Private schools (English medium) ada kupanda maradufu 2023. Serikali iingilie kati

Haahahaa. Sawa Mkuu!!
 
Benki ya biashara haiwezi kukopa mtu ada ya shule wanakopesha kwenye biashara, labda kama alikopa kwenye his microfinence au sacco
ujanisoma vizur, nikwamba pesa nyingine aliingiza kwenye biashara yake, nyingine %kubwa ni ada ya watoto 2, changamoto ya Covid19 ilipelekea biashara kuyumba then na mengineyo yakatokea
 
Yaani serikali iache kuimarisha shule zake hazina vyoo na madawati ije kusaidia shule private zenu matajiri?
 
Kwa nini serikali iingilie kati? Hii itakuwa double standard ambayo tunaipigia kelele na kuipinga kila siku.

Sasa hivi bidhaa za chakula mf. mahindi, maharage na mchele vimepanda sana mpaka wengine tunakula mlo 1 kutwa lakini serikali haijaingilia kati kudhibiti bei hizo. Tunaambiwa ni msimu wa wakulima kupiga hela. Sasa tusubiri huu msimu wa shule kupiga hela. Wala msiwabughudhi. Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, Wallah!
 
Hizi shule za gharama zinawafilisi wazazi, au zinawachelewesha kupata maendeleo; kuna mtu namfahamu, kipato chake laki 5, kasomesha mtoto chekechea mpaka la saba, ada shilingi milioni 2.5 kwa mwaka; kijana akafaulu na kupangiwa shule ya serikali.

Akampeleke tena private, kwa ada ya milioni 3 kwa mwaka; sasa yuko kidato cha tatu; mzazi wake ana ha ha; ata kununua nguo mpya avae imekuwa shida.

Mwisho wa siku, huyu kijana atakuja akutane na kijana aliyesoma kayumba pale chuo kikuu; sasa hapo sijui ni nani ataonekana mjanja?​
 
Haya mawazo yanatoka kwa sababu ya umasikini..shule za elimu bure ni majanga matupu..pili hizo gharama za kuwalipa hao walimu wa twisheni sidhani kama zitapishana sana na ada ya mwaka ya private.

Kaa chini upige hesabu vzr.

Nashauri tuendelee kusaka hela ili kuwapa elimu bora watoto na pia kuwapa urithi mwisho wa siku.

#MaendeleoHayanaChama
 
Suala siyo vyeti Bali elimu
 
Na shule nyingi za English medium watoto wengi wanaanza kuaribikia huko na ushoga na usagaji unaanzia huko nimeshaona mifano mingi na mwisho wa siku mzazi unaanzia kulalamika mtoto ameharibika na kumbe wewe ndio chanzo
 
Tafuta hata akili ya kuazima
 
Wapo sahihi kabisa kupandisha ada kwa kuwa shule ni mali yao, hiyo ni biashara (wanatafuta faida na soko ndio huamua bei/ada). Kama huridhiki na ada zao wewe achana nao tu. Shule za pasipo kulipa ada (elimu bure) zipo nyingi sana, mpeleke mwanao huko ukiona huwezi kulipa hizo ada za private.

Kizuri gharama ndugu.
 
Aisee ,kuna shida sana. And there is no guarantee to a brighter future.
 

Nakuelewa lazima ulinde ugali wako.

Safari ya elimu Tanzania wanaofanya vizuri darasani vyuo vikuu huwa wanakutana udsm,mzumbe na Muhas .. haijalishi umesoma kayumba ama shule zenu za kina junior

Nenda udsm hata leo hii kafanye research wangapi wamesoma kayumba primary na wangapi wamesoma shule zenu za kinyonyaji..

Elimu ni content na sylabus sio lugha peke yake....

Mtoto wa shule ya msingi Madenge anafundishwa same sylabus yenye content hizo hizo ambazo wa tusiime primary school anafundishwa tofauti ni lugha ya kufundishia tu.

Sasa why ununue same content kwa bei ya milioni 2. Wakati mwenzako anazipata bure... na mwisho wa siku baada ya kidato cha sita hao wa madenge na tusiime wote wanakutana udsm na kwenye ajira za utumishi na mshahara sawa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…