Prof. Florens Luoga: Crypto-currencies are not safe as far as we know

Nimecheka nilivyona kwamba sio kila anae fanya biashara anataka Faida [emoji23][emoji23][emoji23]
Hujaelewa, watu wanavamia fx wakihisi wanaenda tu piga faida kitu ambacho siyo kweli ndiyo maana walianza wengi waliobaki wachache.
Nimekwambia bitcoin mimi nazinunua na kuziuza kwasababu mbili, moja nazihold kuziuza zikipanda value niuze, hii inanipa faida, jambo la pili nanunua na kuuza kama means ya ku exchange pesa kuwa fiat money. Mfano kuna kipindi nlikuwa natumia ela ya skrill au paypal kununua bitcoin halafu namuuzia mtu ambaye analipa kwa mpesa. Njia hii lazima nile hasara maana hapa lengo kubadilisha fedha tu na ntanunua ghali na kuuza low kwakuwa sitaki kuishikilia nachotaka ni mtu anitumie pesa tu
Tatizo lingine ni kwamba kwasasa cryptos ni more like commodities not currencies.
Ila siku zinavyoenda itakaa sawa ni kitu kisichoepukika
 
Rafiki hakuna mtu anafanya biashara akijua anapata hasara na biashara nzuri ni Ile ya muda mfupi na kuleta faida (Forex ni biashara nzuri ukiwa na mtaji mkubwa) hii ya kwenu sio ambayo inajulikana kwasababu wote waliofanya wamepata hasara!!!..Tunawajua sio story
 
Mimi nje ya bitcoin sijawahi trade fx because from the start nilijua it is not for me.
Nimeingia bitcoin nmechelewa sana lakini kwa cryptos nnazohold nikiuza nakula faida.
Biashara yoyote mtu akiingia bila taarifa akaifanya ndivyo sivyo lazima ale hasara hata iwe ni ya kuuza mchele.
 
And by the serikali inaweza tengeneza cryptocurrency iliyo backed by fiat money au hata gold.
Shida yangu ni kwamba kwasasa bitcoin ni more than a commodity na siyo currency hiyo ndiyo shida.
Yani watu wananunua butcoin si kwa ajili ya kuifanhia transaction ila kuihold ipande thamani wauze
 
Kwahiyo sio biashara hii
 
Kwahiyo sio biashara hii
Mkuu huenda mimi na wewe tunabisha jambo ambalo hatuelewi tunabishana nini.
Labda niseme hivi, mimi ninalosema ni kwamba future ya pesa ni cryptocurrencies. Huo ndo mtazamo wangu.
Kwasasa cryptos ni kama biashara za commodities tu ila serikali zitakapoziadopt basi zitageuka kuwa ndo pesa.
Watu tunaohold cryptos kwa sasa tunazihold zipande bei tuuze wala hatuzihold kwa ajili ya kununulia vtu. Ni wachache wanaofanya hivyo.
Tena na ujio wa metaverse ndiyo kabisa cryptos zitakuwa pesa ya future.
 
Hayo ni mawazo yako ila point ya msingi ni kwamba hapa duniani kuna nchi inatumia bitcoin kama legal tender yao. Na hilo umekubali.
 
Kwani kwa nchi kama Tz rais hamiliki TZS? yani rais hamiliki hata jero kweli?

Sasa kama rais wa Tz anamiliki TZS kwanini iwe kosa rais wa el savador?
 
Nimebakia najiuliza, so wewe ndio size ya kila mtu humu?! Kwenye mjadala wa hoja jikite kwenye hoja na sio kushambuliana. Kwani ni wapi mie nmesema nimekuzidi chochote kipato, akili au hekima??!

Haya tukirudi kwenye hoja, mfano bonds ndio safest investment lakini return yake huwa ndogo(2% -7% kwa makampuni mengi), then hisa zinafuatia japo ni riskier ukilinganisha na bonds ila zinakuwa na returns kubwa kidogo (8%-15%) then tuziweke na crypto hapo mwisho, ni the most riskiest investment (ni sawa na kununua penny stocks kwa baadhi ya coins) lakini ndio zenye most return (Yaani kupata 100%+ ni jambo la kawaida sana). Kauli ya Gavana wa BOT ipo sahihi kwa mlengo huu, kwamba cryptos investment ni speculation. Yaani unaingia ila sio investments salama kama hizi zingine ila sio kwamba watu hawawezi kupata pesa au faida yenye maana. Tumia dictionary kuelewa maana ya neno "speculation" ila kwa ufupi najua kuwa ni "not certain" huwezi uza kila ulichonacho ukanunua cryptos ukaonekana ni mtu mwenye akili timamu (sababu tu ni speculation hio unafanya na kweli Gavana yupo sahihi, lakini kwa kunikejeli na kunishambulia haukuwa sahihi hata kidogo.

