Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Dawa ya Deni Kulipa, ILA NASHAURI, AVAE YALE MANGUO YA JWTZ, apande nayo ndege mpaka CANADA watamuogopa na kuachilia ndege
 
Serikali hii ina hulka ya dhuluma sana hata humu nchini imewadhulumu wazabuni mbali mbali waliokuwa wakiwapa huduma na kwa bahati mbaya jinsi mwenendo wa sheria ulivyowekwa kando kipindi hiki, hawana namna inabidi tu wafirisiwe na mabenki.

Kwa kadri serikali hii itakavyozidi kudhulumu hata haki za raia wake ndivyo watu watakavyozidi kushangilia taarifa kama hizi.

Inatakiwa wajifunze kulipa madeni sio kudhulumu na kwa trend hii watu watastuka sana kupanda hizo ndege kwani hawajui ni muda gani watafaulishwa. Very pathetic indeed.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] unatia huruma balaa

Ni mtazamo wako tu. Lkn kwa mtu ambaye anajua kutumia uwezo wake wa kufikiri vizuri, lazima atajiuliza kwa nini ndege au kitu kingine chochote kikamatwe awamu hii? Je huko nyuma hakukuwa na malimbikizo ya madeni? Fikiria nje ya sanduku la uelewa wako.
 
Tundu Lisu ndio injini behind kukamatwa ndege kanada kupitia kampuni yake ya uwakili aliyoajiriwa.Yeye ndie technocrat wao wa kisheria wa kuikomoa serikali ya Tanzania wa kesi za wadai wa kimataifa wanaoidai Tanzania .Hana uzalendo mjinga mkubwa
 
Daaah hii Sasa imeshakua tabu, tumlipe tu huyu jamaa ili, ndege zetu ziwe na nafasi ya kufanya biashara kimataifa
 
Haya mabaya mengine tunajitakia wenyewe,kwa nini tusilipe madeni ya watu kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa tuachane na usumbufu usio wa lazima?
Pia hata kuongea naye tu tuonyeshe ustaarabu kwamba tunalitambua deni Hilo na tunaandaa utaratibu wa kumlipa kidogo kidogo. Kumgeuzia kibao mtu anayedai chake hata huku uswahilini si njia sahihi sana!
 
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Sasa mtu muelewa anaweza kuunganisha dots ...sababu ya waziri Kamwelwe kuwaka wakati habari za Dreamliner ya Tanzania kuwasili nchini zilipovuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…