Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?

Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?

I noted that as well. Mara nyingi hizi regulations haziwi published. Unakumbuka ile sheria aliyo-cite Magufuli inayompa mamlaka ya kupandish nauli feri? Wengi tulikuwa hatujawahi kuisikia. Ni mpaka itokee issue ndio zinaenda kutafutwa kwenye makabati. Lakini kama ulivyosema, hiyo sheria inaipa NECTA extensive and discretionary powers.

Ni kweli mkuu regulations nyingi sana huwa haziwi published ila kukiw ana issue utaziona
Ila its time now sheria na kanuni nyingi kuwa published na kwa hili nilidhani TLS wana jukumu kubwa sana kuhakikisha kuwa sheria na kanuni zote zinakuwa kwenye mtandao na uwepo wa access ya sheria na kanuni kwa kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo
Ila sijui TLS wanafanya kazi gani maana kazi zao ni hizo na pia kutetea sheria na kanuni nyingi kuwa kwenye lugha ambayo inaeleweka kwa watu wote kuliko kubakia kuwa chama ambacho kinakutana kutoa matamko tuu yasiyo na nguvu au utekelezaji
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ulitegemea atapata div one?! Like father like daughter ....subiri necta watampa div one ya heshima!
 
Mie naona hata miaka ile mfumo huu haukuwa sawa. Na kwa sababu tu tumekuwa tukifanya kitu namna fulani kwa "miaka yote" haina maana kwamba kufanya hivyo ni sawa.

Njia bora, kwa miaka ile na hii, ni kutoa matokeo kwa namba.

Ukizidisha habari za mitandao ndipo unapata sababu zaidi za ku protect identities za watu.

Na hapa ninachosema sisemi kwa sababu huyu binti ni mtoto wa JK. Ni kwa sababu mie ni staunch supporter wa privacy.


Unaongea watu wasiojua kutofautisha mazoea na sheria. Kutangaza matokeo ni BIG NO.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
tena mimi nimuombe mama salma kuwa kwa sasa amwangalie sana Ali.....la asivyo waaibika sana na hao watoto wao!!!

Mkuu Edson..unakaa Urisino au Maeneo Ya Regent nini?...maana unaongea vitu vya ukweli sana...na s ALi tu hata Yule Khalifani na Khalifa pamoja na Rashidi Chodo aanze kuwaangalia sasa...ila mama Salma si mwalimu kwann anashindwa kuwa na watoto karibu ili awasimamie katika ELIMU?
 
Tambua kaka baba ake ana uwezo wa kubadili yote hayo. Tusilalamike tu kwa ajili ni mtoto wa raisi. Kuna wengine pia wana athiriwa na hili. Labda mzee wake ataona sasa umuhimu wa swala la privacy.

Nimeeleza hapo juu kwamba mie siongelei mtu, naongelea system.

System nzima ya kuanika matokeo ya mitihani kwa majina, especially mtandaoni ni mbovu. Mtoto wa rais au mvuvi wa mto Rufiji.

It just so happens kwamba issue imekuwa magnified sasa.

Kaka na babayake wana uwezo wa kubadilisha hayo kivipi? Wapige simu baraza la mitihani na kuamuru matokeo yatolewe kwa namba halafu mseme Kikwete dikteta? Au wabadili vipi?
 
Nadhani wengi hamsomi na kuelewa kile mtoa mada anachosema. Kuna sheria za kulinda haki za information za watu.

Kinachofanyika sasa na Baraza la mitihani cha kutoa majina ya watu na vile walivyofanya kwenye mitihani yao sio kitendo halali.

Mwanzilishi ametumia Jina la mtoto wa Kikwete hili kuipa nguvu hoja. Lakini ukweli ni kuwa matokeo ya mitihani yanatakiwa kubakia kuwa ni information ya mtu binafasi.

Mnamsema mtoto wa Kikwete, lakini huyo wazazi wake wana nafasi. Kuna watoto wengi wanapata matokeo kama hayo na hawana nafasi za kusaidiwa. Na jinsi tunavyochukulia kuwa matokeo ya shule ni mwanzo au mwisho wa maisha, tunawakatisha tamaa watanzania wasiofaulu mitihani.

