Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Mpango upi wakati wanadai cost za damages!! kilichobakia ni utekelezaji wa uhukumu sio kupewa leseni. Yaani miaka 5 Sasa hajachimba kitu Leo alainike kisa amerejeshwa nchini? Zile cost za miaka 5 atazifidia nani?

Haya makampuni kweli ni yakinyonyaji lakini ni CCM wenyewe mmeingia hii mikataba so mnapoivunja msitumie ujuaji maana hela za hongo mmekula alafu mnakiuka makubaliano mnategemea Nini?
Unaweza kuleta ushahidi ata wa picha kuonyesha hiyo migodi ikiwa imeendelezwa ata kidogo.
 
It doesn't matter, makubaliano ni makubaliano. Kama mlijua mkataba wa kihuni kwanini mslisign? Yaani mnakubaliana alafu baadae unakuja kukiuka makubaliano. Lazima ulipe fidia!!

Kuna procedure, ni sawa na mtu hajachukua Hela benki miaka 5 waka assume amekufa kumbe yupo nje ya nchi. Siku anarudi anataka Hela zake unadhani hatoshitaki?

Zimefutwa sababu ya regulations kubadilika na ndio kesi ya msingi Iko hapo. Kwanini ulete sheria mpya alafu unataka compliance kwa leseni ambazo umeshatoa na muda wa kuhuisha bado. Mlikubaliana say standards Fulani alafu baada ya miaka 3 uje na regulations mpya zenye standards mpya then una revoke licence kisa mtu Hana vigezo vipya!! Mahakamani utaanguka tu.
Hizo leseni wengine walipata toka enzi za Mkapa na hakuna cha maana walichofanya.

Achilia mbali sheria na regulations mkataba pia una ‘performance clause’ umepewa eneo uchimbe madini; sio ulihodhi tu.

Uwezi kazi kwanini uachiwe umiliki tu, hizo kesi watashindwa sio kwa sababu serikali ilikosea, wameingia na kuvuruga strategy waliyoikuta na kufanya mambo kwa staili wanayoijua wao wenyewe.
 
Tatizo la Watanzania huwa wanarukia sentesi moja na kuipa uzito mkubwa badala ya kusoma taarifa nzima inalenga kuzungumzia kitu gani.

Nina hakika Prof. Kitila kaeleweka vibaya kwa sababu, hoja yake hakuzungumzia kesi hizi zimetokana na makosa ya kuwanyang'anya liseni Wawekezaji bali hoja yake ni Ushauri uliotolewa wakati wa kusaini mikataba ya madini miaka ya nyuma na sasa.

Makosa haya ndio yalosababisha leo tuna kesi hizo 3 akilenga uwepo wa madini adimu kabisa ambayo Marekani walienda South katika mkutano wa madini na kueleza malengo yao. Hii ni tahadhali kwetu juu ya maamuzi na Ushauri atakao pewa rais.

Akatahadhalisha zaidi kuwa madini hayo tunayo na tuwe makini sana haswa washauri wa rais wamwelekeze vema na sii kwa Ushujaa wa kibabe tukatoka na ZERO! Mfano wa wasomi wanao disco!

Hizi lawama zote kwa Prof. Kitila sijui kina Paramagamba ni mchepuko wa kuondosha hoja muhimu sana aloweka Prof. Kitila kuhusu mikataba mipya ya madini ambapo alikuwa akiunga mkono bajeti ya wizara ya Madini lakini akiongezea kuwa hizo asilimia 16 za sheria mpya tulonayo hazijatosheleza kabisa mchango wa sekta ya madini nchini.

Hizi kesi 3 kati ya 7 mnazopigia kelele ni mpango mpya wa Wawekezaji hao warudi nchini. I bet, watarudishwa kama ilivyo Symbion na Wawekezaji wengine kina IPTL walofungua kesi zao za madai ndani na nje ya nchi ili wapate kurudi katika Biashara zao.

Hakuna jipya chini ya jua..
Na Uwezekano wa kuendelea kupigwa kama kawaida yetu upo palepale !!
 
Hizo leseni wengine walipata toka enzi za Mkapa na hakuna cha maana walichofanya.

Achilia mbali sheria na regulations mkataba pia una ‘performance clause’ umepewa eneo uchimbe madini; sio ulihodhi tu.

