Prof. Kabudi abananishwa kuhusu kufutwa kwa Jina Magufuli City pale Dodoma

Prof. Kabudi abananishwa kuhusu kufutwa kwa Jina Magufuli City pale Dodoma

Mjinga wewe, Benjamin Franklin yupo kwenye pesa ya Marekani for Years, mamako nani? Afrika hivi afrika vile ujinga umewajaa vichwani kila kitu afrika kenge wadogo nyinyi
MIongoni yanayonishangaza pia ni hili la kizazi hiki cha sasa. Kila unapotofautiana na mtu kwa hoja ni lazima akutukane na kutweza utu wako hata kama hajui umri wako. Pengine labda hiyo ndio njia mpya ya kushinda mjadala!

Ungeweza kusema hoja yako bila kulazimika kuandika maneno ya ziada ya kunikashifu ndugu yangu. Mimi sikurudishii chochote sababu sio malezi yangu na nimekusamehe

Nakubaliana na hoja yako kua kuna baadhi ya vitu vichache hata kwa wenzetu hupewa majina ya watu kama ilivyo Marekani walivyofanya kwa kina George Washington, JF Kenedy na Benjamin Franklin.

Lakini angalia kwa mfano kazi alizofanya Frnklin kwa taifa la Marekani, ni very outstanding na alikua Founding Father wa USA. Hata hivyo picha yake iliwekwa kwe pesa miaka baada ya yeye kufa

Sio sisi huku Afrika na hasa Tanzania every Dick, Tom and Jerry tunawapa majina ya vitu vya umma bila ridhaa ya wananchi na tena wengine wakiwa bado wapo hai na baadhi yao wanakuja kua wahalifu. Tunakua na fahari gani kwa hilo?
 
Mimi sipendi hilo jina la mtumba, kwanini serikali wasibadili hili jina? Mtumba si kudhalilishana huko?
 
Hata January Makamba alisoma hotuba nzima ya bwawa la mwl nyerere bila kumtaja Magufuli popote lakini aliishia kuzomewa na watanzania.
Hata wakifuta watanzania wanajua aliyehamishia serikali Dodoma ni Magufuli.
Na ulikuwa ni uamuzi mubaya huo wa kwenda kujenga ikulu nyingine huko mbali enzi hizi za WhatsApp
 
Kwani ile stendi ya Serikali pale mboni inaitwa jina la mtu? Au huijui stendi ya Magufuli kuna ubaya gani eneo la makazi ya viongozi likiitwa jina la alieanzisha ujenzi wa hilo eneo husika mfano Kijazi flyover interchange aliyejenga si unamjua na ile pale Mfugale flyover interchange aliyejenga si unamjua kapewa jina lake kwanini haujahoji hii flyover ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu, kuna shule inaitwa Samia Sekondari School kule Tabora vipi ushawahi kusema hii shule ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu, hospital JKCI au niseme The Jakaya Kikwete Cardiac Institute hio ni hospital ya serikali kwanini hukuwahi kusema hii kwanini inaitwa jina la mtu? Kuna shule inaitwa Yusuphu Makamba kwanini hujasema hii shule ya serikali kwanini inaitwa jina la mtu? Kuna shule ya sekondari ya serikali mpaka mabweni ya wanafunzi yanaitwa Salima Kikwete kwanini hujawahi kuhoji haya majengo ya serikali kwanini yapewe jina la mtu? Are you people insane? What's the fucks is this?
Hakuna shida kaka, ila Dodoma isiitwe mji wa mama sa100 mana naona machawa wanatabika kubadili, hakuna lolote alilofanya kwenye hili
 
Ndiyo mambo ya serikali yalivyo ndugu yangu..
Wakati mwingine ni vigumu kuyaelewa.
Ila nikipewa kuchagua kati ya Mtumba na Magufuli City, nitachagua Magufuli City.
Hata ikulu badala ya kuitwa Ikulu ya Chamwino, ingeitwa Magufuli State House.
Ni ushauri tu kutoka kwa raia wa chini kabisa asiye na sauti.
 
Nimesema kwanini hakuhoji kabla nipe uzi wake wa zamani akiwa anahoji hilo jambo au mpaka jamaa waje waulize kwamba kwanini huu mji ulikua na jina hili nyinyi mnataka kufanya janja janja mlifute muweke majina yenu, hivi sijui tunaelewana wewe Samia Scholarship?
Ukiwa una akili ya hivi, huwezi kuelewa umuhimu wa jamaa alichouliza wala kujibu umuhimu wa hayo majina.
 
