Prof. Kabudi abananishwa kuhusu kufutwa kwa Jina Magufuli City pale Dodoma

Prof. Kabudi abananishwa kuhusu kufutwa kwa Jina Magufuli City pale Dodoma

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Muandishi ashangazwa kuhusu matumizi ya neno Mji wa serikali ambapo mara nyingi ulikuwa ukifahamika kama Magufuli City, lakini jina hilo limekuwa nadra sana kutamkwa.

Baada ya hotuba ya Waziri Mhe. Kabudi, mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Mji wa Serikali, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, mwandishi wa habari Awadhi Omary kutoka KANIKI TV ameibua hoja kuhusu jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Awadhi Omary alihoji sababu za hotuba hiyo kutotaja jina la Hayati Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihusishwa na uanzishwaji na ujenzi wa Mji wa Serikali, huku akieleza kuwa jina la Magufuli City au Mji wa Magufuli limekuwa likitumika katika mazoea ya wengi wanapoutaja mji huo.

Swali hilo limeibua hoja kuhusu utambuzi wa mchango wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati wa Serikali.

Ule mji wa serikali utaitwaje jina la mtu?
Kwani ile stendi ya Serikali pale mboni inaitwa jina la mtu? Au huijui stendi ya Magufuli kuna ubaya gani eneo la makazi ya viongozi likiitwa jina la alieanzisha ujenzi wa hilo eneo husika mfano Kijazi flyover interchange aliyejenga si unamjua na ile pale Mfugale flyover interchange aliyejenga si unamjua kapewa jina lake kwanini haujahoji hii flyover ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu, kuna shule inaitwa Samia Sekondari School kule Tabora vipi ushawahi kusema hii shule ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu, hospital JKCI au niseme The Jakaya Kikwete Cardiac Institute hio ni hospital ya serikali kwanini hukuwahi kusema hii kwanini inaitwa jina la mtu? Kuna shule inaitwa Yusuphu Makamba kwanini hujasema hii shule ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu? Kuna shule ya sekondari ya serikali mpaka mabweni ya wanafunzi yanaitwa Salima Kikwete kwanini hujawahi kuhoji haya majengo ya serikali kwanini yapewe jina la mtu? Are you people insane? What's the fucks is this?
 
Umemwaga povu bure.

Mbona jamaa kauliza swali la msingi kwa upana, na hajamaanisha kuulizia jina la JPM pekee.

Naungana na jamaa, ni upuuzi kuipa miradi ya umma maana haina tija wala maana yoyote. Kuna ufahari gani kila sehemu au kitu kinaitwa jina la mtu mmoja au inasaidia nini Taifa?
 
Muandishi ashangazwa kuhusu matumizi ya neno Mji wa serikali ambapo mara nyingi ulikuwa ukifahamika kama Magufuli City, lakini jina hilo limekuwa nadra sana kutamkwa.

Baada ya hotuba ya Waziri Mhe. Kabudi, mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Mji wa Serikali, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, mwandishi wa habari Awadhi Omary kutoka KANIKI TV ameibua hoja kuhusu jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Awadhi Omary alihoji sababu za hotuba hiyo kutotaja jina la Hayati Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihusishwa na uanzishwaji na ujenzi wa Mji wa Serikali, huku akieleza kuwa jina la Magufuli City au Mji wa Magufuli limekuwa likitumika katika mazoea ya wengi wanapoutaja mji huo.

Swali hilo limeibua hoja kuhusu utambuzi wa mchango wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati wa Serikali.

View attachment 3699878
Mbona mnalilia vitu vidogo sana na kuacha mambo makubwa na muhimu. Sasa hilo jina litakusaidia nini?
 
