Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Kweli kabisa tunataka Prof Kabudi awafuate huko huko Brussels au amuite mwakilishi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU nchini Tanzania na mabalozi wa nchi wanachama wa EU wenye balozi zao Dar es Salaam awaambie uso kwa uso kuwa wale wabunge wa kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Umoja wa Ulaya " Ni wahuni wachache" wazandiki wanapata wapi uwezo wa kuijadili nchi yetu dona-kantri na Tanzania haibabaiki.

Hapo ndipo tutajua ujabali wa serikali ya Tanzania kuwa nchi huru na haikubali kuburuzwa.
Hapa ndipo ile tabia yao ya ajabu inapojirudia, wakija kwa wananchi; sisi ni matajiri, wakienda kwa wazungu tunaomba Euro 27m kwaajili ya Corona.
 
Zamani nilidanganyika kuwa ukisoma sana unaelimika kumbe siyo, nilimsikia huyu mjinga anamshukuru raisi kwa kumteua na kumtuma ulaya akapata bahati ya kulala hoteli ya nyota tano,

Kuna madogo wengi wafanyabiashara hapo kariakoo hawajaenda shule, utawakuta China, Dubai kwenye five star hotel.

Hao ndo wasomi tunaowaamini Waka negotiate mikataba kwa ajili ya nchi,
Kulala nyota tano kwao Ni archievement
 
Huu "ubabe" wa kuongea na wafanyakazi wa wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, siyo ubabe wa kweli. Mheshimiwa Prof toka hapo wizarani ukifuatana na waandishi wa kimataifa kwenda kuelezea msimamo usioterereka wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba 2020 ili dunia na wadau wa maendeleo wakusikie.

Hii style ya kujifungia umejitenga kimataifa ndani ya jengo lako la wizara lenye madirisha ya nondo na kuwaeleza mabeberu waliopo nje 'hatuwaogopi' haina mashiko.
 
Mtu huyu ni kibudu katika maarifa hata kama ametumia muda mwingi kukaa shule. Sidhani kama ana msaada wowote katika Taifa hili. Mtu huyu na Family Law yake, huenda angekuwa na msaada angeoelekwa ofisi ya ustawi wa jamii akashughukike na mambo ya mirathi na ndoa lakini kwa hapa alipowekwa, ni hasara tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa letu limekosa viongoz waadilifu na wenye huruma kwa wenzao ,100% ya misaada inalenga kwa wananch wanaitwa wanyonge wanaimba wao ni viongoz wa wanyonge ila wanayoyafanya hawana ata chembe ya huruma n hao wanyonge ,binafs naumia kwa sababu najua madhara tutakayoyapata sio wao ,leo hii tunasaidiwa ila bado hali dhoofu je tukikosa kabisa ,viongoz wetu wawafikirie watu wa hali duni wasitake kuwapa mzigo wa makodi na mfumuko wa bei
 
Mkuu JokaKuu
Wiki moja iliyopita tuliongelea ujasiri wa Mwalimu mwaka 1965 kwa Waingereza na 1964 kwa Wajerumani

Profesa anaonekana kuilinganisha Tanzania ya Nyerere na ya leo, kosa! Mwl alikuwa ''super Diplomat''

Hili suala la EU limeifanya serikali ku-panic sana, na ukweli upo wazi wanaogopa vikwazo
Katika kuogopa wamekurupuka sana

1. Kamati za Bunge la EU zinaongea na Bunge lao,ni mambo ya Bungeni kwao. Tanzania haipaswi kujibu maongezi ya Wabunge. Pale Dodoma Wabunge wakiongea EU haiwezi kuwajibu kwasababu wanaongea kama Watanzania

EU wangejibiwa ikiwa tu suala hilo lingetoka Bungeni na kuwa kauli au msimamo rasmi wa EU kuhusu Tanzania.
Hapo ndipo Balozi, Waziri na wahusika wangetafuta mawasiliano ya kuongelea hili jambo.

Kwasababu ya ku-panic hakuna anayefuata taratibu za kidiplomasia, wanakurupuka tu.

2. Hoja iliyopo siyo misaada, ni matumizi ya Euro Milioni 27. Watanzania hawakujua kuna hizo pesa
Ili kuwajibu EU muda ukitimia (siyo sasa) serikali inapaswa kuwaeleza Watanzania na EU pesa zimekwenda wapi?

Watu hawataki kujibu milioni 27 wanataka tuamini kuna vita ya uchumi! hakuna vita ya uchumi kati ya Wazungu na Waafrika. Tanzania, uchumi wake haupo 'intertwined' na uchumi wa dunia, vita inatoka wapi?

Fuateni taratibu za kidiplomasia, andaeni majibu kuhusu Euro ambazo Watanzania wenyewe hawakujua zipo ingawa leo wanaombwa washikamane !