Mkuu hii ni changamoto na kutoa matokeo ya mtihani na kuonyesha namna wanafunzi walivyopata matokeo mabovu sio kumkatisha tamaa mtu yoyote ila ni kuionyesha jamii iangalie ukubwa wa tatizo na chanzo cha tatizo
Wanafunzi wengi wamefail sio kwamba ni huyo aliyetajwa tuu ila wako wengi sana wana zero kabisa ambazo haziwapi hata vyeti kuonyesha kuwa wamefikia form four
Je tatizo ni nini na kwa nini wanafunzi wengi hivyo wamafail mitihani yao
Je kwenye shule husika hakukuwa na continue assessment za wanafunzi husika
Je walimu wa hizo shule hawakuwa na record za wanafunzi wao kujua maendeleo yao
Walifanya nini ili kuepusha aibu ya shule zao kuwa na matokeo mabaya
Je ni walimu wabovu au ni wanafunzi ambao walikuwa wanaenda tuu shule kukamilisha ratiba
Je serikali ina mkono wake katika kufanya matokeo kuwa mabaya kihivyo kwa kuwalipa mishahara walimu ambayo haiwatoshelezi au kutohakikisha kuwa mazingira ya kusomea ni mazuri kwa wanafunzi kwa maana ya vifaa na vitendea kazi kwa walimu na wafunzi
Je huu mfumo wa zimamoto wa kuanzisha shule nyingi ambazo hazina walimu wala vitendea kazi una manufaa
Tungejiuliza hayo wala tusingekuwa tunajadili privacy za watu maana matokeo yasingekuwa mabaya wala kusingekuwa na aibu ya wanafunzi wengi kupata zero
 
Unaongea watu wasiojua kutofautisha mazoea na sheria. Kutangaza matokeo ni BIG NO.

Kwa mawazo yako mkuu yafanyweje
maana hata wangeandika no bado buku la matokeo linapatikana kwenye kila shule na mtu yoyote anaweza kwenda pale na kujionea
May be ungewashauri NECTA wawe na utaratibu wa kumtumia kila mwanafunzi matokeo yake kwenye private email yake au barua
na ujue sio wote wenye access na email au hata hizo barua
 
Huyu mtoto angepata div one mngelialia hivi?

Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
 
Ni kweli mkuu regulations nyingi sana huwa haziwi published ila kukiw ana issue utaziona
Ila its time now sheria na kanuni nyingi kuwa published na kwa hili nilidhani TLS wana jukumu kubwa sana kuhakikisha kuwa sheria na kanuni zote zinakuwa kwenye mtandao na uwepo wa access ya sheria na kanuni kwa kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo
Ila sijui TLS wanafanya kazi gani maana kazi zao ni hizo na pia kutetea sheria na kanuni nyingi kuwa kwenye lugha ambayo inaeleweka kwa watu wote kuliko kubakia kuwa chama ambacho kinakutana kutoa matamko tuu yasiyo na nguvu au utekelezaji

Kweli Mkuu TLS wanaweza kusaidia lakini pia mamlaka husika zilizopewa na bunge delegated power ya ku-legislate inabidi nao wa-publish hizo delegated legislation kwenye tovuti zao. Kwa mfano, kama NECTA wana Regulations zilizotengenzwa chini ya hiyo Act, it does not make any sense kuweka sheria mama kwenye tovuti bila ya hizo Regulations. The Act provides a general framework lakini details zinapatikana kwenye regulations, guidance, notices, etc.
 
Mie naona hata miaka ile mfumo huu haukuwa sawa. Na kwa sababu tu tumekuwa tukifanya kitu namna fulani kwa "miaka yote" haina maana kwamba kufanya hivyo ni sawa.

Njia bora, kwa miaka ile na hii, ni kutoa matokeo kwa namba.

Ukizidisha habari za mitandao ndipo unapata sababu zaidi za ku protect identities za watu.

Na hapa ninachosema sisemi kwa sababu huyu binti ni mtoto wa JK. Ni kwa sababu mie ni staunch supporter wa privacy.

Tatizo sio NECTA, tatizo ni sisi tunaokuwa kama hatujawahi watoto au ndugu zetu waliofeli. Kiukweli inasikitisha sana pale mwanao au ndugu yako anapofanya vibaya kwenye mtihani, hasa hasa anapokuwa the only failure.