Katika vitu ambavyo vinanishangaza hasa Afrika ni kuvipa majina ya watu vitu au maeneo yetu ambayo ni ya kitaifa

Ni sawa kutoa baadhi ya vitu vichache na kuwapa baadhi tu ya watu waliofanya mambo makubwa sana kwa taifa

Lakini kila kitu kukipa majina ya watu na wengine bado wapo hai huku hatujajua hatima yao hapa duniani kama itakua ya heshima au ya aibu sio sawa, na ni kuwadhulumu vizazi vijavyo ambao nao watakuja kutoa mchango wao kwa taifa

Sasa hivi tuna shule tena za umma zinaitwa Ali Hapi, Paul Makonda nk ambao wapo hai na wanashikilia madaraka ya kisiasa na hatujui mwisho wao utakuaje.

kuna shule zingine zinaitwa Daniel Yona, Basil Mramba(hawa waliwahi kuhukumiwa kifungo gerezani kwa matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni). Inamaana walikuja kuharibu baadae na sio fahari tena kwa umma wa Watanzania

Kwani tukiishia kusema Bwawa la Umeme la Rufiji, daraja la interchange la Ubungo, Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam nini kitaharibika? Mbona tuna ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, Ziwa Nyanza(Waingereza walimpa Malkia Victoria), Ziwa Natron, ziwa Manyara nk?

Kizazi hiki ndio kingekua kina mamlaka miaka ya nyuma basi hata mbuga na hifadhi zetu kama Manyara, Mikumi, Ngorongoro, Serengeti au mito na maziwa makubwa vingepewa majina ya watu

Kumkumbuka mtu sio lazima ukipe jina lake kitu tena cha umma. Sio vibaya kuvipa majina vitu vichache kama ilivyokua kwa Mwalimu Nyerere, Mkapa au Mwinyi(maana kwanza washatangulia mbele ya haki) lakini si sawa kila mradi wa umma au kila kitu cha kitaifa lazima tutafute jina la mtu

Hata miaka ya awamu ya kwanza lilikuwepo hili lakini ilikua ni kwa watu wachache waliofanya mambo makubwa kwa taifa kama kina Shaaban Roberts, Lawi Nangwanda Sijaona, Sheikh Amri Abeid Kaluta nk na tena wanyewe wakiwa washatangulia mbele ya haki

Mwalimu alikua hapendi vitu vipewe jina lake na yeye aliidhinisha watu wachache sana na vitu vichache sana ndio vipewe majina ya watu tena baada ya wao kua wamesha fariki.

Mfano wakati Nyerere akiwa bado na maelewano mazuri na Oscar Kambona halafu akaridhia baadhi ya vitu vipewe jina lake ingekuaje alipokuja "kuharibu" na kukimbia nchi? Mwalimu angefuta jina la Kambona?

Tuyaache majina ya miji, majiji, vijiji na vitongoji vyetu yashamiri kwa miradi mikubwa kupewa majina yalipo ili tuitangaze zaidi nchi kuliko personalities
 
Umemwaga povu bure.

Mbona jamaa kauliza swali la msingi kwa upana, na hajamaanisha kuulizia jina la JPM pekee.

Naungana na jamaa, ni upuuzi kuipa miradi ya umma maana haina tija wala maana yoyote. Kuna ufahari gani kila sehemu au kitu kinaitwa jina la mtu mmoja au inasaidia nini Taifa?
Nimesema kwanini hakuhoji kabla nipe uzi wake wa zamani akiwa anahoji hilo jambo au mpaka jamaa waje waulize kwamba kwanini huu mji ulikua na jina hili nyinyi mnataka kufanya janja janja mlifute muweke majina yenu, hivi sijui tunaelewana wewe Samia Scholarship?
 
Katika vitu ambavyo vinanishangaza hasa Afrika ni kuvipa majina ya watu vitu au maeneo yetu ambayo ni ya kitaifa
Mjinga wewe, Benjamin Franklin yupo kwenye pesa ya Marekani for Years, mamako nani? Afrika hivi afrika vile ujinga umewajaa vichwani kila kitu afrika kenge wadogo nyinyi
 
Hata January Makamba alisoma hotuba nzima ya bwawa la mwl nyerere bila kumtaja Magufuli popote lakini aliishia kuzomewa na watanzania.
Hata wakifuta watanzania wanajua aliyehamishia serikali Dodoma ni Magufuli.
 
Back
Top Bottom