Private schools (English medium) ada kupanda maradufu 2023. Serikali iingilie kati

English Medium Schools siyo kwa ajili ya kila mtu.

Nyie wazazi mnaotaka serikali ipeleke pua kule mnataka hizo shule ziwe kama za serikali.
 
Wazazi jikuneni mnapofikia kama una uwezo mpeleke private kama ni apeche alolo mbombo ngafu mlete kidumu na mfagio. Kitu kingine nafikiria mtoto hata ukimleta shule za serikali ukimsimamia na ukawa mfuatiliaji mzuri atafaulu tu.
 
Mtu aliyeelimika vizuri atajiongoza vyema
Hamna kitu hapo; tutapambana nao kwenye hizi nafasi chache za tamisemi; usikubali uingie mtego wa kuwekeza gharama kubwa, ile ni biashara mkuu; wekeza gharama kubwa kama anaenda kusoma chuo cha nje mfano Oxford, Harvard na asome fani technical zenye tija, sio mambo ya history, sociology n.k.​
 
Akili yako imeishia kwenye kuajiriwa...kwa kuwa umepata elimu mbovu
 
Ipande tu tubaki wachache
 
Kwaio mzee inawezekana haujasimama vizuri kwenye maisha jipange msomeshe mtoto shule bora kua na masters sio hata tija..shule za private mtoto anapata na exposure hawezi kua mzembe mzembe...🤣🤣🤣
 
Hao wanaonunua syllabus kwa 2m ni sababu wazazi wao wanamudu kulipa..tukija kwenye ajira hao wa private wengi hu opt kwenda private wakati waliosoma shule za umma huamini kwa public employment ndo kila kitu...nkt hao wengine exposure inawawezesha kujua public employment haina issue yoyote...90% ya wanaolalamikia ajira za serikali wamesoma shule za serikali waliopiga private education hawataki hata kuzisikia hizo ajira za serikali za 900k kwa mwezi...🤣🤣😍
 
Sasa mkuu kama ni same content ...kwanini Private schools ndio zinaongoza mitihani ya kitaifa!!?
 
Sasa mkuu kama ni same content ...kwanini Private schools ndio zinaongoza mitihani ya kitaifa!!?
Ni sawa na kuku wa kienyeji anayejitafutia chakula chake mwenyewe vs kuku wa kisasa anayeletewa chakula; yule wakisasa atanona tu
 

Ndiyo, huko hakuna ada! Na walimu wengi wanaofundisha Private schools ni hawa hawa wa Kayumba, kwa hiyo tupeleke huko watoto wetu!
 
Na shule nyingi za English medium watoto wengi wanaanza kuaribikia huko na ushoga na usagaji unaanzia huko nimeshaona mifano mingi na mwisho wa siku mzazi unaanzia kulalamika mtoto ameharibika na kumbe wewe ndio chanzo
Kwa hili napinga hii ipo kwa shule zote la muhimu nikuwaombea watoto wetu wawe na hofu ya Mungu na pia kuongea nao... Nina watoto ninao wafahamu wapo shule za kawaida wengine walianza kusagana darasa la 4 mzazi amekuja kugundua mtoto yuko la saba. Walimu wanasema hawana cha kufanya maana watoto wengi katika hiyo shule wako hivyo..
 
Braza mahindi kilo ni 1500, maharagwe kilo ni 3400, mchele kilo ni 2800.
Mafuta ni 125.000 kwa ndoo, kuni hazishikiki na bado wafanyakazi ulionao na wao inabidi waongezewe mshahara maana tayari na wao wananunua bei hiyo hiyo. Petroli na dizeli ni 3000+ kwa lita. Mchukue mwanao mpeleke serikalini kabla ya mwakani. Hakuna namna vitu havitapanda bei aisee yani hakuna kabisaaaa
 
Wewe uwezo ndo unao kusumbua tu hamna lolote sabb zako hazina mashiko
Sasa mbona mnalalamika wanapandisha Ada huku mna uwezo wa kulipa , sasa lawama za nini c mlipe tu
 
Sasa mkuu kama ni same content ...kwanini Private schools ndio zinaongoza mitihani ya kitaifa!!?

Kabla sijajibu swali lako,

Unaelewa maana ya content ni nini?

Sasa najibu swali lako. Shule za private tena shule chache zinazoongoza mitihani ya kitaifa ni sababu ya factor nyingi mojawapo ni udanganyifu kwenye mitihani. Shule za private zipo zaidi ya 5000 . Je shule zote hizo 5000 huwa zinaongoza mitihani ya taifa ama shule chache kati ya hizo.

Pia Shule za private haziongozi mitihani ya kitaifa miaka yote. Kuna miaka shule za goverment zinaongoza pia.

Swali kwako pia. Je Mtaala wanaofundishiwa shule za private unazozitetea una ubora mkubwa wa maarifa ( knowledge) kuliko mtaala wanaofundishiwa shule za serikali za elimu bure?
 
Peleka kayumba mkuu , yaani serekali iingilie shule za private wakati serekali yenyewe inasimamia shule zake ambazo Ada ni bure .
Kumpeleka mtoto wako private ni kihere here chako tu, Kama huwezi mpeleke kayumba acha kulalamika , waachie wenye uwezo waende private
 
Kweli kabsa ndugu ada zimepanda mpka zinakalibia juu mbinguni Serikali itusaidie tu kwenye hili
 
Gharama za kuendesha shule ni kubwa sana kwa kweli. Nilitamani nifungue shule ila kupiga gharama za uendeshaji na uwekezaji kwenye miundo mbinu, nikaona mara kumi ni heri ufungue hoteli/ Guest...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…