I symphathize with Mwanaasha na her family.
 
Hapa ulichofanya, huja address issue ya privacy. Umei dismiss. Umeihalalisha kwa sababu privacy imevunjwa kwa wote.

Hujasema kwamba lack of privacy ni nzuri au mbaya.

Ni kama vile mtu mmoja akilalamika kwamba mtoto wake kauawa katika genocide ya Rwanda halafu wewe ukaja kusema "genocide my foot, wangapi wameuawa uje kusema wewe tu"

Two wrongs don't make a right. Kitu kibaya ni kibaya tu, kikifanyika kwa mtu mmoja au wengi. Tatizo ni kile kitu nilichokisema mwanzo, wabongo wengi tunaogelea katika maji ya kukosa privacy. Hewa tunayoivuta imechafuliwa na kukosa privacy na wala hatujui hili.

Bongo si ajabu mtu kukosa concept ya personal space na kukuongelesha all up in your face!! Hatuna sense of privacy.

Wewe mtu anakaa chumba kimoja na baba na mama yake pamoja na wadogo zake watatu, chumba kimepigwa pazia upande wa pili wanalala baba na mama. Huyu by default ukimwambia kwamba matokeo ya mtihani yanatakiwa kuwa private hawezi kukuelewa.

Kwa sababu nyumbani hata baba anapomjua mama hakuna privacy. Maybe this is an extreme example, lakini ukweli ni kwamba wengi tunaishi / tumeishi katika small variations za hilo. Kwa hiyo ndiyo maana ni rahisi kusema "privacy my foot". Si utamaduni wetu!

Mtu anaoga choo cha passport size ukipita nje unamuona, leo unataka kumwambia matokeo ya mtihani yanatakiwa kuwa private atakuelewa vipi?

Ndiyo predicament yetu wabongo hii. Naona watu wanaongelea sana sheria, ni vizuri. Lakini sheria bila utamaduni tutabaki na sheria kwenye vitabu.

Kinachotakiwa hapa ni kuimarisha uchumi na kubadili utamaduni.

Ungefikiria vyema tangia NECTA wameanza kutoa majina ya watu siyo leo kwa vile mtoto wa Jeykey au Pombe kafeli ndiyo privacy isisitizwe.
Mleta mada kauliza kama huyo binti anaweza kuishtaki NECTA ila siyo wanafunzi wote. Siku zote tulikuwa wapi kufikiria kuna breach of privacy?
Angefaulu huyo binti, tungesisitiza hiyo privacy? Hayo mengine uliyoongelea kuhusu utamaduni ndiyo hivyo mkuu!
 
Hata bila NECTA kutoa matokeo haya hadharani, JF wangeyakosa?
 
Watu tunatofautiana akili. Ndiyo maana kuna ule msemo: "Akili ni nywele, kila mtu ana zake". Hivi karibuni kuna mzazi huko Mkoani Pwani maeneo ya Ikwiriri kama sikosei alimfuata Mtendaji wa Kijiji na kumuuliza afanye nini na mwanae ambaye amechaguliwa kwenda Kidato cha Kwanza wakati hajui "KUSOMA na KUANDIKA". Huenda Mwanaasha aliingia Sekondari akiwa kama huyo mtoto wa Ikwiriri. Achunguzwe alivyosoma Elimu ya Msingi na maendeleo yake huko Sekondari kabla ya kujibu hoja zake huko Mahakamani. All in all hana kesi.

imwan
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
Mkuu uko sahihi kabisa. Issue ni faragha ya mtu. Nadhani hii itawafumbua macho NECTA na come next year watakuwa wamejirekebisha. Waanze kutumia namba na siyo majina. Zile namba wanazopewa wanafunzi zinakuwa zina maana gani? Pia matumizi ya ICT nadhani yapo chini sana. Miaka ya huko nyuma NBAA nasikia nao walikuwa wakiwaanika wazee wazima wakiwa wamezungusha wakati wengi wao walikuw ni mabosi, baadaye ikabidi jamaa wabadili na kuanza kuweka namba tu.

