani yapo chini sana. Miaka ya huko nyuma NBAA nasikia nao walikuwa wakiwaanika wazee wazima wakiwa wamezungusha wakati wengi wao walikuw ni mabosi, baadaye ikabidi jamaa wabadili na kuanza kuweka namba tu.

Faragha muhimu jamani. Hata humu ndani ya JF tunajitutumua na kuwasema watu openly kwa sababu tuna faragha.
 
Reactions: EMT
Huyu mtoto angepata div one mngelialia hivi?

Mods pelekeni hii thread kwenye jukwaa husika. Inaonekena watu wengi hawajui core issue inayojadiliwa humu. Wabongo tumezoea kujadili issue nyepesi nyepesi tuu.
 
Wakuu zangu,
Ni bahati mbaya sana kwamba hoja hii imetokea tu baada ya kuona mtoto wa rais kashindwa na ndiye kawa kigezo cha hoja nzima lakini kiukweli swala hili limekuwapo kwa miaka mingi sana. Kama sikosei toka wakati wa Kigoma Malima lilizungumziwa na kwa sababu nyingine tofauti kabisa..

La muhimu hapa kujiuliza ni kwamba Je, ni kweli kutoa majibu ya mitihani kwa kuweka majina ya watoto wetu ktk gazeti la serikali linavunja HAKI na UHURU wa watoto wetu?... Jibu lake ni YES..ndiyo tena kwa herufi kubwa na hakuna ubishi hata iwe yeye ni mshindi au sio mshindi..Kinachotakiwa kfanyika ni baraza hilo kutuma matokeo ya mtihani kwa mzazi iwe matokeo ya kia mwezi, semister au final badala ya kuyaweka hadharani kila mtu anayasoma.

Utaratibu mzima wa mchujo wa mitihani nchini ni utapeli mtupu, ambao umesukuma wazazi na wanafunzi kutafuta na kununua majibu ili kuwaandaa watoto wao washinde mitihani badala ya kuelimika. Huku majuu mbali na mtihani wa mwisho, mtoto anayefanya vizuri darasani, mwenye mahudhurio mazuri, tabia nzuri, mwenye kupenda kushirikiana na kuonyesha kuelimika vizuri darasani kupata mark kwa asilmia fulani ambazo huchangia ktk mtihani wa mwisho hivyo anaweza pata div 4 ktk mtihani lakini ile record yake ya darasa la saba ikambeba na kupanda hadi div 3. Na kikubwa zaidi matokeo ya mitihani hupelekewa mzazi nyumbani ktk bahasha kwa njia ya posta au mzazi mwenyewe kwenda kuchukua shuleni..

Kwa nini tumekuwa na matokeo mabaya nchini?.. ni kwa sababu elimu yetu inawa andaa watoto kushinda mtihani wa darasa la 7, na kwa bahati mbaya walimu pia hawajali sana ikiwa malipo ya kazi yake hayaridhishi. Leo hii tunalazimisha walimu kufundisha watoto wetu wakati maisha yao wenyewe yanawashinda. Hii inamsukuma mwalimui kutafuta mbinu za maisha nje ya mshahara mdogo alopewa, na ndio hapo unapokuta biashara ya maandalizi ya kushinda mtihani..Wazazi wanalipa extra kwa masomo ya jioni ili mtoto wao ashinde mtihani na kazi hiyo wanamwachia mwalimu kutafuta mitihani na kuwajazia majibu...

Hivyo ni muhimu sana tukubali pale sheria yetu inapowanyanyasa wananchi iwe mtoto wa rais au asiwe yeye na maajabu tu ni kwamba leo sheria inaonekana baada ya mtoto wa rais kuhusika, lakini siku zote watu wameifumbia macho jambo hili wakati halifai kabisa kutumika hivyo..Mimi kam a mzazi sintapenda kabisa kuona matokeo ya mwanangu yakianikwa ktk gazeti na wala sii UTU bali ni ushenzi wa sheria..

Kesho hapa JF kina Maxence wakianza kutumia majina yetu halisi au Mkandara hapa nikitaja majina yenu ktk mtandano huu mtahama wote na pengine hata kushtaki kuvunja haki yenu ya msingi lakini imekuwa rahisi kwenu kuwapinga watoto ambao kwa bahati mbaya hawana mtu wa kuwatetea isipokuwa pale mtoto wa rais anapohusika..
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.

Kama kweli una nia njema naomba unitajie wanafunzi wengine japo 10 tu ambao wamepata zero na unawaonea huruma kwa matokeo yao kuanikwa hadharani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…