Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Kauli zake mbovu za kujimwambafai ndo zinamfanya achukiwe kila kona ! Ukiwa na maslahi naye haya yanayosemwa juu yake utabaki kushangaa
Hivi ni kwa nini mnamchukia sana P.Kabudi? Kwanza Wizara yake haina uhusiano wowote wa moja kwa moja na Upinzani sasa hii chuki kwake inatokea wapi? I mean, mnamchukia Kabudi klk hata Waziri wa mambo ya ndani anayekataza mikutano yenu, kwa nini? Kawakosea nini? Au ni Wivu tuu?
 
Tony254 asante sana kaka, sio tu kimewafurahisha Wakenya, hata mimi Mtzi kimenifurahisha na vile ame deliver meseji yake nimefurahia sana Tony254,
 
Nchi inayojinasibu ya kidemokrasia kama Kenya inaingia kwenye chaguzi na mandate ya viongozi wa kikabila kuungana ili kushawishi kura; badala ya utaratibu wa kunadi sera za chama na mgombea sahihi anaekubalika na wote.

Hawa kweli ndio wa kuifananisha na Tanzania
Kwa hali ilivyo sasa Tanzania, siwezi kamwe kuishutumu Kenya kwa mtindo wao huo wa ukabila, ambao ni mbaya, lakini mtindo wetu wa sasa ni mbaya mara dufu.
Sisi na Burundi, Rwanda na Uganda hatuna nafuu yoyote ya kuwadharau Kenya na ukabila wao.
 
Mada nzima hakuna anayezungumzia kuwepo kwa Kabudi huko. "Building Bridges Initiative' (BBI) inatuhusu nini sisi waTanzania, hadi tualikwe na kuruhusiwa kuhutubia?
Mbona Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, au hata Ethiopia na Somalia hawakuwepo?

Kuwepo kwetu kwenye hadhira hiyo, kunatusaidia nini sisi?

Kwani sis ni bora zaidi ya hao Wakenya, au wametualika kutuonyesha wanavyojitahidi kurekebisha mambo yanayohatarisha umoja wao?

Je, sisi kwa hali ilivyo sasa hivi ni mfano wa kuigwa, au ni watu tunaotakiwa tujifunze kwa hawa wenzetu wanaojitahidi kurekebisha, wakati sisi ndio kwanza tunatumbukia huko wanakojitahidi kupaacha!

Je, amealikwa kwa kuwa "rafiki yetu mkubwa" Odinga ni mhusika mkuu wa mchakato huo?

Je, tunayp maslahi fulani katika mchakato huo, ili kumwinua Odinga rafiki yetu, kwa hali na mali siku zijazo naye aweze kuonja kiti alichotumia maisha yake yote akikigombea?

Kama sababu ya kuwepo kwetu ni hii ya mwisho, wakenya wachukue tahadhari kubwa. Odinga akichukua Kenya hatakuwa tofauti na rafiki yake hapa kwetu. Lakini bahati yao nzuri Kenya ni kwamba, akifuata nyayo za huyu mwenzake, atalitumbukiza taifa hilo katika vita ngumu sana. Walle hawakubali ujinga kama tunavyoukubali sisi.
 
Na wewe umeiamini ile email ya "mwanasheria" isiyokuwa na subject wala letterhead?

Kwa kifupi mumeanguka mtihani nyote ikiwemo TISS yenu, haya mambo mlipaswa kuanza kuyashughulkia kimya kimya baada ya aibu mliyopata Afrika Kusini, ni aibu kupigwa mzinga kwa mara ya pili na huyo huyo mkulima, inaonyesha jinsi gani vitengo vyenu vyote vimelala.

Hivi hivi ndio mtakuta mnanyang'anywa hata majengo ya balozi zenu na mali zilizopo nje, pia pona yenu mlikubali yaishe baina yenu na Barrick japo hamkuambulia chochote cha muhimu, maana mngeendeleza ugomvi nao, kisha waanze kuwadai mabilioni ya dola za Kimarekani, na kwa jnsi mlivyo dhaifu kwenye kutetea hoja zozote, mngevurugwa sana.
 
MK254,
Ndiyo vita ya kiuchumi hiyo, unafikiri kwa nini mkulima hakufanya hivyo kipindi cha Kikwete?
 
