Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Msioijua Singida mnahangaika kweli..Kitila Mkumbo hawezi kugombea S.Kaskazini, huko siyo kwao.Kwao ni Iramba..wanyaturu na wanyiramba ingawa si maadui lkn Mkumbo atapata shida mno kupata kura kule kwa wanyaturu..
 
Hata kwa macho tu hauoni ushindi wa nyalandu na jamaa kashafanya kampeni za kutosha tu ila sins hakika kwamba hapo ndio target nadhani bado kuna target IPO.
 
Hapo ndio naamin vyama vyetu vya siasa viongozi wao wanafikiria kwa makalio badala ya vichwa.... hv mtu kang'atuka hata mwez hujafika then mnampa nafas ya kugombea ubunge ... unazani watajisikiaje wale wafia chama
Siasa ni kama mchezo wa karata mkuu. Ukihisi mwenzako anataka kutupa karata fulani, na wewe unabadili karata unatupa ile unayofikiri itamshinda. Kama hiyo match ni kweli, huoni both parties wanawaweka wasio wafia vyama vyao? Hiyo ndo inaitwa kubadili gear angani mkuu.
 
Karibu mkuu wa wizara anaanzaje siasa wakati hajaomba kuacha kazi?
Yeye ni MTENDAJI wa wizara..... Hapo sheria inamziba mdomo kuongelea politics.

Au wajuzi wa mambo mnasemaje?
Subiri uone. Kwani ukatibu mkuu ulimteua wewe, aliyemteua anaamua atengue match inaendelea kama kawaida. Na baada ya match kama "akikosa" anapangiwa kazi nyingine.
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Dr Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Dr Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Dr Nyalandu. Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

MAONI YANGU
Mimi kete yangu naitupia kwa Dr Nyalandu kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwa bado ana wafuasi wa kutosha kutoka upande wa CCM, hasa wale wasioridhishwa jinsi CCM inavyomwandama Dr Nyalandu na kashfa za kutunga huku wakijua fika utumishi wa Dr Nyalandu haujawahi kuwa na doa lolote.

Je, wewe dau lako unalitupia kwa nani na kwa sababu gani? Toa maoni yako sasa!
Hivi Nyarandu kapata lini PhD, au ndiyo ya Akina Maji marefuu?
 
Kwa hiyo nani mwingine mwenye uwezo wa kuchukua hilo jimbo zaidi ya Nyalandu?
Kwa siasa zilivyo sasa hivi Nyalandu anachukua jimbo lake mchana kweupe
Anaogopa huyo, angependa awekwe mtu weak ili CCM ishinde...
 
Nyalandu ataibuka mshindi kama atagombea ila Kitila Mkumbo naona anaandaliwa kwa 2020 kumng'oa mwigulu Iramba
 
Anaweza kuongea mengi kama haya;
e5a3fcc4727cfd444a17f8306a3c9272.jpg

f5f543ddc6cbba11f388480edce2b1f6.jpg
Ccm wakirejea haya wanaweza wakaamua waweke MTU mwingine ambaye amekuwa mwanasisiem kwa muda mrefu zaidi!
 
Back
Top Bottom