Ndege zisizo za keshi ndizo huingiza faida??
Katika biashara ya anga, faida hutegemea mpango-mkakati wa biashara (Business Plan) na sera za nchi husika. Hili halihusiana kabisa na manunuzi ya ndege: Utaratibu mzuri ni kwamba nchi lazima iingie kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease Agreement) na mashirika husika kama ya kule Ireland, na siyo kwenda kiwandani na kuanza kutengeneza na kufuma ndege mpya kitu ambacho ni gharama.
Ukienda kiwandani hawakutozi tu bei ya utengenezaji wa ndege, bali wanaanza kukutoza bei ya pango (Slot) ambayo ndege yako itafumiwa na kutengenezwa. Gharama nyingine za matengezo, usajili, bima na waendeshaji wa hiyo ndege (Crew). Sasa kama huna mpango-mkakati wa kibiashara (Business Plan) lazima itakula kwako na hasara yako itakuwa kubwa kama ambavyo imekuwa kubwa hapa kwetu.
Lakini ukiingia kwenye mkataba wa matumizi ya ndege (Aircraft Lease Agreement) unaweza ukasaini mkataba mkubwa (Wet-Lease) ambapo, shirika linalokuzima wewe ndege (The Lessor) litahakikisha kwamba lenyewe ndiyo litalipia gharama za matengenezo ya hiyo ndege, bima, waendeshaj (Crew) na mengineyo ambayo mtakubaliana. AU unaweza kuingia kwenye mkataba mdogo (Dry-Lease) ambaopo kampuni (Lessor) litakupa wewe ndege lakini gharama za matengenezo, bima na waendeshaji ni za kwako wewe mtumiaji (Lessee).
Sasa huu utaratibu husaidia sana kwasababu biashara ya ndege ina matatizo mengi (High Risks) na wakati wowote unaweza kupata hasara zitokanazo na mambo kama vita, mlipuko wa magonjwa, ushindani mkubwa, mabadiliko makubwa ya teknolojia au madeni ya kimataifa. Sasa unaweza kuamua kuingia kwenye mkataba mkubwa (wet-lease) au mdogo (dry-lease) kwa muda mfupi ili uweze kupima kama unaweza kupata faida au hasara; ukiona umepata faida basi ndipo unaweza kuingia mkataba wa muda mrefu au kununua kabisa.
Kibaya zaidi ni kwamba sisi, Tanzania tuna madeni mengi ya kimataifa jambo ambalo lilipelekea kutokuwa na safari nyingi za kimataifa kama ilivyotegemewa. Ndege ikienda nje wadai wetu wanaweza kwenda mahakamani na kuzikamata kama walivyofanya kipindi kile CANADA na AFRIKA KUSINI, jambo ambalo lilipelekea sisi kupoteza mabilioni ya pesa bila sababu za msingi. Tungekuwa kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease) wasingeweza kukamata zile ndege hata kama zingekuwa zinatumiwa na ATCL kwasababu siyo za Tanzania.
Lakini njia nyingine rahisi kama tumenunua ndege kwa pesa taslimu ni kuhakikisha tunasajili kampuni la ndege nje ya Tanzania, kwenye nchi rafiki kama Uchina halafu hilo shirika litaingia kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease) na ATCL ili ndege zionekane siyo za kwetu. AU tungeweza kutengeneza kampuni hapa nchini ambalo itaonyesha linamilikiwa na bodi ya wadhamini (Board of Trustees) wa Kanisa kubwa kama Roman Catholic au Lutheran au yote kwa pamoja kisha wao ndiyo wakanunua hizo ndege ikaonesha kwamba ni za kwao lakini kumbe hela ni za serikali.
