Private schools (English medium) ada kupanda maradufu 2023. Serikali iingilie kati

huna pesa....acha kutuletea excuse ya kijinga.
 
Kuna jirani yangu nyumba ilipigwa mnada na bank, alikopa hela bank kwajili ya ada za watoto walikuwa wanasoma sijui FEZA SCHOOL, Sasa bwana hile corona ya Kwanza mwaka 2021, biashara zake ziliporomoka vibaya Sana.

Nyumba ikapigwa mnada na watoto wameenda shule za kawaida huko kwa Bibi yao, na wao wameenda kupanga,

Nadhani muda mwingine Inatakiwa tujikune tunapoweza
 
Masikini kwa kujifaraji hawajambo, kwani pesa alikopa kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya ada za shule?
 
Masikini kwa kujifaraji hawajambo, kwani pesa alikopa kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya ada za shule?
Halafu ukute wewe ni kula kulala tu kwa shemeji unaita watu masikini mbbwa wewe,
Unataka kila mtu aonyeshe humu anachomiliki au ana wadhifa gani kennge wewe?

hapo wapi nimemaanisha ni kujifariji?kuelezea Jambo ambalo lilimtokea mtu ni kujifariji mmbwa wewe
 
Masikini kwa kujifaraji hawajambo, kwani pesa alikopa kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya ada za shule?
Kwahiyo Mimi nawewe Nani anajua zaidi kuwa huyo alikopa kwajili ya kitu gani Kati ya hivyo?

Maana ni jirani yangu na Ni mshkaji pia.
 
Kwahiyo Mimi nawewe Nani anajua zaidi kuwa huyo alikopa kwajili ya kitu gani Kati ya hivyo?

Maana ni jirani yangu na Ni mshkaji pia.
Benki ya biashara haiwezi kukopa mtu ada ya shule wanakopesha kwenye biashara, labda kama alikopa kwenye his microfinence au sacco
 
Niliwahi kutana na hio, unakuta watoto wote wamepangwa wa kwanza hadi wa 10 na shule Darasa lilikuwa na watoto 40, unakuta No 1 ina watoto kama 6
 
Mpeleke mtoto shule za serikali na uwe unamkagua na kumfanyia usimamizi, inatosha kabisa.

Wanangu wanasoma Kayumba nawakagua, vitabu vyote nimewanunulia.

Na ratiba ya kusoma nimewapangia kuanzia 7:00 hadi saa 8:30 usiku niwakute mezani. Saa 8:30 hadi saa 9:00 kula.

Saa 9:30 wawe kitandani. Tamthilia wataangalia wiki endi.

Sisi wazazi wao tumesoma shule hizo hizo za St Kayumba na leo tuna masters, na mambo yanaenda.

Wengine wanapeleka watoto huko academy kufuata mkumbo tu. Hasa wazazi wasiosoma shule wazazi wenye elimu ndogo, wazazi vilaza, wanajivunia mtoto kuongea ze ze wanaona ndio mwanao anapaata elimuu.

Hitimisho kama uwezo unaruhusu mpeleke, lakin kama wewe mwenyewe kodi inakushinda halafu unakuja kutupigia kelele hapa.
 
Dah!! The struggle is real. Kayumba ni changamoto mkuu. Watoto wanahudhuria shule tu.

Walimu wana stress..pesa hamna madeni..hakuna ufundishaji
Mbona wanafundisha? Huko English Medium wanako karirisha watoto ndiko unaona kuna elimu?
 
Na watapandisha kweli hawa jamaa.
 
Mchele umepanda, maharage yamepanda, Reem zimepanda, Mahindi yamepanda, Mafuta ya kula yamepanda, Petrol, deasel, kila kitu kimepanda kwanini ada isipande....

Watoto shule watakula Mawe,?

Nilikuwa naangalia budget moja ya kufanya mtihani kwa shule moja ya serikali tena ya kata ni million karibu 7 maana yake Hawa wanatumia Kama 28 million kwa mwaka mmoja kwa mithihani tu tena ya ndani sio ya nje.

Mimi naona ipande hata kwa 50% Ili tuweze kujiendesha na kulipa kodi, other wise tupewe ruzuku au zikose walimu Bora, tuue ajira, na tuue elimu maana watoto wa wakubwa wote ndio tupo nao huku wanasoma.

Other wise tuzifunge
 
Itakua una uelewa duni na umuhimu wa 'msingi'..elimu ya msingi ni muhimu,yapasa kuwa bora
 
Acha uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…