Mag3 tindo Sky Eclat The Boss
 
21 November 2020

WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AWAJIBU MABEBERU, HATUJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI, UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI

Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi aijibu EU - Umoja wa Ulaya kufuatia kikao cha bunge hilo la ulaya huko makao makuu ya EU kutishia uwezekano wa vikwazo kupitia Kamati yake Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili uwezekano wa kuibana Tanzania kwa vikwazo vya aina mbalimbali ikiwemo kusitisha msaada wa kuifadhili bajeti ya Maendeleo ya Tanzania.

Prof. Palamagamba Kabudi ameomba msaada wa vyombo vya habari nchini kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kujitokeza na kuieleza Jumuiya ya Kimataifa ukweli wa mambo. Na kueleza Nyerere aliwahi kuwadindia Germany na United Kingdom na kukataa misaada na fedha zao. Prof. Palamagamba Kabudi anashangaa waTanzania kuanza kutetemeka ktk mitandao ya kijamaii kuhusu nchi yetu kuwekewa vikwazo.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa watu wahuni wachache wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya EU hawawezi kuitisha na kuidhalilisha Tanzania na watambue Tanzania ni nchi huru.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema maneno hayo mazito akiongea na Wafanyakazi wa Wizara hiyo muhimu ya Mambo ya Nje akatumia fursa hiyo kujibu uvumi kuwa Tanzania itanyimwa misaada na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa.

.....................................................

EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania​

Tujikumbushe walioitwa "wahuni wachache" na Prof. Kabudi, tarehe 19 November 2020 jijini Brussels kwa dakika 45 mfululizo walisema nini kuhusu Tanzania ktk kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje cha Bunge la Jumuiya ya EU
Tazama / sikiliza dakika 45 za mjadala ktk kamati hiyo:

Tanzania haijawahi kushindwa vita yeyote? Tanzania sasa inaenda kushindwa vita hii ndipo profesa Kabudi atajutia kauli zake
 
Ana

Ananikumbusha waziri wa Mambo ya nchi za Nije wa Iraq Enzi za Sadam Hussein Mr. Tareq Azioz alikua kiburi sana na mwisho wake ulikua mini?

Sidhani kama Enzi za Mwalimu Nyerere kulikua na watu wasio julikana ambao waliumiza watanzania Hivi
Tanzania ya Mwalimu Sidhani kama ilikua inachukiwa na watanzania Hivi
Let's wait and see
 
21 November 2020

WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AWAJIBU MABEBERU, HATUJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI, UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI

Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi aijibu EU - Umoja wa Ulaya kufuatia kikao cha bunge hilo la ulaya huko makao makuu ya EU kutishia uwezekano wa vikwazo kupitia Kamati yake Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili uwezekano wa kuibana Tanzania kwa vikwazo vya aina mbalimbali ikiwemo kusitisha msaada wa kuifadhili bajeti ya Maendeleo ya Tanzania.

Prof. Palamagamba Kabudi ameomba msaada wa vyombo vya habari nchini kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kujitokeza na kuieleza Jumuiya ya Kimataifa ukweli wa mambo. Na kueleza Nyerere aliwahi kuwadindia Germany na United Kingdom na kukataa misaada na fedha zao. Prof. Palamagamba Kabudi anashangaa waTanzania kuanza kutetemeka ktk mitandao ya kijamaii kuhusu nchi yetu kuwekewa vikwazo.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa watu wahuni wachache wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya EU hawawezi kuitisha na kuidhalilisha Tanzania na watambue Tanzania ni nchi huru.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema maneno hayo mazito akiongea na Wafanyakazi wa Wizara hiyo muhimu ya Mambo ya Nje akatumia fursa hiyo kujibu uvumi kuwa Tanzania itanyimwa misaada na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa.

.....................................................

EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania​

Tujikumbushe walioitwa "wahuni wachache" na Prof. Kabudi, tarehe 19 November 2020 jijini Brussels kwa dakika 45 mfululizo walisema nini kuhusu Tanzania ktk kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje cha Bunge la Jumuiya ya EU
Tazama / sikiliza dakika 45 za mjadala ktk kamati hiyo:

Sawa. Lakini tunakumbuka hali ilivyokuwa mpaka Mwalimu alipoamua kung'atuka na kumuachia Mwinyi. Madukani kulikuwa na majani ya chai tu.

Amandla...
 
😂😂 vituko uchaguzi ulikuwa huru afu bado linasema eti tupo tiali kukaa kukaa katika meza ya mazungumzo kuondoa kasoro ndogondogo😲.

Ndio mibunge ya CCM inasifia serikali kwa bajeti nzuri alafu yanaishia kusema hakuna maji majimbon kwao. Hutaki kuburuzwa unaomba meza ya mazungumzo ya Nini?? Kumpa uwaziri Kabudi ni Mara 2900 angepewa hata MASELLE ambaye ametuwakilisha vyema. Poor kabudi
 
Mkuu uchambuzi wako naona bado unaegemea tu kwenye utegemezi
Lini Africa itajitegemea yenyewe? Mbona akili zetu bado sana kiutegemezi?
In short Prof kasema tu ukweli, sisi ni taifa huru na ni hatutayumbishwa na kusitishiwa misaada
 
Back
Top Bottom