Nyamatare1987
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 416
- 493
Tuna maprofesa wajinga sana hapa Tanzania
Ndege zisizo za keshi ndizo huingiza faida??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndege zisizo za keshi ndizo huingiza faida??
Mjinga ni mtu ambae hajui lakini akielimishwa anajua na ujinga unaisha.Kwanini anamtukana merehemu.. Elimu bado haija msaidia kutumia lugha nzuri.
Kwa kauli hii huyu nguli Prof Assad,Jiwe angekuwepo lazima wasiojurikana wangefsnya yaoHii ni tweet inayoombatana na video huko twitter:
Prof. Assad anasema "..You can't buy airline by cash, hakuna yeyote anayenunua ndege kwa cash...wapi umeona?..hakuna mtu ananunua ndege kwa cash. Watu wajinga sana ndio wanaweza kufanya jambo hili..."
Umeandija maelezo mengi sana,ila hujaonyesha gharama ya ku-lease na gharama ya kununua cash,yaani unataka kutuaminisha kwamba lessor hataweka profit kufidia yote hayo anayosema,acheni ujingaKatika biashara ya anga, faida hutegemea mpango-mkakati wa biashara (Business Plan) na sera za nchi husika. Hili halihusiana kabisa na manunuzi ya ndege: Utaratibu mzuri ni kwamba nchi lazima iingie kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease Agreement) na mashirika husika kama ya kule Ireland, na siyo kwenda kiwandani na kuanza kutengeneza na kufuma ndege mpya kitu ambacho ni gharama.
Ukienda kiwandani hawakutozi tu bei ya utengenezaji wa ndege, bali wanaanza kukutoza bei ya pango (Slot) ambayo ndege yako itafumiwa na kutengenezwa. Gharama nyingine za matengezo, usajili, bima na waendeshaji wa hiyo ndege (Crew). Sasa kama huna mpango-mkakati wa kibiashara (Business Plan) lazima itakula kwako na hasara yako itakuwa kubwa kama ambavyo imekuwa kubwa hapa kwetu.
Lakini ukiingia kwenye mkataba wa matumizi ya ndege (Aircraft Lease Agreement) unaweza ukasaini mkataba mkubwa (Wet-Lease) ambapo, shirika linalokuzima wewe ndege (The Lessor) litahakikisha kwamba lenyewe ndiyo litalipia gharama za matengenezo ya hiyo ndege, bima, waendeshaj (Crew) na mengineyo ambayo mtakubaliana. AU unaweza kuingia kwenye mkataba mdogo (Dry-Lease) ambaopo kampuni (Lessor) litakupa wewe ndege lakini gharama za matengenezo, bima na waendeshaji ni za kwako wewe mtumiaji (Lessee).
Sasa huu utaratibu husaidia sana kwasababu biashara ya ndege ina matatizo mengi (High Risks) na wakati wowote unaweza kupata hasara zitokanazo na mambo kama vita, mlipuko wa magonjwa, ushindani mkubwa, mabadiliko makubwa ya teknolojia au madeni ya kimataifa. Sasa unaweza kuamua kuingia kwenye mkataba mkubwa (wet-lease) au mdogo (dry-lease) kwa muda mfupi ili uweze kupima kama unaweza kupata faida au hasara; ukiona umepata faida basi ndipo unaweza kuingia mkataba wa muda mrefu au kununua kabisa.
Kibaya zaidi ni kwamba sisi, Tanzania tuna madeni mengi ya kimataifa jambo ambalo lilipelekea kutokuwa na safari nyingi za kimataifa kama ilivyotegemewa. Ndege ikienda nje wadai wetu wanaweza kwenda mahakamani na kuzikamata kama walivyofanya kipindi kile CANADA na AFRIKA KUSINI, jambo ambalo lilipelekea sisi kupoteza mabilioni ya pesa bila sababu za msingi. Tungekuwa kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease) wasingeweza kukamata zile ndege hata kama zingekuwa zinatumiwa na ATCL kwasababu siyo za Tanzania.
