Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Kwa taarifa timu kama hujui Nyalandu hatagombea singida tena anasubilia 2020.

Na kitila mkumbo hvo hvo watachuana na Lisu 2020 pole kwa tetesi zako uchwara.
 
Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani,
1. Mkumbo Kitila HAJAWAHI kuwa na "chembechembe" za UPINZANI. Ni ccm DAMU tangu zamani.
2. Mkumbo Kitila anatoka NDAGO (Singida Kusini), kugombea Singida Kaskazini ni kujitangaza KUSHINDWA kabla ya ushindani kuanza.
3. Itakuwa ni ushindani wa Kitila "aliyeTOKA" upinzani kwenda CCM na Nyalandu aliyetoka CCM kwenda upinzani. Watakuwa wanajibu swali la Paskali wa JF: "Yupi mzuri, shetani aliyebadilika kuwa Malaika, au Malaika aliyebadilika kuwa shetani?"
4. Inawezekana pia wana Singida wakapiga kura "KUMPA ZAWADI TLS" .....
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Dr Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Dr Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Dr Nyalandu. Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

MAONI YANGU
Mimi kete yangu naitupia kwa Dr Nyalandu kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwa bado ana wafuasi wa kutosha kutoka upande wa CCM, hasa wale wasioridhishwa jinsi CCM inavyomwandama Dr Nyalandu na kashfa za kutunga huku wakijua fika utumishi wa Dr Nyalandu haujawahi kuwa na doa lolote.

Je, wewe dau lako unalitupia kwa nani na kwa sababu gani? Toa maoni yako sasa!
Mh!?Dk Nyalandu???rekebisha hapa kwanza mkuu halafu ntarudi!
 
Sasa kwa lip ajiuzuluu km bado anataka huoo ubunge...
Mkuu mbona sababu za kujitoa CCM ameishaziweka wazi au wewe hukuwepo duniani wakati anaondoka CCM? Uliza au fuatilia taarifa kwenye social media, ikiwemo humu JF.
 
Labda Nyalandu aweke D.E.D wake wa kumtangaza mshindi,kinyume na hapo,ajiandae kuangukia pua.
 
Eti nimesikia baadhi ya wanaCCM wanajinasibu kwamba hata akishinda Nyalandu watamtangaza Kitila! Hizi naziona kama dua za kuku.
Sio za kuku Bali za fisi, mkono udondoke niule
 
Kitila Mkumbo Pr, akichukua fomu ya kugombea singida kaskazin , nitakuja kukupigia kampen na ninaamini ndiye mtatuzi wa matatizo hapo.

Pr ,Kitila ni mtu ambaye yupo smart na anafanya research na kutambua chanzo cha matatizo katika utendaji kwa mana
Alipokuwa cdm, cdm ilikuwa moto kwanini jibu ni dogo sana ,huyu mh alikuwa haonekani lakin kazi yake ilikuwa kubwa sana kufanya tafiti na kuwaletea viongozi wa juu wa cdm ,kama Zitto, Mbowe na Slaa.

Pr, Kitila ndiye aliyekuwa anafundisha vijana kujenga hoja pale cdm , na ikafikia mahali hata serikali awamu ya nne kuwaagopa wadogo kama ,Zitto, Mnyika na Mdee. Lkn leo baada ya baba kuondoka angalia uwezo wao ulivyopomoko

Angalia pia Udsm alivyofanya kazi iliyotukuka.


Singida Kaskazin inamhitaji zaid Mkumbo kuliko yeye anavyohitaji
 
Back
Top Bottom