Mbona mnalilia vitu vidogo sana na kuacha mambo makubwa na muhimu. Sasa hilo jina litakusaidia nini?
Wewe umejawa na chuki... kwani majina yameanza kuitwa leo.... mpaka vyuo vikuu vinapewa majina ya watu

Ni kama hamasa kwa vizazi
 
Hata January Makamba alisoma hotuba nzima ya bwawa la mwl nyerere bila kumtaja Magufuli popote lakini aliishia kuzomewa na watanzania.
Hata wakifuta watanzania wanajua aliyehamishia serikali Dodoma ni Magufuli.
Kweli.... na ukweli usemwe

Watu wanaleta janja janja
 
Muandishi ashangazwa kuhusu matumizi ya neno Mji wa serikali ambapo mara nyingi ulikuwa ukifahamika kama Magufuli City, lakini jina hilo limekuwa nadra sana kutamkwa.

Baada ya hotuba ya Waziri Mhe. Kabudi, mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Mji wa Serikali, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, mwandishi wa habari Awadhi Omary kutoka KANIKI TV ameibua hoja kuhusu jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Awadhi Omary alihoji sababu za hotuba hiyo kutotaja jina la Hayati Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihusishwa na uanzishwaji na ujenzi wa Mji wa Serikali, huku akieleza kuwa jina la Magufuli City au Mji wa Magufuli limekuwa likitumika katika mazoea ya wengi wanapoutaja mji huo.

Swali hilo limeibua hoja kuhusu utambuzi wa mchango wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati wa Serikali.

View attachment 3699878
Kwani huo mji umeanzishwa bila sheria, bila formal name?

What is the legal formal name of that place?
 
MIongoni yanayonishangaza pia ni hili la kizazi hiki cha sasa. Kila unapotofautiana na mtu kwa hoja ni lazima akutukane na kutweza utu wako hata kama hajui umri wako. Pengine labda hiyo ndio njia mpya ya kushinda mjadala!

Ungeweza kusema hoja yako bila kulazimika kuandika maneno ya ziada ya kunikashifu ndugu yangu. Mimi sikurudishii chochote sababu sio malezi yangu na nimekusamehe

Nakubaliana na hoja yako kua kuna baadhi ya vitu vichache hata kwa wenzetu hupewa majina ya watu kama ilivyo Marekani walivyofanya kwa kina George Washington, JF Kenedy na Benjamin Franklin.

Lakini angalia kwa mfano kazi alizofanya Frnklin kwa taifa la Marekani, ni very outstanding na alikua Founding Father wa USA. Hata hivyo picha yake iliwekwa kwe pesa miaka baada ya yeye kufa

Sio sisi huku Afrika na hasa Tanzania every Dick, Tom and Jerry tunawapa majina ya vitu vya umma bila ridhaa ya wananchi na tena wengine wakiwa bado wapo hai na baadhi yao wanakuja kua wahalifu. Tunakua na fahari gani kwa hilo?
Vitu alivyofanya magufuli, ilibidi hata Nchi isiitwe Tanzania, ilitakiwa iitwe Magufuli Nation


Yule Mwamba wa Chato kapiga miradi mikubwa ndani ya miaka 5 tu... ambayo hakuna raisi amewai kufanya...
 
Lilikuwa Pori tu, haukuwa mji
Lilikuwa pori, haukuwa mji.

Lakini mji umeanzishwa kiholela tu? Hakuna sheria iliyopitishwa? Haujaandikishwa rasmi?

Umeandikishwaje rasmi kisheria?

Maana mara tunasikia "Mji wa Serikali Mtumba" mara "Magufuli City", huu ni mji mmoja?

Na kama ni mji mmoja, jina lake rasmi ni lipi?

Tujue kama kuna firmal name na nickname.

Maana mtu anaweza kuitwa Juma "Bonge" Msafiri.

Wengine wakajua Bonge ni jina lake rasmi mpaka jina lake rasmi Juma Msagiri lisijulikane.

Kumbe Bonge ni nickname, jina lake rasmi ni Juma Msafiri.

Sasa kwenye huu mji, kuna jina rasmi na nickname?

Kama ni hivyo, jina rasmi ni lipi na nickname ni ipi?
 
Naheshimu msimamo wako.

Nina reserve my comment/opinion
Hivi unajua Timeline ya Miaka 5 tu...

Kafanya projects ambazo marais wengine wamechukua Decade kuikamilisha au kuifanya nusu....

Alafu akafariki... huyo jamaa angekaa miaka 10 je, si ingekuwa balaa
 
Lilikuwa pori, haukuwa mji.

Lamini mji uneanzishwa kiholela tu? Hakuna sheria iliyopitishwa? Haujaandikishwa rasmi?

Umeandikishwaje rasmi kisheria?