Lakini njia nyingine rahisi kama tumenunua ndege kwa pesa taslimu ni kuhakikisha tunasajili kampuni la ndege nje ya Tanzania, kwenye nchi rafiki kama Uchina halafu hilo shirika litaingia kwenye mkataba wa matumizi (Aircraft Lease) na ATCL ili ndege zionekane siyo za kwetu. AU tungeweza kutengeneza kampuni hapa nchini ambalo itaonyesha linamilikiwa na bodi ya wadhamini (Board of Trustees) wa Kanisa kubwa kama Roman Catholic au Lutheran au yote kwa pamoja kisha wao ndiyo wakanunua hizo ndege ikaonesha kwamba ni za kwao lakini kumbe hela ni za serikali.
Hivyo mwisho kabisa watu wanaotudai hawawezi kukamata mali ya makanisa makubwa na yenye ushawishi duniani kama hayo maana siyo mali ya serikali. Hivyo haya makanisa yataamua kwamba yaingie mkataba sasa wa matumizi ya ndege na ATCL. Lakini sisi tulidhani ni sifa kujisifia mbele ya wale wazungu kwamba tunanunua ndege kwa pesa taslimu ilhali wao hawatupendi kabisa, wanatupa misaada, tunakopa kwao na wanatudai, figisu lazima wakufanyie tu. Marekani, Uchina na Urusi wanatumia sana huu mchezo kwenye biashara mbalimbali ili kukwepa vikwazo vya kimataifa visivyo vya msingi.
Kubwa zaidi mashirika makubwa yaliyofanikiwa kwenye biashara za anga kama KLM, huwa yanakuwa yanashirikiana na mashirika ya nchi nyingine (In Partnership or Joint-Venture). Kwamba nchi moja itatoa wahandisi wa ndege (Auronatic Engineers), nyingine itatoa waendeshaji (Crew Members), nyingine italipia bima na nyingine itatoa eneo la uwekezaji (Area for investment). Mwaka 1922 Urusi ya Kisovieti (The Soviet Union) ilifanya hivi na Ujerumani (The Weimer Republic) na nakumbuka hata KLM imewahi kufanya hivi na Airfrance, (Japo sikumbuki ni mwaka gani na mkataba wao ulisemaje).....
Namalizia kwa kusema mitazamo ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya siasa, UJAMAA umedumaza fikra za watanzania. Ndiyo maana hata ukienda sehemu nyeti kama Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshini na Vyuo Vikuu unaweza kukutana na mtu mwenye fikra finyu hadi ukabaki mdomo wazi (They are crude, dimwitted and lackadaissical ): Shirika la ndege la Tanzania haimaniishi lazima liwe linamilikiwa na serikali ya Tanzania, raia wa Tanzania wakimiliki shirikia kubwa lenye faida ni sifa njema kwa nchi.
Ndiyo maana nchi kama Marekani biashara ya ndege hufanywa na watu binafsi chini ya uangalizi mkubwa wa serikali. Hata Ulaya nako mashirika mengi yanamilikiwa na watu binafsi kwa ushirikiano na serikali. Rais Paul Kagame, naye ashaanza kufanya hivi na waarabu kwenye Air-Rwanda, na siyo muda atawashinda na kufika mbali (The Man Knows the rules of the game).
Sasa ninyi endeleeeni kusikiliza The PolePolez, The Bashiruz an The Kabudiz na wengine wote wenye COLD-WAR NOSTALGIA ambao bado wanaishi karne ya ishirini halafu muone matokeo yake.Ukiataka kuamini nachokisema wewe angalia tu kwenye teuzi: Yaani TISS kwasababu wazijuazo wao wenyewe wakaamua kupeleka kada kutoka UVCCM akaongoze TPDC (One among critical Industries of the State).
