Mkuu Pasco, usidhani sina ufahamu kwa kile nilichokieleza, inawezekana tu labda namna ya nilivyokiwasilisha ndio hukunielewa, maana yangu kubwa ni kwamba hawa ni mafisadi na wametajirika kwa migongo ya Watanzania ndio maana hawa hata mahakamani wao wanaona ni kwenda kupoteza muda tu.
Huyu Sinare unayemsema wewe sio ndio yule wakili alietuingiza mkenge kupinga malipo ya Dowans huku akijuwa hukumu inatamka kwamba mahakama ya usuluhishi ndio ya mwisho!!?? je huyu hana undugu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani? Je unaweza kututhibishia uhalali wa utajili wa Ridhiwani miaka 5 tu baada ya kumaliza chuo kikuu?
Mkuu Matola, Dr. Hawa na Mwanaidi ni sisters na wote ni lawyers na walikuwa patners kwenye Epitome Law Firm. Ni kweli Dr. Sinare amehusika in one way or another kuandika legal opinion ya Dowans but its through a specific legal firm hivyo hiyo firm ndio itabeba corporate liability!.
Kuhusu ukwasi wa kutisha in a short period of time. Its possible!. Nina class mate wangu ni Lawyer, kuna siku nilimuibukia kwenye law firm yaka anifanyie paper work nipate bond ya M.10 nikatibiwe South, baada ya kuniona hali niliyokuwepo, alivuta draw akatoa US 10,000 cash! na kuniwekea mezani na kuniambia just take!. Nikasita kwa sababu bond niliohitaji ni ya TZS M.10 hivyo hiyo US $ 10,000 ni over and above sitaweza kulipa!. He said take it and go!.
Ndipo akanieleza he did a single transaction worth billions and his legal feez is above 10 Billions!. Jamaa alinunua a beach house masaki, bought himself 2 vogue in UK na akazileta aboard British Airways Cargo!, akalipia ushuru TZS 86 Millions each!. Sasa ameturn in real estate developer amezinunua hizo nyumba za Oysterbay na kuzi re develop. Law firm ipo kaajiri vijana.
Ukiona success ya ghafla kwa watu basi ndio unageuka fisadi!.
Kitu kimoja ambacho ni wazi, ili kushika hizo super deals, one got to have connections!. Kijana ni lawyer kama my friend who is nobody amevuna more than 10 bilions in a single transaction how about somebody?!.
Ila pia kutokana na lever ya umasikini wetu, we have lots of hate preachers kwa kila mwenye nacho kumuita fisadi!. Kwetu uswazi Vogue imebatizwa jina ni gari ya mafisadi, whoever atakayeshuka toka ndani ya vogue ni fisadi hata kama umepewa lift tuu!.