Uwezi kazi kwanini uachiwe umiliki tu, hizo kesi watashindwa sio kwa sababu serikali ilikosea, wameingia na kuvuruga strategy waliyoikuta na kufanya mambo kwa staili wanayoijua wao wenyewe.
Kesi za namna hiyo kwa wenzetu wengine wasio na uzalendo huzitumia kama ni Fursa !! Na ndicho tunacho tahadharisha !! Lakini huenda tunajisumbua tu maana Uzalendo uliobakia ni msamiati wa kizamani !!
 
Ni muhimu kwanza kutambua kesi hizo 7 ni za madai gani? Kama mtakumbuka ndege yetu ilizuiwa Canada na South kwa madai ya mwaka 1974. Je, hilo lilikuwa kosa la nani?
Mkuu ngoja nikueleweshe... Hayo madai ya toka mwaka 1974 yalikuwa yakilipwa kidogo kidogo kila mwaka,
Mwinyi alipunguza, Mkapa alipunguza, Kikwete alipunguza..

Sasa tukapata eti mzalendo no moja.. Akakataa.....
Kuna kesi imeisha juzi juzi, Serikali itatakiwa kulipa Billioni 290 ..kama sikosei.. Na kosa lilifanyika 2016 kwa Serikali kuchukua ardhi kwa nguvu maeneo ya Bagamoyo na kumpatia Bahresa kujenga kiwanda cha sukari..

Ile ardhi ilikuwa ya mwekezaji wa nje.. Jiwe akatuma wasaidizi wake wakafyeka kila kitu kwenye hiyo ardhi..Kisha wakampa hati mpya Bahkresa..

Hapo yote yanafanyika kwa Jiwe mwenyewe na washauri wanampamba bila kujua kwamba watu wakienda mahakamani itakuja kuleta hasara kwa Serikali
 
Kitila Mkumbo hakuwa katika serikali muda huo?

Katika kanuni za "collective responsibility", unapokutana na uamuzi mkubwa ambao hukubaliani nao, una mambo matatu ya kufanya.

1. Unaweza kujenga ushawishi wa hoja kwamba yakataliwe katika uamuzi wa pamoja.

2. Ukishindwa kujenga ushawishi huo, unaweza kuyakubali maamuzi, na ukishayakubali, wewe mwenyewe unakuwa sehemu ya maamuzi. Lawama zozote zinazotokana na maamuzi unastahili kupata, kwa kuwa wewe ni sehemu ya maamuzi pia.

3. Kama unaona mambo haya ni mabaya sana, na huwezi kujenga ushawishi yakataliwe wala kuyakubali, unaweza kujiuzulu cheo chako utike serikalini, ili usiwe sehemu ya maamuzi hayo na uweze kuyapinga kwa uhuru nje ya serikali, au kama backbencher (mbunge asiye waziri, naibu waziri, spika, naibu spika, au AG) bungeni.

Sasa, naomba uhakiki kwa watu wenye rekodi nzuri, Dr. Kitila Mkumbo alikuwapo au hakuwapo serikalini wakati haya madudu ya makinika yanaendelea?

Kama hakuwapo serikalini, aliyapinga lini na wapi?

Kama alikuwapo serikalini, alichukua uamuzi gani kati ya maamuzi matatu hayo hapo juu?
 
Kesi za namna hiyo kwa wenzetu wengine wasio na uzalendo huzitumia kama ni Fursa !! Na ndicho tunacho tahadharisha !! Lakini huenda tunajisumbua tu maana Uzalendo uliobakia ni msamiati wa kizamani !!
Kitendo tu cha kukosoa hatua za serikali hadharani ni makosa it doesn’t matter raisi angekuwa Lissu, Zitto, Magufuli, Samia or whatever.

Wanasiasa wa nchi yeyote na wa vyama vyote standard of behaviour ni kuweka national interest fist, wanyukane kwenye mambo mengine.

Clearly mtu ana conditional/repudiatory breach ya mkataba, amefungua kesi kwenye mahakama za uonevu. Badala ya mtu msomi kusoma sababu za hiyo mikataba kufutwa alichoangalia ni nchi imeshitakiwa na kwenda kuropoka bungeni.