Yaani hili linchi tumekuwa kama Pakistan (A Diabolical Mafia State), kila sehemu nyeti kuanzia mashirika ya umma yanaongozwa na mijasusi na wanajeshi, lanchi haliendi mbele, huku wenzake India wanapiga hatua kubwa kiuchumi. Nilikuwa nakasirika sana zamani, lakini baada ya kujua kwamba hii nchi iko kwenye AUTO-PILOT na kuko salama kwasababu ya NEEMA ZA MUNGU, nimeamua kufanya mambo yangu na familia yangu.
HII NCHI BADO TUNA SAFARI NDEFU SANA, HIVYO KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE.......
Prof Assad kasema mengi ya ukweli.
Lakini Dr Magufuli alikuwa na mboni Kali zaidi. Duniani kote, maendeleo ya vitu yaliambatana na kudorora kwa haki za binadamu. Hii sacrifice ndio ilikuwa lengo la Dr Magufuli.
Hugo Chavez wa Venezuela alitumia hii njia, lakini madhara aliyopata ni makubwa mno.
Waachiwe sekta binafsi km ilivyokuwa fast jetUkifuta ATCL airline ina maana yeye ataendeshaji sekta ya utalii. TOURISM ECONOMIC CHAIN anaijua.
Hii ni tweet inayoombatana na video huko twitter:
Prof. Assad anasema "..You can't buy airline by cash, hakuna yeyote anayenunua ndege kwa cash...wapi umeona?..hakuna mtu ananunua ndege kwa cash. Watu wajinga sana ndio wanaweza kufanya jambo hili..."
Somo:
Wenye mamlaka/madaraka, tumieni vizuri mamlaka mliokabidhiwa ili mnapotangulua mbele za haki, msiwaache ndugu na jamaa zenu na maumivu mara mbili: kufiwa na Marehemu kusemwa vibaya.
Unataka nikueleze zaidi kibiashara, Basi iko hivi: Biashara ya ndege inaendeshwa kwa gharama kubwa sana duniani kote. Lakini kitaalamu biashara ya ndege kama yenyewe haingizi faida ya moja kwa moja. Kinachofanyika ni kwamba usafirishaji wa anga kama miundombinu mingine, hutumika katika kufanikisha shughuli za kiuchumi ambazo zenyewe sasa ndizo huleta faida kwa nchi.Umeandija maelezo mengi sana,ila hujaonyesha gharama ya ku-lease na gharama ya kununua cash,yaani unataka kutuaminisha kwamba lessor hataweka profit kufidia yote hayo anayosema,acheni ujinga
Mkuu usipende kuongea vitu vya ukweli maana humu tuna ma mizimu hatari hata uyaelekeze vipi hayaamini na hayakubali kama mazombi tuHii report ingetolewa kabla mwendazake hajazikwa tusinge lia na kuzunguka naye vile na tungezika haraka haraka. Warudishe machozi yetu
Kumbe na wewe una karoho ka kishetani hivi!Ndio nafurahia coz damage aliyoifanya sio ya dunia hii..ni kama mwizi kuchomwa moto,wewe utahuzunuka?
Sasa bwana barafuyamoto huwa nakuonaga mtu mwenye busara kuliko hao wenzako kumbe na wewe ni walewale tu. Hebu nisaidie labda wewe mwerevu kulimo Prof Assad, hayo mashirika yanayonunua ndege kwa pesa taslimu yanamilikiwa na serikali au mashirika binafsi ???Prof. Atalisha matango wengi sana ila wengine tulishaga kataa kulishwa ujinga. Atawapata vilaza tu. cheki link hii chini alafu eti prof anakuja na matapishi akiaminibyeye ndio source ya taarifa sahihi..
Naweza kuwa nina roho nzuri kushinda wewe unayesema nina roho ya kishetani..sipendi uonevu mimi.
Kwahiyo kusimanga marehemu ni roho nzuri?Naweza kuwa nina roho nzuri kushinda wewe unayesema nina roho ya kishetani..sipendi uonevu mimi.