Prof Jay: Ferooz akiwa wa moto sana alikuwa hagusiki yaani uvimbaji kama wote

Prof Jay: Ferooz akiwa wa moto sana alikuwa hagusiki yaani uvimbaji kama wote

2003 huyo mtoto Feruz (miaka ile kuonana uso kwa macho na msanii hata wale wa mchiriku ilikuwa bonge moja la sifa) akiwa na Jeep yake dark blue akaja dukani kwa bro wangu Ilala wezi walikuwa wamempiga side mirror yake so akawa anatafuta.

Tulikuwa tumekaa nje kwenye bench kama watu saba hivi alipofika aka-park gari mbele yetu akashusha kioo nusu bila hata salamu akamtaka mwenye duka hakuna aliyemjibu na tulikuwa tunamkubali sana akamshusha mpambe wake mmoja akaulize moja kwa moja pale dukani bro akamrusha mshkaji amwambie “hatuuzi” ila alikuwa na akili mwisho akajua kosa lake akajirudi.

Siku zote hela zinapokuwa nyingi hasa kwa vijana wakikosa management nzuri hushindwa kuzi-control mwisho ndo kama hivi
 
Mziki tatizo ni kuchuja
Sasa leo hii nice aje aimbe
Kuku kapanda baiskeli
Watu watamuelewa kweli

Sasa leo hii nice mtu wa kunywa bia bar na kugoma kulipa au kukimbia bill

Ova
Kwa ishu ya mziki kweli kabisa
 
Hii hali huwakuta wengi walio kwenye huo mfumo wa kupata pesa kwa mkupuo...hii ipo hata huko mbele, wanazuzuka sema wengi wanaokolewa na management kama zipo imara.

Nilimsikia Jack Chan kwenye interview anasema alilipwa pesa nyingi kwenye movie akachanganyikiwa akawa ananunua kila kitu hovyo..anasema akikumbuka huo wakati anajiona mjinga wa mwisho.

Sema tu pesa ikawa inaendelea kuingia mpaka ikamkuta anakomaa akili.
 
Ilikua kama miaka kadhaa nyuma aliazima akafanyie video. Ni kipindi hiki alichokua ameshapotea. Kuna video fulani alifanya na mdada kama ya mnanda sijui ndo chiriku. Kenge maji. Alikua anaringa sana. Tulimkata mitama
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna siku Mr nice alikuja masai club akanunua stick ya pool table kwa mwana anayecheza na akawa anamlipa kila anayemfunga ili aendelee kucheza
Umenikumbusha kitambo Masai Club Kino kule au sivyo?
Mshikaji wetu alikuwa na pesa mingi sana ya madini tukaenda itumia hicho kiwanja akaanza ushamba wake wa Kisukuma anafungua bia kwa chupa kizibo kinaruka karibu atoboe watu macho.
Mbavu wakaja mtoa nje anagoma ilikuwa vurugu ila mwenyeji wetu mangi flani mpole mtoto wa mjini mwenye pub nyingi kali akawasihi mbavu na meneja wakamuacha jamaa aendelee kula starehe.
Hiyo wayback awamu ya kwanza au ya mwisho ya JK.
 
Kuna siku Mr nice alikuja masai club akanunua stick ya pool table kwa mwana anayecheza na akawa anamlipa kila anayemfunga ili aendelee kucheza
Na alikuwa anawabadilisha akina Halima kama kyupi
 
Back
Top Bottom