Mkuu
JokaKuu
Wiki moja iliyopita tuliongelea ujasiri wa Mwalimu mwaka 1965 kwa Waingereza na 1964 kwa Wajerumani
Profesa anaonekana kuilinganisha Tanzania ya Nyerere na ya leo, kosa! Mwl alikuwa ''super Diplomat''
Hili suala la EU limeifanya serikali ku-panic sana, na ukweli upo wazi wanaogopa vikwazo
Katika kuogopa wamekurupuka sana
1. Kamati za Bunge la EU zinaongea na Bunge lao,ni mambo ya Bungeni kwao. Tanzania haipaswi kujibu maongezi ya Wabunge. Pale Dodoma Wabunge wakiongea EU haiwezi kuwajibu kwasababu wanaongea kama Watanzania
EU wangejibiwa ikiwa tu suala hilo lingetoka Bungeni na kuwa kauli au msimamo rasmi wa EU kuhusu Tanzania.
Hapo ndipo Balozi, Waziri na wahusika wangetafuta mawasiliano ya kuongelea hili jambo.
Kwasababu ya ku-panic hakuna anayefuata taratibu za kidiplomasia, wanakurupuka tu.
2. Hoja iliyopo siyo misaada, ni matumizi ya Euro Milioni 27. Watanzania hawakujua kuna hizo pesa
Ili kuwajibu EU muda ukitimia (siyo sasa) serikali inapaswa kuwaeleza Watanzania na EU pesa zimekwenda wapi?
Watu hawataki kujibu milioni 27 wanataka tuamini kuna vita ya uchumi! hakuna vita ya uchumi kati ya Wazungu na Waafrika. Tanzania, uchumi wake haupo 'intertwined' na uchumi wa dunia, vita inatoka wapi?
Fuateni taratibu za kidiplomasia, andaeni majibu kuhusu Euro ambazo Watanzania wenyewe hawakujua zipo ingawa leo wanaombwa washikamane !
Mag3 tindo Sky Eclat The Boss