LGE2024 Prof. Jay: Wagombea wetu wote Wilaya ya Kilosa wameenguliwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Tatizo ni CCM
 
Yaaan

Huyu joseph haule tumemhudumia pale hospital nusu afe mama katoa mamilion ya fedha ya kumtibia lakini leo anasema tusije laumiana anatishiana na serikali aisee
Mkuu hapo unataka kusema mama Samia ndiyo anatishiwa kwasababu ameenguq wagombea wote? Au unamaanisha kuwa mama Samia ndiyo anahusika kuengua majina? Na kama anahusika unaona siyo busara kupewa vitisho?
 
Nilivyoona kapiga chini kinana na kuwarudisha wahuni kwenye system nikajua shuguli imeisha hapa.
 
We're still on process✊🏿
 
Hii ni kazi rahisi kama ofisi ya kijiji ipo mtaani kwetu halafu ambaye hajachaguliwa anakuja kuikalia na sisi tunamuangalia wenye makosa ni wananchi. Lazima ofisi ya kijiji iwe chini ya mtu mliye mchaguwa wenyewe kinyume na hapo fanyeni kama mmkuta mwizi ndani ya nyumba yako.
 
Ccm wanazungumza na watanzania kwa lugha nyepesi sana na mnajidai hamiluelewi..wanachosema..." Hamtawatoa madarakani kwa njia ya kura"..period!
Means mfikirie alternative way ya kudeal nao,otherws next yr haya haya yanaenda tokea.
 
Tuliwaambia Futeni uchaguzi hamsikii
Mlisema watake wasitake haya sasa kimewaramba.

Futeni uchaguzi msipoteze muda wa wananchi.

Eti watalinda kura, watakomaaa, ni kuwapotezea tu wanainchi mda wao
 
Hivi kwanini Watanzania tumeamua kujitoa ufahamu kwa kiwango hiki!? Fikiria msimamizi wa uchaguzi anaengua majina YOTE ya wagombea wa CHADEMA Wilaya nzima! Kwa namna yoyote ile hili linaweza kueleweka au kukubalika katika JAMII ya KITANZANIA!?

Huku kujitoa ufahamu kwa kiwango hiki na kujifanya Mazombi kunalisaidia nini Taifa!? Walianza na kukimbia Ofisi za umma kujificha ili wagombea wa vyama vya upinzani wasipate kuchukua au kurudisha fomu. Walio bahatika kupata fomu na kuzirejesha ,majina yao wameeng'uliwa! Kama hatukua tayari kufanya uchaguzi ilikua ni bora tukaacha kupoteza pesa ,kupoteza muda watu kujiandikisha,na kuwapotezea muda watu kuchukua fomu.

Hii Tanzania ni ya wote , huu ubaguzi katika uongozi ulio anzishwa na Hayati Magufuli haukubaliki.

Hayati alikua akituhumiwa hata akiwa bado Mbunge kwa tuhuma za kuwateka wapinzani wake katika Ubunge na mbinu chafu wakati wa uchaguzi.Sasa tumerithi umekua ndio mfumo wa Taifa was uchaguzi, kubaguana kwa vyama! Haikubaliki duniani na mbinguni, haikubaliki!
 
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 0
Mkuu safari ni ndefu mno
 
Hakika sintaacha kumlaani Magufuli muasisi wa huu upumbavu. Chura kiziwi ajitazame sana haki za watu huwezi kuzichezea Mungu akakuacha salama.
Tuendelee kumuomba Mungu mpaka aamue huu ugomvi dhidi ya Haki
Si mlishangilia kwamba dhalimu kafa sasa mnapumua huku mama yenu akipiga mwingi?

Vilio vya nini sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…