Na tukirudi kwenye ukweli wa pili, hii ni biashara ya watu wenye UKWASI. Kwenye hili kwa kipato cha ngama huwezi fanya crypto investment yenye maana. Utategemea sana on kubahatisha sababu most stable coins walau zina price ya $200 on average. Sasa kwa kipato gani na kwa biashara gani hapa Tanzania unaweza cheza michezo hii. Lazima uwe na kahela cha kuchezea walau $200 kila mwezi kwa lengo la kununua small chunks kila price dip inapotokea, hivyo Gavana kuonya ypo sahihi watu wasije kujiua aftermaths. Yangu ni hayo tu.
 
"As far as we know Crypto-currencies are not safe. We cannot give timelines when to issue regulations, we are still researching – we will give regulations when we have finished our research" - Prof. Florens Luoga, Governor, Bank of Tanzania.

Ni sawa na kuambiwa parking at owner's risk.
 
Twende kwenye hoja wakati umeshatoka kwenye hoja!!..fedha za kudownload hakuna Ndugu!!!
 
Kwani kwa nchi kama Tz rais hamiliki TZS? yani rais hamiliki hata jero kweli?

Sasa kama rais wa Tz anamiliki TZS kwanini iwe kosa rais wa el savador?
Ni kosa sana rais kuhamasisha kamari na yeye akiwa mshiriki. Au wewe unadhani jero ya TZS anayomiliki raisi ana-speculate akisikilizia ipande thamani aiuze?
 
Ni kosa sana rais kuhamasisha kamari na yeye akiwa mshiriki. Au wewe unadhani jero ya TZS anayomiliki raisi ana-speculate akisikilizia ipande thamani aiuze?
Ni nani wamesema wana speculate? El savador wana speculate ki vipi? El savador hawa speculate bali wanatumia bitcoin kama shilingi yao ya kufanyia malipo ya kila siku!
 
Uliniuliza swali kuhusu rais wa TZ kumiliki TZS
Kwani kwa nchi kama Tz rais hamiliki TZS? yani rais hamiliki hata jero kweli?

Sasa kama rais wa Tz anamiliki TZS kwanini iwe kosa rais wa el savador?
Halafu unauliza tena swali lingine na mada nyingine
Ni nani wamesema wana speculate? El savador wana speculate ki vipi? El savador hawa speculate bali wanatumia bitcoin kama shilingi yao ya kufanyia malipo ya kila siku!
Na kwa msingi wa swali hili inaonyesha hiyo El Salvador yenyewe hufaitilii kiundani.
Pamoja na BTC kugeuzwa legal tender, el salvador kwa sasa wanaspeculate vile vile, Serikali ya El Salvador wana account ya bitcoin wanaiita Bitcoin Trust Account (FIDEBITCOIN) ambayo mpaka sasa ina bitcoin 1,120. Ambapo serikali ilisema mwezi wa 11 ilitengeneza faida hivyo faida waliyopata baada ya uwekezaji kwenye speculation kupitia FIDEBITCOIN account itapelekwa kutengeneza shule 20.

Sasa wewe unasemaje kuwa hawaspeculate.
 
Kabisa! Muda ni mwalimu tosha, wacha tusiongee sana kiongozi maana wanaeza tuita SCAMS aise.
Kwamtazamo wangu naona mabenk ndio Scam juzi nilitumiwa laki mbili wakata elfu 20 nikatoa 180,000 elfu 20 ikagoma kutoka lakini kwenye wallet ya BTC fees ni kidogo sana nadhani BOT wanalinda mabenk yanayotumiza ukweli sarafu ni habari ya mjini naikubali nimeitumia muda mrefu sana ndomana kunaupotoshi mwingi
 
Wewe unajifananisha na Luoga kweli [emoji24][emoji24] hapo ndio mnapo onekana matapeli!!..Unajua BOT kuna wataalamu wangapi?!!.. Unadhani hizo benki binafsi ziko chini ya Nani?!!.
Wataalamu kuwa wengi sio tija wanaisaidia nini akina Lipumba mbona uchumi uko hoi?
 
Imeisha hiyo.
 
All Paper Money eventually returns to its intrinsic value; Zero ..., ila U-Scam wa Banks haufanyi Pesa zao kutokuendelea kuwa Legal Tender (its backed by the Powerful) wala haimaanishi kwamba Bitcoin ndio yenyewe (Liquidity yake itaendelea kuwa kikwazo)

All in all ingawa tutaondoka kwenye currency as we know it na kuhamia kwenye digital currency backed by Block Chain..., lakini hio itakuwa centralized na sio uncentralized kama bitcoin..., that's my humble opinion; na kila mtu afanye investment huko kwa utashi wake na sio jukumu la BOT kuhamasisha watu kwenye kitu ambacho huenda wakaungua hapo kesho (it needs to be proven beyond reasonable doubts)...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…