Prof. Kabudi na Tundu Lissu wanastahili kuwa kwenye Serikalli ya Rais Samia

S.M.P2503

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
2,421
Reaction score
4,344
Sijatumwa, lakini ikikupendeza,

Hawa watu waweke kwemye serikali yako. Wataiva tu pamoja, hata kama wana itikadi tofauti.

tuletee watu wa kutupeleka mbele hata kama wanatofautiano kimtizamo.

Chonde chonde, mrudishe huyu mwanazuoni huko serikalini, amekaa bench muda mrefu na ana madini ya kutosha kwa nchi na kwenye baraza lako la mawaziri. Tundu Lissu pia, bila kujali ni chadema, fanya juu chini, muweke serikalini ana mambo mazuri, malumbano yamekuwa mengi, muweke aje kuwa sehemu ya suluhisho sio kila siku ngangara ngarara...na wewe anakuheshimu sana maana hata kule Nairobi ulienda kumuona, hata kataa ukimulika kwenye serikali yako kama kweli ana nia njema ya kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Kwa jinsi ile ile Mtoto wako Paul Bashite Christian Makonda alivyokuombea kule kwenye Bunge la katiba, nami leo nakuja kwa style ile ile. Huyu professor Kabudi na Tundu Lissu usiwaache kwa mustakabari wa nchi yetu.

Nguchiro, mchwa wanaishi ndani na kichuguu bila mkwaruzano.

Mapovu ruksa, mimi sina chama na nawaangalia hawa wawili toka nje ya boksi pamoja na madhaifu ya hapa na pale na ambayo ni ya kibinaadam , chonde chonde Mama, walete waje kusaidia mambo ya nchi yetu. umewaficha sana. Watoe mtondo goo, nchi isonge kwa style ya Mchwa na Nguchiro ndani ya kichuguu.
Walete bila hiyana.

Tundu Lissu hawezi kurubuniwa kirahisi namna hiyo!
Sio kurubiniwa, tunahitaji apewe nafasi na yeye atoe mchango wake kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Anahubiri habari njema za wovoku, na ccm nao yao ni hayo hayo, sasa kama wote wanahubiri habari njema, kwa nini wasikae pamoja kama Mzee Warioba alivyo washauri waje tuijenge nchi yetu bila kugombea fito?
 
Kabudi is just talktive,muongeaje mzuri,ila sio mtu wa kutoa solutions,

Tundu lissu SAWA ungemuombea na Zito kabwe ni watu at least wanaweza kutoa Majibu juu ya matatizo,hii nchi tunahitaji viongozi wa kutoa majawabu/ suluhu Kwa matatizo ya wananchi sio viongozi waongeaji wazuri.
 
Msitutoe kwenye mjadala. Habari ya mjini kwa sasa ni mawaziri wanamtukana Samia.
 
Mmmm j3 sio mbali ila tunapotezwa kuna hoja gani nzito week hizi ??
 
Sijatumwa, lakini ikikupendeza,

Hawa watu waweke kwemye serikali yako. Wataiva tu pamoja, hata kama wana itikadi tofauti.

tuletee watu wa kutupeleka mbele hata kama wanatofautiano kimtizamo.

Chonde chonde, mrudishe huyu mwanazuoni huko serikalini, amekaa bench muda mrefu na ana madini ya kutosha kwa nchi na kwenye baraza lako la mawaziri. Tundu Lissu pia, bila kujali ni chadema, fanya juu chini, muweke serikalini ana mambo mazuri, malumbano yamekuwa mengi, muweke aje kuwa sehemu ya suluhisho sio kila siku ngangara ngarara...na wewe anakuheshimu sana maana hata kule Nairobi ulienda kumuona, hata kataa ukimulika kwenye serikali yako kama kweli ana nia njema ya kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Kwa jinsi ile ile Mtoto wako Paul Bashite Christian Makonda alivyokuombea kule kwenye Bunge la katiba, nami leo nakuja kwa style ile ile. Huyu professor Kabudi na Tundu Lissu usiwaache kwa mustakabari wa nchi yetu.

Nguchiro, mchwa wanaishi ndani na kichuguu bila mkwaruzano.

Mapovu ruksa, mimi sina chama na nawaangalia hawa wawili toka nje ya boksi pamoja na madhaifu ya hapa na pale na ambayo ni ya kibinaadam , chonde chonde Mama, walete waje kusaidia mambo ya nchi yetu. umewaficha sana. Watoe mtondo goo, nchi isonge kwa style ya Mchwa na Nguchiro ndani ya kichuguu.
Walete bila hiyana.

Kabudi tumemuona awamu ya JPM , huyu bwana uongozi hauwezi kabisa kifupi alikuwa exposed kirahisi sana, Professor anafika mahali anasema ametolewa jalalani 😂😂😂 na bado unaona ni kiongozi . Hatuhitaji watu wa kupinda pinda maneno ili kumfurahisha mtawala.

Lissu ni mpinzani mzuri ila si kiongozi , Lissu hana charisma ya uongozi, anakaa kuwa mfundishaji na mkosoaji. Uongozi ni mgumu sana
 
Tundu Lissu hawezi kurubuniwa kirahisi namna hiyo!
Kuteuliwa kufanya kazi ya nchi yako siyo kurubuniwa.
Kama taifa linakuhitaji kufanya kazi furani kwa sababu ya uwezo ulionao ni hiyari kukataa ama kuridhia, lakini si kweli kwamba kila anayeteuliwa amerubuniwa.
 
Sijatumwa, lakini ikikupendeza,

Hawa watu waweke kwemye serikali yako. Wataiva tu pamoja, hata kama wana itikadi tofauti.

tuletee watu wa kutupeleka mbele hata kama wanatofautiano kimtizamo.

Chonde chonde, mrudishe huyu mwanazuoni huko serikalini, amekaa bench muda mrefu na ana madini ya kutosha kwa nchi na kwenye baraza lako la mawaziri. Tundu Lissu pia, bila kujali ni chadema, fanya juu chini, muweke serikalini ana mambo mazuri, malumbano yamekuwa mengi, muweke aje kuwa sehemu ya suluhisho sio kila siku ngangara ngarara...na wewe anakuheshimu sana maana hata kule Nairobi ulienda kumuona, hata kataa ukimulika kwenye serikali yako kama kweli ana nia njema ya kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Kwa jinsi ile ile Mtoto wako Paul Bashite Christian Makonda alivyokuombea kule kwenye Bunge la katiba, nami leo nakuja kwa style ile ile. Huyu professor Kabudi na Tundu Lissu usiwaache kwa mustakabari wa nchi yetu.

Nguchiro, mchwa wanaishi ndani na kichuguu bila mkwaruzano.

Mapovu ruksa, mimi sina chama na nawaangalia hawa wawili toka nje ya boksi pamoja na madhaifu ya hapa na pale na ambayo ni ya kibinaadam , chonde chonde Mama, walete waje kusaidia mambo ya nchi yetu. umewaficha sana. Watoe mtondo goo, nchi isonge kwa style ya Mchwa na Nguchiro ndani ya kichuguu.
Walete bila hiyana.

Unaweza kuwa na hoja. Tatizo sio Rais au kukosa washauri wazuri. Yawezekana mfumo na katiba ndio mzizi wa hali hii mpaka kufikia hatua ya wewe kupendekeza Profesa Kabudi na Lisu wateuliwe.
 
Back
Top Bottom