Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alipwe pesa yake mambo yaendeleeWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani
NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA
- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa
- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani
"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.
======
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.
Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.
Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.
Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”
Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.
“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.
Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.
Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.
Mabalozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Abu Dhabi), Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji), Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia) na Dk Jilly Elibariki (Burundi).
Chanzo: Mwananchi
Bwashee toa Maelezo yaliyokamilika!
Mkuu umewapatia kwelikweliHizo Habari ndio mnazipenda badala ya kushughulika na Ada na kodi za January
Kuna mambo mengine yanatia hasira .hata kama ni mtanzania anahujumu nchi anafaa kupigwa Risasi akapumzike huko aendako.shenzi kabisa
Wahindi wote wa kisutu kwao ni Canada!“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”Prof Kabudi😆😆😆😅😂😂
Huyu ndiyo mkulima???Jamani watanzania huyo si mkulima, atakuwa mfanyabiashara. Wakulima hawa hawa tunao wafahamu sisi
Bumpkin ni tofauti na pumpkin mkuu!😂 Pole!"The pumpkin of the old homestead must not be uprooted"- Okot P' Bitek in "Song of Lawino".
P
Nasikitika jambo moja tu: waziri wanaonekana kuinyoshea kidole serikali ya Canada! Methinks this is unfair kwa mtu mwenye upeo tena Profesa wa sheria. Hili ni suala la mtu binafsi anajaribu kutumia sheria kupata haki. I stand to be corrected but I think this has nothing to do with government of Canada.
Yafaa mtu huyo mmoja anayelisumbua taifa kufa ili watanzania 54 miliion wanUifaike na miradi ya taifa inayoendelea kujengwa .Acheni kubebesha watu lawama.....lipeni deni
hahahaaaa labda mtawapiga kwa p***mbuHawa mabeberu sasa ufike wakati tuwachakaze kwa mtutu mpaka watuheshimu. Tuwapige kila wakileta chokochoko zao.
Unayemshauri Muoga kama niniMabeberu na michezo yao ya kishetani
Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu
Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo
PovuKwa mfano hata wakikamata for 100 years, wewe unanufaikaje as individual?
...tena babu mwenyewe anaogopa ata kukamata pkpk anatuma moshi akiwa kajificha kilingeni😁😁😁Jamani watanzania huyo si mkulima, atakuwa mfanyabiashara. Wakulima hawa hawa tunao wafahamu sisi ambao ukiwadhulumu wanakuendea kwa babu kukuloga.
Magufuri kawatilia mchanga kitumbua cha Acacia lazima watu surubu wa canadaNgoja huko Canada si ndio kule kwa akina barick na acacia ?
Hawa tushaelewana nao? Waongee na ndugu zao ,ndege irudi
Hapana.Meko ana bahati mbaya