Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo Habari ndio mnazipenda badala ya kushughulika na Ada na kodi za January
Mabeberu na michezo yao ya kishetani
Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu
Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo
Dawa ya Deni Kulipa, ILA NASHAURI, AVAE YALE MANGUO YA JWTZ, apande nayo ndege mpaka CANADA watamuogopa na kuachilia ndegeWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani
======
NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA
- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa
- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani
#JFLeo
"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.
===
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.
Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.
Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.
Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”
Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.
“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.
Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.
Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.
Mabalozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Abu Dhabi), Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji), Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia) na Dk Jilly Elibariki (Burundi).
Chanzo: Mwananchi
Wee jamaa, mmewanyooshaje sasa??Mabeberu kwisha Habari yao
Tutawanyoonsha
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] unatia huruma balaa
Wapuuzi mnasikia raha sana sasa hivi, etiJamaa naona kashikwa sehemu nyeti
Huu ni uhuni mkubwa.
ACACIA sasa inamtumia mkulima kutuadabisha... hao barik wapo Canada hivyo wanajua nini wanakifanya
Kwaiyo ulikua unasemaje?Tundu Lisu ndio injini behind kukamatwa ndege kanada kupitia kampuni yake ya uwakili aliyoajiriwa.Yeye ndie technocrat wao wa kisheria wa kuikomoa serikali ya Tanzania wa kesi za wadai wa kimataifa wanaoidai Tanzania .Hana uzalendo mjinga mkubwa
Usaliti una gharama zake nadhani Tundu lissu Hilo analijua Kama Yuko tayari kulipa gharama it is okKwaiyo ulikua unasemaje?
Pia hata kuongea naye tu tuonyeshe ustaarabu kwamba tunalitambua deni Hilo na tunaandaa utaratibu wa kumlipa kidogo kidogo. Kumgeuzia kibao mtu anayedai chake hata huku uswahilini si njia sahihi sana!Haya mabaya mengine tunajitakia wenyewe,kwa nini tusilipe madeni ya watu kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa tuachane na usumbufu usio wa lazima?
Sasa mtu muelewa anaweza kuunganisha dots ...sababu ya waziri Kamwelwe kuwaka wakati habari za Dreamliner ya Tanzania kuwasili nchini zilipovuja.“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”