KIBIASHARA: Biashara ya usafiri wa anga, huendeshwa kwa gharama kubwa sana na mara zote faida huwa hazitokani na safari za anga bali shughuli nyingine ambazo usafiri huo wa anga unalenga kuzikuza na kuzifanikisha: Mfano shughuli za kitalii na kibiashara. Makampuni kama Continental Airlines, Delta Airlines au Fly-Emirates huendeshwa kwa gharama kubwa hivyo shughuli za kitalii na kibiashara ambazo zinawezeshwa na usafiri wa anga hufidia uendeshaji wa hayo mashirika. Tanzania kuna shughuli gani kubwa ambayo ingefanikishwa na usafiri wa anga ndani na kimataifa hadi kuzalisha faida ambayo ingetumika kufidia gharama za uendeshaji wa ATCL ????
Hivyo mwisho kabisa watu wanaotudai hawawezi kukamata mali ya makanisa makubwa na yenye ushawishi duniani kama hayo maana siyo mali ya serikali. Hivyo haya makanisa yataamua kwamba yaingie mkataba sasa wa matumizi ya ndege na ATCL. Lakini sisi tulidhani ni sifa kujisifia mbele ya wale wazungu kwamba tunanunua ndege kwa pesa taslimu ilhali wao hawatupendi kabisa, wanatupa misaada, tunakopa kwao na wanatudai, figisu lazima wakufanyie tu. Marekani, Uchina na Urusi wanatumia sana huu mchezo kwenye biashara mbalimbali ili kukwepa vikwazo vya kimataifa visivyo vya msingi.
Kubwa zaidi mashirika makubwa yaliyofanikiwa kwenye biashara za anga kama KLM, huwa yanakuwa yanashirikiana na mashirika ya nchi nyingine (In Partnership or Joint-Venture). Kwamba nchi moja itatoa wahandisi wa ndege (Auronatic Engineers), nyingine itatoa waendeshaji (Crew Members), nyingine italipia bima na nyingine itatoa eneo la uwekezaji (Area for investment). Mwaka 1922 Urusi ya Kisovieti (The Soviet Union) ilifanya hivi na Ujerumani (The Weimer Republic) na nakumbuka hata KLM imewahi kufanya hivi na Airfrance, (Japo sikumbuki ni mwaka gani na mkataba wao ulisemaje).....
Namalizia kwa kusema mitazamo ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya siasa, UJAMAA umedumaza fikra za watanzania. Ndiyo maana hata ukienda sehemu nyeti kama Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshini na Vyuo Vikuu unaweza kukutana na mtu mwenye fikra finyu hadi ukabaki mdomo wazi (They are crude, dimwitted and lackadaissical ): Shirika la ndege la Tanzania haimaniishi lazima liwe linamilikiwa na serikali ya Tanzania, raia wa Tanzania wakimiliki shirikia kubwa lenye faida ni sifa njema kwa nchi.
Ndiyo maana nchi kama Marekani biashara ya ndege hufanywa na watu binafsi chini ya uangalizi mkubwa wa serikali. Hata Ulaya nako mashirika mengi yanamilikiwa na watu binafsi kwa ushirikiano na serikali. Rais Paul Kagame, naye ashaanza kufanya hivi na waarabu kwenye Air-Rwanda, na siyo muda atawashinda na kufika mbali (The Man Knows the rules of the game).
Sasa ninyi endeleeeni kusikiliza The PolePolez, The Bashiruz an The Kabudiz na wengine wote wenye COLD-WAR NOSTALGIA ambao bado wanaishi karne ya ishirini halafu muone matokeo yake.Ukiataka kuamini nachokisema wewe angalia tu kwenye teuzi: Yaani TISS kwasababu wazijuazo wao wenyewe wakaamua kupeleka kada kutoka UVCCM akaongoze TPDC (One among critical Industries of the State).
Yaani hili linchi tumekuwa kama Pakistan (A Diabolical Mafia State), kila sehemu nyeti kuanzia mashirika ya umma yanaongozwa na mijasusi na wanajeshi, lanchi haliendi mbele, huku wenzake India wanapiga hatua kubwa kiuchumi. Nilikuwa nakasirika sana zamani, lakini baada ya kujua kwamba hii nchi iko kwenye AUTO-PILOT na kuko salama kwasababu ya NEEMA ZA MUNGU, nimeamua kufanya mambo yangu na familia yangu.
HII NCHI BADO TUNA SAFARI NDEFU SANA, HIVYO KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE.......