Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Mlimtukana Lissu leo mmeanza kushtakiwa na bado.
Walishtakiwa kipindi kile kile. Hata Kabudi akiwa Waziri wakati Samia alikiri mahali kuwa Acacia wameishtaki Serikali.

Labda kesi zimefika pabaya sasa ndio maana wananyoosheana vidole hadharani maana ndio hulka ya watu wanafiki na wapumbavu.

Tungekuwa na Katiba nzuri na taasisi imara tungewashtaki akina Magufuli, Kabudi, Osoro na wenzao kwa uhujumu uchumi na uzembe. Lakini ndio hivyo wananchi waitwao "wanyonge, wavuja jasho" ndio watabeba hiyo gharama na hasara; na kuendelea kuwahudumia akina Kabudi ustaafu wao wa "kulitumikia Taifa".
 
Ndio maana tunataka na kusisitiza tupate Katiba Mpya.
 
..walifungua kesi wakati yupo hai.

..umesahau ndege zilikamatwa mara ngapi wakati Magu akiwa madarakani?

..umesahau kwamba acacia walifungua kesi wakati Magu akijadiliana na barrick?
Walimalizana na mpaka Boss wao akaja Ikulu Dar na inasemekana hao acacia wakakubali watalipa baadhi ya pesa walizotakiwa kulipa !
 
Hahahahaha wanamkana Marehemu? Lissu alisema akaitwa kibaraka?
 
Ndege si zilikamatwa wakati akiwa hai madarakani, au unajizima dat?
Nakumbuka zilikamatwa kwa madai mengine ya mikataba tofauti sio ya madini ! Lakini mimi Twendeni tu mnavyotaka maana kwa sababu ya baadhi ya watu kumchukia Magu basi mpo tayari hata kuwatetea wanyang’anyi wanaotaka kupiga pesa za Nchi bure bure tu eti kwa sababu ya kumkomoa Mwendazake !! Yule alishakwenda harudi tena ! Tuzitetee mali za Nchi angalau watoto wa masikini wa Nchi hii waweze kupata unafuu katika maisha yao. !! Yule alishaenda for good tuache ushabiki wa Simba na Yanga kwenye mali za Nchi πŸ™πŸ™πŸ™
 
Ujamaa na waamini wa ujamaa ni watu hatari sana, ubabe wa kijinga na hii bado upo sana.

Ila viongozi wa Africa ni watu hatari sana wakikuzunguka... bahati mbaya sana Magufuli hakuwajua wabaya wake.

Walikuwa wanamchekea huku wanafurahia perdiems..
Huwa sitaki hata kuwaona wakati wowote,ni watu wa mihemko,jazba na wakurupukaji wanaotaka Kuendesha mambo Kwa Imani badala ya facts na analysis..

Ni watu hatari sana wanaweza sababisha maafa makubwa ndio maana wakitokea Dunia inawawahisha kuzimu kabla ya kuharibu zaidi..
 
Huna hata uwezo wa kuthibitisha dai lako hata Moja..Wajamaa ni watu wajinga sana nyie.
 
Nani alithubutu kusema haya ukiacha Lisu ambae aliponea kifo? Unajizima data si ndio? Inahitaji kujitoa mhanga na sio Kila binadamu ana huo ujasiri
 
Kwanini hakumshauri Magufuli hivi anakuja kuleta umbeya sasa??
Wewe ungeweza kumshauri Magufuli? Ulikuwa unamjua vizuri au unamuona kwenye tv? Kamuulize Mpango atakupa wasifu wake πŸ˜„πŸ˜„
 
Si wanapima upepo yule ameshtaki Amelipwa kwa nini mimi nisishtaki ili nilipwe wanaangalia na aina ya rais na utawala uliopo
Alipolipwa haraka haraka Symbio mabilioni nikajua tayari mchezo umeshaanza !! Wajanja kazini ! Na watu wanashabikia eti wanafikiri wanamkomoa Mwendazake πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hii nchi kila mtu husubiri hadi jambo liharibike kisha aanze kunyooshea wengine mkono...

Nilitarajia mtu kama Kitila sasa aoneshe mfano kwa kupigania katiba mpya ili isijetokea tena mtu anayeweza cheza na hatma ya taifa...
Ndio madhara ya kunyima forum watu kuongea ,waliosema kuzuia watu kuongea kunahatarisha usalama wa Nchi sio wajinga..

Siku upenyo ulitokea Nchi inavurugika ndio hayo ya Sudan,Rwanda,Burkina Faso,Libya nk nk
 
Kwa mfano Mpina anajaribu kusimamia ukweli japo amejiandaa Kwa lolote ,so tungekuwa na Wanasiasa wengi wa hivyo ujinga ujinga usingekuwepo.
 
Unawajua Watzn vizuri? Watzn walio wengi kwenye Uongozi Ukiwa unamshauri anaona wewe ni threat kwake Kwa hiyo hawezi fanyia kazi Ushauri wako..

Unadhani Jiwe aliposema ukinishauri ndio sifanyi aliongea uongo? Ndio hulka za Watzn hizo Kwa taarifa Yako
 
kwa sababu ya baadhi ya watu kumchukia Magu basi mpo tayari hata kuwatetea wanyang’anyi wanaotaka kupiga pesa za Nchi bure bure tu eti kwa sababu ya kumkomoa Mwendazake !! Yule alishakwenda harudi tena !
πŸ”Œ
πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…