Prof. Assad: Ni wajinga tu ndio wanaonunua ndege kwa cash

Prof. Assad: Ni wajinga tu ndio wanaonunua ndege kwa cash

Sasa kama cash ipo kwa nini tusilipe taslimu..
Watu wako bado wanachangia maji na ng'ombe kwenye sima kimoja hiyo cash inatoka wapi, wanafunzi darasani wako 100 walimu hawatoshi hiyo cash ya kuchezea inatoka wapi? barabara za vumbi kufika mawilayani, vituo vya afya viko mbali nk na hivyo nilivyokutajia hakuna anayeweza kukukopesha
 
Akiweka ushauri wake nini kifanyike baada ya huoujinga anaodai umetumika kununua ndege, ndio haitakuwa ujinga pia.
 
Uchumi level ya nchi sisawa na levo ya familia uelewe,kuna utaalamu wa kiuchumi na hesabu zake kifaida pale unapoingia kwenye big businesses!! Ndege sio bodaboda ulipe cash!! Anayo pesa mbona kunawatoto wanasoma wamekaa chini? Mbona deni lataifa limeongezeka? Msidanganyike kwa maneno ya siasa za kijinga.
Jiwe alijua kilakitu alijipa utaalamu kwenye uchumi,udaktari,kodi,uinjinia,kilimo hakutaka wataalamu wasekta kumshauri.
Ametutia hasara kubwa kwa walichosema waandishi kenya "ukaidi usiofaa"!!
Ukishauri tofauti na awazavyo unageuka adui,unafukuzwa kazi!! Wasaidizi wake walipata shida sana kwakweli
Kuna hadi waliokuwa wanalia baada ya ushauri wao kupuuzwa
 
Ila linapokuja suala la madawati. Mnatembeza bakuli? Nyumba unaishi hauna maji, badala uvute bomba, unaenda kununua gari halafu maji unaenda kuchota kwa jirani. Unajua bado kuna uhaba wa madawati?
Uongozi wa mwendazake, ukipiga picha ktk shule moja wanafunzi wanakaa chini. Ww hauna bahati, ni jela na faini juu kwasbb siyo Mzalendo
Kila mwendo una hatua zake..
 
Hii ni tweet inayoombatana na video huko twitter:

Prof. Assad anasema "..You can't buy airline by cash, hakuna yeyote anayenunua ndege kwa cash...wapi umeona?..hakuna mtu ananunua ndege kwa cash. Watu wajinga sana ndio wanaweza kufanya jambo hili..."


Aisee,this is a turnaround.Ngoja tusubiri,tutasikia mengi.Hypocrites have been loosened.

Mimi hua najiuliza, hivi kukopa kumbe ni sifa.Sijawahi kufikiri. hivyo,na sitakuja kufikiri.Siku zote nitaamini kwamba kukopa ni aibu,na the reverse is actually true.Jambo la msingi la kutambua ni kwamba akopaye ameshindwa maisha,kwa hiyo ni mjinga kiasi fulani.Hata vitabu vya dini,Biblia kwa mfano inasema,"akopaye ni mtumwa wa akopeshaye!"Sasa commonsense inaniambia kwamba hakuna mtu apendaye utumwa.

Lakini kwa nini watu wameangukia kwenye mitego ya Shetani na kukubali mifumo yake.The answer is simple,wamemuacha Mungu,kwa hiyo wanatumia akili zao,bila kuongozwa na Mungu katika kufanya mambo yao.This has made it possible for Satan to have a foothold in their lives,including Professor Assad.Hivi kama nina hela kwa nini nikope,nitalipa baadae anyway.Kwani kukopa ni sifa.Funny.

Kumuita marehemu mjinga ni kumtukana bila sababu ya msingi,na ni a desperate effort ya kumchafua.Sio uungwana hata kidogo.Nilitegemea mtu aliyefika ngazi ya CAG kiutumishi awe na hekima na busara,kumbe hamna kitu,very sad.
 
Watu wako bado wanachangia maji na ng'ombe kwenye sima kimoja hiyo cash inatoka wapi, wanafunzi darasani wako 100 walimu hawatoshi hiyo cash ya kuchezea inatoka wapi? barabara za vumbi kufika mawilayani, vituo vya afya viko mbali nk na hivyo nilivyokutajia hakuna anayeweza kukukopesha
Kumbuka Nduguzo wanasoma bure.. Changamoto hazishi alaka kama tufikiriavyo... Tufanye kazi tulipe kodi tutatue changamoto mpya na za zamani..
 
Hii ni tweet inayoombatana na video huko twitter:

Prof. Assad anasema "..You can't buy airline by cash, hakuna yeyote anayenunua ndege kwa cash...wapi umeona?..hakuna mtu ananunua ndege kwa cash. Watu wajinga sana ndio wanaweza kufanya jambo hili..."



Prof Assad kasema mengi ya ukweli.

Lakini Dr Magufuli alikuwa na mboni Kali zaidi. Duniani kote, maendeleo ya vitu yaliambatana na kudorora kwa haki za binadamu. Hii sacrifice ndio ilikuwa lengo la Dr Magufuli.

Hugo Chavez wa Venezuela alitumia hii njia, lakini madhara aliyopata ni makubwa mno.
 
Back
Top Bottom