..huko ICSID hatuwakilishwi na mawakili toka hapa Tz.
..kuna taratibu zake za kumpata msuluhishi ambaye anaaminika na kukubalika na pande zote kusikiliza shauri.
..ofisi ya mwanasheria mkuu kazi yake ni kutoa ushirikiano na supporting evidence / documents kutetea upande wa Tanzania.
..tatizo huwa linaanza hapa nyumbani kwa viongozi wetu kujifanya wababe na kukiuka mikataba waliyosaini.
..Matokeo ya ubabe wa viongozi wetu ni kushindwa ktk mashauri mengi yanayopelekwa ICSID.
..Kama tunataka tusipigwe basi tuhakikishe tunatengeneza mikataba inayotulinda, na baada ya hapo tuiheshimu.
..Jambo lingine, ambalo ni gumu, na serikali inaogopa kulifanya, ni kujitoa ktk mikataba inayoelekeza kwamba migogoro na wawekezaji itakwenda ICSID, au uwekezaji hapa nchini italindwa kupitia MIGA. Hali hiyo itaondoa uwezekano wa Tanzania kushtakiwa huko nje.