Barbarosa ,

..kwa kiwango kikubwa Prof hajakosea kwa yale aliyoyasema.

..tatizo ni kwamba hana " udhu " au uhalali wa kutoa matamshi na maelekezo yale kwa Wakenya.

..Dhuluma na ukatili wa ccm na serikali dhidi ya wapinzani vinamfanya Prof akose "udhu" / uhalali / moral authority, ya kukosoa tabia na mienendo ya wanasiasa na viongozi wa Kenya
 
Ndiyo vita ya kiuchumi hiyo, unafikiri kwa nini mkulima hakufanya hivyo kipindi cha Kikwete?

Kipindi hicho cha Kikwete mlikua mnamlipa, hii deni mumekua mkimlipa sema awamu hii mlianza kwa vurugu nyingi sana na kuharibu mahusiano yaliyokuwepo kote kote, nakumbuka miaka michache ya mwanzo ilikua full vurugu, mara mkamate ng'ombe wetu, mtie vifaranga viberiti yaani visa vingi vya kihuni na chuki, ila naona kama itakua mumeshauriwa kupunguza mihemko, maana siku hizi kidogo mnaonekana kama mumezinduka na kutia akili.

Sasa kwa hili la mkulima, mlifaa mtumie akili na kutafuta jinsi ya kuzima kimya kimya, maana mfahamu huyo ni mmoja tu wa wanaowadai, wengine watapata jeuri hiyo na kuwasababishia aibu zaidi
 
Tabutupu,
I want to categorically state that I listened prof Kabudi speak to Kenyan and through out his speech he spoke well like a stateman.

Prof. Kabudi amezungumza vizuri sana amesisitiza umoja, amani, na mshikamano miongoni mwa watu wa Kenya, wanasiasa na viongozi. Amesema ukabila umezalisha rushwa. Amezungumzia ungwana wa rais Kenyatta na Raila Odinga. Amezungumza kuhusu Nyerere kutokufa kwa ajili ya wema wake. Yote aliyoyazunmza ni mema tu. Sijaona neno bays aliotia kwenye mazungumzo yale. Hivyo acheni kuabambikizia watu mabaya Mungu hapendi
 
pingli-nywee, Kweli, winner takes it all ndio inayosababisha vurugu, lakini sijaona hii BBI iki adress hilo, kuwa atayeshindwa Urais atatulizwa na cheo gani, na hicho cheo kina nguvu gani, maana kwenye Urais ndio kunakoleta kashkash nyingi kwa sababu ya nguvu kubwa ya Urais

Na hili ndio chanzo cha hii BBI
 
Charity begins at home

Kinyume na hapo ni unafiki mkubwa

Kama umeshindwa na huwezi kabisa ndani ya familia yako, kujitweza kwa jirani ni wehu tu.
 
Kati ya watu ambao na amini wanamshauri rais kwa makosa ni huyu Kabudi. ...
Uzur ni kwamba ameshashtukiwa. .. muongo muongo alaf mjivuni sana
Anamshauri Rais vipi kwani ye si Waziri na washaur wa Rais wanafanya kazi gani?
 
binafsi najiuliza ivi ni kweli BBI ndio muharubaini wa UKABILA ktk nchi ya Kenya ? au BBI itapunguza gharama za serikali ? issue ya IEBC ....kwa issue ya ukabila naipa asilimia ndogo sanaaa sababu bado haita adress mzizi wa ukabila ndani ya kenya ... political admistation ndio watafanikiwa zaidi sababu naona hapa wanakwenda kutengeneza mihimili 3 ya dola ss iliyokamilika.. ktk uchaguzi wa KIBRA tuliona issue ya HAND SHAKE ilivyoleta mtazamo tofauti baina ya wabunge ndani ya Jubilee
Kumaliza ukabila sidhani kama katiba itaweza kuwa muarobani, nadhani attitude tu ya watu, hasa wanasiasa kuacha kutumia kabila lao kama kigezo cha kuungwa mkono, hili ni ngumu sana kuondoka, hata Tz ambayo tulisifika sana hakuna ukabila, naona limeanza kujitokeza sana sasa hivi