Kwanini tusione anatafuta fursa, inawezekana kabisa anafanya lobbying kwa niaba ya wawekezaji walipwe apewe chake.
 
Hapana sisi wengine tunajaribu kutahadharisha tu kwamba tusishabikie Nchi kunyonywa na Mumiani kwa kisingizio cha jamaa yule alifanya makosa !! Yapo makosa aliyafanya lakini na Wakora huwa wanachukuaga advantage ya kuingiza madudu yao !! Ndicho kitu ninachojaribu kutahadharisha Mkuu !
Hao Wakora wataje..
 
Mimi namfahamu vizuri nimefanya nae kazi nilikuwa simwogopi nilimwambia ukweli akanifukuza nchi kwa kutumia mawaziri wake hakudhubutu kuniambia mwenyewe kwa hiyo alikuwa ananiogopa kwa uwezo wangu na sio upumbavu
Na wewe ulifungua kesi ya kuvunjiwa mkataba ?
 
Kitendo tu cha kukosoa hatua za serikali hadharani ni makosa it doesn’t matter raisi angekuwa Lissu, Zitto, Magufuli, Samia or whatever.

Wanasiasa wa nchi yeyote na wa vyama vyote standard of behaviour ni kuweka national interest fist, wanyukane kwenye mambo mengine.

Clearly mtu ana conditional/repudiatory breach ya mkataba, amefungua kesi kwenye mahakama za uonevu. Badala ya mtu msomi kusoma sababu za hiyo mikataba kufutwa alichoangalia ni nchi imeshitakiwa na kwenda kuropoka bungeni.

Kwanini tusione anatafuta fursa, inawezekana kabisa anafanya lobbying kwa niaba ya wawekezaji walipwe apewe chake.
Fursa !!
 
Prof. Kitila Mkumbo anadai Tanzania imeshtakiwa na makampuni ya madini, na mashauri hayo yanapelekea serikali kuingia hasara.

Prof anadai Wasomi walitoa ushauri ili kuwafurahisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli kuhusu madhara ya kuvunja mikataba ya kimataifa.

Haya ni matokeo ya kuingiza siasa kwenye mambo ni kitaalamu.
 
Na ukojitoa, hakuna mwekezaji atakayekuja Tanzania kwa sababu mahakama zetu hizi za uzalendo wa Rais, haziaminiki.

..wengi wametoa maoni kwamba kama hatutaki kupelekwa ICSID, MIGA, etc, basi tutangaze kwamba tumejitoa na hatutambui vyombo hivyo kama alivyofanya yule jamaa wa Bolivia.
 
Kuna ajabu kushtakiwa ukipigania haki zako?

..unapigania vipi haki bila kufuata sheria na taratibu zilizowekwa?

..Magu alidai wataalamu wake wamegundua wizi wa Usd 191 billion, sasa utaratibu ulikuwa kupeleka ushahidi huo MAHAKAMANI ili tupate haki yetu.

..kiongozi anayekubali kulipwa usd 300 mil wakati anadai ameibiwa usd 191 bill unaamini anapigania haki? Kiongozi wa aina hiyo ni mzalendo kweli, au mbabaishaji?
 
..wengi wametoa maoni kwamba kama hatutaki kupelekwa ICSID, MIGA, etc, basi tutangaze kwamba tumejitoa na hatutambui vyombo hivyo kama alivyofanya yule jamaa wa Bolivia.
Hata ukijitoa bado utawajibika kwa miaka kumi zaidi that’s what we call sunset clause kwenye mikataba ya BIT and am not referring MIGA which is an insurance that an investor has to have to protect thier investments so please 🙏🏿 you need to educate your self before you take the risk of investing in Tanzania
 
Walimalizana na mpaka Boss wao akaja Ikulu Dar na inasemekana hao acacia wakakubali watalipa baadhi ya pesa walizotakiwa kulipa !

..madai yetu yalikuwa usd 191 billion.

..tukakubali barrick watulipe kidogo kidogo usd 300 million.

..sasa jiulize kama huo sio ulaghai na ubabaishaji.

..mimi nahisi Magu na genge lake walichukua RUSHWA toka kwa Barrick.
 
Ndio maana tunasema tusikubali kuwa na ushabiki kama wa Simba na Yanga katika masuala ya rasilmali za Nchi !!
 
Back
Top Bottom