Faragha muhimu jamani. Hata humu ndani ya JF tunajitutumua na kuwasema watu openly kwa sababu tuna faragha.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Huyu mtoto angepata div one mngelialia hivi?

Mods pelekeni hii thread kwenye jukwaa husika. Inaonekena watu wengi hawajui core issue inayojadiliwa humu. Wabongo tumezoea kujadili issue nyepesi nyepesi tuu.
 
Wakuu zangu,
Ni bahati mbaya sana kwamba hoja hii imetokea tu baada ya kuona mtoto wa rais kashindwa na ndiye kawa kigezo cha hoja nzima lakini kiukweli swala hili limekuwapo kwa miaka mingi sana. Kama sikosei toka wakati wa Kigoma Malima lilizungumziwa na kwa sababu nyingine tofauti kabisa..

La muhimu hapa kujiuliza ni kwamba Je, ni kweli kutoa majibu ya mitihani kwa kuweka majina ya watoto wetu ktk gazeti la serikali linavunja HAKI na UHURU wa watoto wetu?... Jibu lake ni YES..ndiyo tena kwa herufi kubwa na hakuna ubishi hata iwe yeye ni mshindi au sio mshindi..Kinachotakiwa kfanyika ni baraza hilo kutuma matokeo ya mtihani kwa mzazi iwe matokeo ya kia mwezi, semister au final badala ya kuyaweka hadharani kila mtu anayasoma.

Utaratibu mzima wa mchujo wa mitihani nchini ni utapeli mtupu, ambao umesukuma wazazi na wanafunzi kutafuta na kununua majibu ili kuwaandaa watoto wao washinde mitihani badala ya kuelimika. Huku majuu mbali na mtihani wa mwisho, mtoto anayefanya vizuri darasani, mwenye mahudhurio mazuri, tabia nzuri, mwenye kupenda kushirikiana na kuonyesha kuelimika vizuri darasani kupata mark kwa asilmia fulani ambazo huchangia ktk mtihani wa mwisho hivyo anaweza pata div 4 ktk mtihani lakini ile record yake ya darasa la saba ikambeba na kupanda hadi div 3. Na kikubwa zaidi matokeo ya mitihani hupelekewa mzazi nyumbani ktk bahasha kwa njia ya posta au mzazi mwenyewe kwenda kuchukua shuleni..

Kwa nini tumekuwa na matokeo mabaya nchini?.. ni kwa sababu elimu yetu inawa andaa watoto kushinda mtihani wa darasa la 7, na kwa bahati mbaya walimu pia hawajali sana ikiwa malipo ya kazi yake hayaridhishi. Leo hii tunalazimisha walimu kufundisha watoto wetu wakati maisha yao wenyewe yanawashinda. Hii inamsukuma mwalimui kutafuta mbinu za maisha nje ya mshahara mdogo alopewa, na ndio hapo unapokuta biashara ya maandalizi ya kushinda mtihani..Wazazi wanalipa extra kwa masomo ya jioni ili mtoto wao ashinde mtihani na kazi hiyo wanamwachia mwalimu kutafuta mitihani na kuwajazia majibu...

Hivyo ni muhimu sana tukubali pale sheria yetu inapowanyanyasa wananchi iwe mtoto wa rais au asiwe yeye na maajabu tu ni kwamba leo sheria inaonekana baada ya mtoto wa rais kuhusika, lakini siku zote watu wameifumbia macho jambo hili wakati halifai kabisa kutumika hivyo..Mimi kam a mzazi sintapenda kabisa kuona matokeo ya mwanangu yakianikwa ktk gazeti na wala sii UTU bali ni ushenzi wa sheria..

Kesho hapa JF kina Maxence wakianza kutumia majina yetu halisi au Mkandara hapa nikitaja majina yenu ktk mtandano huu mtahama wote na pengine hata kushtaki kuvunja haki yenu ya msingi lakini imekuwa rahisi kwenu kuwapinga watoto ambao kwa bahati mbaya hawana mtu wa kuwatetea isipokuwa pale mtoto wa rais anapohusika..
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.

Kama kweli una nia njema naomba unitajie wanafunzi wengine japo 10 tu ambao wamepata zero na unawaonea huruma kwa matokeo yao kuanikwa hadharani
 
Back
Top Bottom