Prof. Anna Tibaijuka haziivi na Rais Samia?

Prof. Anna Tibaijuka haziivi na Rais Samia?

Acheni uchonganishi, issue kubwa ni mkataba wa bandari, waliomuunga mkono wengi hata humu wamemgeuka. Mama Tibaijuka hakuna sehemu anagombana na mama, mara zote amepinga huu mkataba kwa hekima kubwa.
20230621_123143.jpg

Hamna hekima yoyote,huyo mama ni mmoja waliokua wamiliki wa ticts yeye na mhaya mwenzake karamagi lao 1,lazima wapotoshe ili kutetea maslahi yao
 
Ghafla tu Profesa Anna Tibaijuka kawa mkosoaji wa sera za Samia isivyotarajiwa!

Mengi ya maandiko yake kwa siku za hivi karibuni yanaonyesha kupinga waziwazi sera za uwekezaji za Samia.

Je, Anna ndiyo wale tuliowangojea ama tusubiri wengine?

Pia soma
View attachment 2662100
Samia anauza nchi unataka Prof.Tibaijuka akae kimya?una akili wewe?
 
Huyu aliyekuwa akizichota wakati ule, ghafla kawa mzalendo? Anyways, watu huwa wanabadilika buana.
Acheni uwongo. Prof. Tibaijuka alichota pesa kutoka wapi? Yeye alichangiwa milioni 10 kwaajili ya shule yake. Akaitolea taarifa, akalipa na kodi. Yalipotokea maneno kuwa pesa ile ilikotokea haikuwa halali, akairudisha. Sasa kosa lake lilikuwa ni lipi?

Na huyo Rugemarila waliyesema amepewa malipo yasiyo halali, baadaye imeshihirika kuwa alionewa. Akaachiwa, na wala hata pesa yake haikupokonywa na yeyote hata shilongi 1.
 
Tibaijuka huyu huyu aliyelamba mabilioni ya escrow huku akijinasibu kwamba ni hela ya mboga?

Hivi uzalendo hasa ni nini?

Mzalendo ni nani hasa?
Humu kweli tuna mambumbumbu wa kupindukia ambayo hayajui hata tofauti ya milioni na bilioni.

Hivi wewe ukapewa pesa kidogo na rafiki yako akasema nakusupport kwenye mradi wako wa matikiti, wewe uliyechangiwa una kosa gani?
 
Ghafla tu Profesa Anna Tibaijuka kawa mkosoaji wa sera za Samia isivyotarajiwa!

Mengi ya maandiko yake kwa siku za hivi karibuni yanaonyesha kupinga waziwazi sera za uwekezaji za Samia.

Je, Anna ndiyo wale tuliowangojea ama tusubiri wengine?

Pia soma
View attachment 2662100
Teuzi !!
 
Back
Top Bottom