Mtu kama Rais au makamu wa Rais au kiongozi yoyote mkubwa, kwenda kwao na kuhutubia kwa kilugha chao badala ya Kiswahili au Kiingereza tayari hapo anawaambia indirectly "mimi ni mtu wa kwenu, niungeni mkono''
Hata kama asipotamka wazi wazi, so kuondokana na ukabila ni suala la busara za viongozi na wananchi kiujumla, sio katiba

Pia wananchi wenyewe nao wana wajibu, wana wajibu wa kukataa viongozi wanaotumia kabila kama point ya kuchaguliwa, pia wana wajibu wa kuchunga maongezi yao mtandaoni ama popote ambayo yatakuwa yanaamsha hisia za ukabila
 
Kabudi inaonekana kwa asili yake ni mtu mnafiki, mwongo na mwenye hila. Kwa hali ya sasa, huwezi kuilinganisha Kenya na Tanzania katika demokrasia, uhuru wa watu kutoa maoni yao au hata mshikamano wa Kitaifa.

Ni unafiki wa hali ya juu, kusema eti kuna ubaguzi Kenya kuliko Tanzania. Ni uwendawazimu kumsifia Uhuru kukaa pamoja na Odinga huku akishindwa kumkemea Rais wetu kwa kuhusudu utengano. Tanzania inavunja madaraja ya umoja, uvumilivu na mshikamano halafu kwa unafiki, Kabudu anaenda Kenya kuwalaumu Wakenya wanaotengeneza madaraja ya kuwaunganisha.

Umoja na mshikamano uliojengwa na Mwalimu Nyerere na kuendelezwa na Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete, awamu hii unavunjwa na kuvurugwa vurugwa.

Nawasifu sana Wakenya, namsifu sana Uhuru na Odinga, pamoja na waliyoyapitia lakini wanatembea katika nuru huku wakitafuta nuru zaidi. Mungu azidi kuwabariki zaidi.

Naisikitikia nchi yangu Tanzania, nchi ambayo hapo awali tulikuwa tunatembea katika mwanga hafifu lakini tukiitafuta nuru, ghafla tumegeuka kuelekea kwenye giza totoro. Tunasifu kwa sababu tupo gizani; hatuoni. Tunaimba kuwa barabara ni nzuri sana na mwanga utaonekana hivi punde. Lakini kwa sababu tupo kwenye kiza kinene tunaendelea kusifu kwa vile hatujui wapi ulipo mwanga. Waliotufikisha gizani wanafurahi kwa vile wengi wamepofushwa macho, kwao giza na mwanga hakuna utofauti.
 
Hivi ni kwa nini mnamchukia sana P.Kabudi? Kwanza Wizara yake haina uhusiano wowote wa moja kwa moja na Upinzani sasa hii chuki kwake inatokea wapi? I mean, mnamchukia Kabudi klk hata Waziri wa mambo ya ndani anayekataza mikutano yenu, kwa nini? Kawakosea nini? Au ni Wivu tuu?
Kabudi is one of the hopeless Minister. Yeye ndiye mwenye jukumu la kuionesha taswira ya nchi yetu nje ya Taifa letu. Vitu anavyoongea nje ya nchi ni unafiki wa hali ya juu na upuuzi mtupu.

Fuatilia ile hotuba yake nchini Kenya uone ilivyo ya kinafiki. Unamfundisha mtu aliyevaa suruali na shati namna ya kuvaa suti huku wewe umevaa majani, na baadhi ya sehemu zako za utupu zipo nje.
 
Kwa nini walimwalika kama wanamwona hivyo? Nijuavyo ndo foreigner pekee aliyepewa nafasi ya kuongea, labda kuna wengine sijui lakini, isitoshe aliongea na kutoa maoni yake kama yeye, wewe ulitaka aseme nini labda mazingira kama yale? Ulitaka aongelee Siasa zenu?
Kwa mtu mwenye busara hata kidogo sana, alistahili kuwapongeza Wakenya hatua waliyofikia na wanakoenda. Zaidi angeweza kusema Tanzania inajifunza mengi toka demokrasia ya Kenya, na kutamka kuwa kuna ya kujifunza.
 
Back
Top Bottom