Maana mara tunasikia "Mji wa Serikali Mtumba" mara "Magufuli City", huu ni mji mmoja?

Na kama ni mji mmoja, jina lake rasmi ni lipi?

Tujue kama kuna firmal name na nickname.

Maana mtu anaweza kuitwa Juma "Bonge" Msafiri.

Wengine wakajua Bonge ni jina lake rasmi mpaka jina lake rasmi Juma Msagiri lisijulikane.

Kumbe Bonge ni nickname, jina lake rasmi ni Juma Msafiri.

Sasa kwenye huu mji, kuna jina rasmi na nickname?

Kama ni hivyo, jina rasmi ni lipi na nickname ni ipi?
Maeneo mengi ya yanayoshikikiwa na serikali kwa miradi ya hapo badae bado ni mapori...

Mfano pori la pale sekenke, kwa hiyo wakijenga Ikulu iitwe Sekenke kwa sababu sekenke ilikuwepo kitambo

Hata mitaa ilikuwa na majina hapo awali kabla bado ikiwa mapori, lakini baada ya mtu fulani kujenga na kuwa maarufu hapo mtaa unapewa jina lake

Hata ikulu uitwa jina kwa mujibu wa kitu au mtu au jambo fulani lililopelekea hapo pakawa hivyo.... Mkapa Stadium ulipewa jina la Mkapa kuenzi jitihada zake
 
Vitu alivyofanya magufuli, ilibidi hata Nchi isiitwe Tanzania, ilitakiwa iitwe Magufuli Nation


Yule Mwamba wa Chato kapiga miradi mikubwa ndani ya miaka 5 tu... ambayo hakuna raisi amewai kufanya...
Watanzania wengi kama wewe mna akili ndogo sana, ndiyo maana nchi inashindwa kuendelea.

Wewe una poverty anxiety unaona umuhimu wa rais ni wingi wa miradi mikubwa.

Hiyo miradi yenyewe ukiambiwa utoe hesabu zake hapa huwezi, kwa sababu Magufuli aliminya uhuru mpaka watu wakashindwa kufanya mikutano ya hadhara.

Miradi ya kijinga ya kununua ndege bila uwazi, bila audits, straight from Ikulu, kwa cash, bila business plan.

Wananchi mnashangilia kuibiwa!

Lazima muendelee kuwa masikini.
 
Watanzania wengi kama wewe mna akili ndogo sana, ndiyo maana nchi inashindwa kuendelea.

Wewe una poverty anxiety unaona umuhimu wa rais ni wingi wa miradi mikubwa.

Hiyo miradi yenyewe ukiambiwa utoe hesabu zake hapa huwezi, kwa sababu Magufuli aliminya uhuru mpaka watu wakashindwa kufanya mikutano ya hadhara.

Miradi ya kijinga ya kununua ndege bila uwazi, bila audits, straight frim Ikulu, kwa cash, bika business plan.

Wananchi mnashangilia kuibiwa!

Lazima muendelee kuwa masikini.
Wewe mwenye Akili una impact gani kwenye jamii tu inayokuzunguka, au wewe ni keyboard warrior tu

Hiyo miradi ilikuwa wazi, mbona hata bajeti zake ziliwekwa mitandaoni na vigogo wa serikali walibanwa matumizi yasiyo ya msingi hili fedha zijenge miradi, au wewe ni mgeni hapa nchini

Hao unaosema wameweka uwazi, wamefanya nini mpaka sasa hivi, au wameacha legacy gani....Hao unaowasifia kwa uwazi ndio walioiga watu risasi October baada ya wananchi kudai uozo kwa viongozi.

Usipokuwa na husuda utaelewa nazungumzia nini

Huyo mnaesifia kakaaa anaenda mwaka wa 7 sasa, nitajie project ya maana
 
Maeneo mengi ya yanayoshikikiwa na serikali kwa miradi ya hapo badae bado ni mapori...

Mfano pori la pale sekenke, kwa hiyo wakijenga Ikulu iitwe Sekenke kwa sababu sekenke ilikuwepo kitambo

Hata mitaa ilikuwa na majina hapo awali kabla bado ikiwa mapori, lakini baada ya mtu fulani kujenga na kuwa maarufu hapo mtaa unapewa jina lake

Hata ikulu uitwa jina kwa mujibu wa kitu au mtu au jambo fulani lililopelekea hapo pakawa hivyo.... Mkapa Stadium ulipewa jina la Mkapa kuenzi jitihada zake
Nimekuuliza jina rasmi la kisheria la hiyo sehemu ni lipi?

Hujajibu swali.

Unanipa maoni yako.
 
Back
Top Bottom